TASFIRI YA NDOTO UNAZOOTA USIKU UKIWA UMELALA
NDOTO ZOTE unazo ota zina maana siyo bahati mbaya tu ,au uchovu tu au mawazo yako tu.
NDOTO ZOTE zimebeba maana na ujumbe kwako..na ni KWELI ni halisi ,,ndoto unazo ota usizipuuzie ..
NDOTO MBAYA
1) Kukimbizwa na watu,au wanyama,au ndege hata kama ni kuku tu anakukimbiza.
(Maana yake unawindwa unakimbizwa na nguvu za giza ili zikudhuru.)
2)Makaburi kuona upo makaburi..na ndoto za mauti mauti--Roho ya mauti
3)Kuumia mkono,kukatwa au kuumizwa mkono..kama ni wa kulia (wingi wa siku) wanataka kuku ua
kama ni mkono wa kushoto(heshima na utajiri)--wanataka usifanikiwe.
4)kujiona huna nguo au viatu,au upo kwenye maji machafu,..au unakanyaga kinyesi..umezungukwa na vinyesi..au upo mtupu bila nguo...ni mbaya wanataka kukuondolea kibali,AIBU ,pia ni dhambi za kutubu..
5)upo mazingira ya shule ya msingi,unafeli mitihani,umechelewa mahali,umeachwa na gari,upo mazingira ya kijijini porini,unapanda mlima lakini hufiki kileleni unapanda kwa shida,unakimbia lakini hufiki ,unaanguka shimoni,..umefungiwa kwenye chumba huwezi kutoka,ama unakimbia lakini unazunguka hapo hapo hupigi hatua ,au mbio zako ni ndogo kama mtoto mchanga huna nguvu za kikimbia kwa speed haraka
6)kupigwa mishale kuchomwa kisu,kupigwa risasi,kulishwa chakula ndotoni,..kufunga harusi ndotoni,ama kuzini ndotoni,kunyonyesha ndotoni,kuwa na watoto ndotoni..,kuona wanyama kama nyoka,simba,mamba ,chura mijusi
7)kunyolewa nywele ndotoni,..uko porini..,viumbe wa kutisha kupigana ndotoni ukapigwa ukaumizwa..kuota upo baharini..,unazama kwenye maji,..unavalishwa pete,kula nyama mbichi au iliyopikwa au chakula ndotoni,kulimishwa
na kufa ganzi ndotoni yani huwezi kuongea sauti haitoki ,na huwezi kujisogeza hata kutingishika,kukaliwa na kitu cha baridi unahisi mtu amekukalia wa baridi ametoka kuruka na ungo nje kwenye baridi kaja na baridi yake kukukalia mwilini huwezi kujitingisha(Unakabwa ndotoni)
NDOTO NZURI
1.)kunyesha MVUA kukunyeshea, mvua,KUVUNA mazao,matunda
2)Unapiga mtu ndotoni anakimbia unamshinda,kama ni mnyama wewe unamkimbiza ,kama ni mjusi unapiga ukamuua,kama ni nyoka ,unachinja unakata kichwa,
3)upo kanisani unasali au upo nyumbani unasali unasema wachawi waungue kwa jina la yesu,unawaona wachawi wanaungua hapo dirishani kwako au waliopo ndani wanaungua wanapiga kelele wanalia mamaaaaa mamaa tunaungu aa aaa motoooo...motooo wa Yesu...unatu unguzaaa uwiiii uwiiiiii mamaaaa maaaaaa
4)kuota unapaaa angani..unaruka juuu..unakimbia mbioooo kwa haraka hakuna wa kukufia...
5)kumuona mtu mweupe anga ng'aaa kama jua anakuambia tubu dhambi zako ufalme wa Mungu umekaribia nakuja kukuchukua....malaika na Yesu kuwaona ndotoni...ukakabidhiwa fimbo ina ng'aa na upanga ,na mabundiki na nguo za kijeshi..kuwa mwanajeshi upo jeshini..unaendesha vifaru vya vita..,unaendesha magari ya kifahari,na ndege unarusha angani
mabegani una manyota nyota vyeo..
6)UNAOGA bafuni au mtoni, maji masafi unafua nguo zako(KUTUBU dhambi kusamehewa dhambi na kuziacha kutakaswa)
UKIOTA NDOTO MBAYA CHUKUA HATUA USIDHARAU.
Mikono yako ina maana ukiota umeumia mkono au mkono umekatika au hata mguu vyote vina maana
hebu angalia hapa maana ya mkono ni nini?mana wengine wanaota wame umwa na mbwa mkono au mkono unatoa damu au umekatwa kabisa,au miguu anaota hana viatu...au unaota umezungukwa na vinyesi unakanyaga vinyesi...au huna nguo..au umevaa nguo zimechakaa,au unakimbizwa..,au umechomwa mishale ,au umepigwa risasi...au unaota mjusi amechukua nywele za kichwani kwako...au unapigana unapigwa...hizi ndoto mbaya inatakiwa uchukue hatua ya haraka,mwingine anaota yupo makaburini kila siku,au porini kwenye mibuyu amefichwa ,au amevalishwa pete za kipepo vidoleni japo kwa macho hazionekani ila rohoni umevaa pete..
maana ya mikono
Mit 3:16
Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto
mkono wa kulia =wingi wa siku(kupitia mkono wako wa kulia mtu akikufanyia nguvu za giza anaweza kukuondoa duniani kabisa)
mkono wa kushoto (heshima na utajiri).
na mambo yote ili yatokee yanaanzia ndotoni kwanza.
NDOTO siyo za kupuuzia,ndio maana wakati mwingine unaweza ukaota ndoto moja INAJIRUDIA hata mara tatu kwa siku ,na siku zinazofuata unaota ndoto hiyo hiyo.
LENGO uchukue hatua ,ili KUZUIA mabaya ya sikupate.
Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
maarifa ni kumjua Mungu kuwa na IMANI kwa Mungu,NENO la Mungu ambaye lina nguvu,lina uhai,lina ukali kama upanga..
uwe na uhakika Mungu yupo ndani yako ,ana nguvu huyu NENO ya kufanya jambo lolote,USIOGOPE.tumia mamlaka ya NENO la Mungu na imani yako kukanyaga nyoka ,nge ,simba na mwasimba na joka na nguvu zote za yule adui wala hakuna uovu wowote wala chochote kitakachokudhuru.
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako hautafanikiwa,...hutakufa bali utaishi na utayasimulia matendo makuu ya MUNGU...