Faida/Changamoto za biashara ya Mabasi

Faida/Changamoto za biashara ya Mabasi

Biashara ya bus kama huna roho ya paka lazima ufe presha, kwa miaka hii sio biashara ya kusena ujaribu inabidi ufanye utafiti wa kutosha ujiridhishe la sivyo utakula za uso...
Wengi waliopata faida nzuri ni wale waliofanya hii biashara miaka ya nyuma, hivi sasa ushindani ni mkubwa mno, usishangae bus kusafirisha hata abiria wasiozidi 15
ila nakukumbusha hakuna biashara isiyo na faida wala hasara, hata kipindi hiki kuna kampuni zinaleta mabus mapya kabisa
 
Afrolink-Tz Consult Ltd

Mkuu mimi nipo kwenye tasnia hii muda mrefu najua wapi nipeleke basi gani na la aina gani na wateja wangu wakina nani.pia mimi ni mmiliki wa vyombo hivi vya usafirishaji abiria
 
Wakuu hiv zile Eicher ama Tata zinazo piga ruti katika jiji la Dar es Salaam ni bei gani ikiwa mpya?
Tata mpya ni 115m, hapo utatakiwa kutengeneza carrier na kupaka rangi. Gari inatoka na rangi nyeupe. INA kuwa pia na sehem ya kuwekea TV na music system
Gari hizi zina matumizi mazuri ya mafuta. Tatizo hazipendi milima, rough road, zina matatizo ya Umeme usipokua muangalifu. Mafundi wa gari hizi wapo kwenye kampuni yao
 
Tata mpya ni 115m, hapo utatakiwa kutengeneza carrier na kupaka rangi. Gari inatoka na rangi nyeupe. INA kuwa pia na sehem ya kuwekea TV na music system
Gari hizi zina matumizi mazuri ya mafuta. Tatizo hazipendi milima, rough road, zina matatizo ya Umeme usipokua muangalifu. Mafundi wa gari hizi wapo kwenye kampuni yao
 

Attachments

  • IMG_20170716_101039_479.JPG
    IMG_20170716_101039_479.JPG
    18.3 KB · Views: 174
abiria ndio huwa mnaamini kila gari lazima lina makafara lakini si kweli kabisa
Hili unalolisema ni kweli. Binafsi nilishawahi kufanya biashara ya daladala. Safari za Mwananyamala-Ubungo; Tandika-Gongo la Mboto na Kariakoo-Ubungo. Sasa kuna nyakati gari zilikuwa hazitulii barabarani yaani kila mara majanga. Mara trafiki, mara inasumbua hiki, mara ajali. Daah, basi wale madreva kwa kuwa nilikua na umri mdogo na wengi wao watu wazima ikabidi siku waniite waniweke chini na kuniambia masuala ya shirki wakidai kampuni ishaingiliwa na "mdudu". Daah nikawakatalia. Lastly nikaona wanazingua tu. Nikauza mabasi yote 10. Nilianza na daladala moja hadi 10 ndani ya miaka 3 tena si kwa kukopa.
 
Mkuu hili mm sio mjuzi. Masuala haya ninkwa mujibu wa wenyewe wamiliki na wafanyabiashara hizo
sawa sawa . mkuu katika web za mabus nmeona zhongtong climber ni 98500usd CIF cost. sasa inakujaje 400mil kama ndo cost ya bus hadi liwe barabarani. inamaan ushuru tra wa climber ni zaidi ya 120mil?
 
Shukrani kwa huu uzi.
Naomba kufahamu yafuatayo:
1.kwa Dar, bus zipi ni bora kununua kwa ajili ya daladala?
2.ukiwa na bus za daladala zaidi ya 3,tumeshauriwa tufanye biashara ya spare?
3.tutajuaje nyota ya chuma? Ni miezi ya kuzaliwa au mpaka tuende kwa consultant wa hayo mambo
 
Back
Top Bottom