Hili unalolisema ni kweli. Binafsi nilishawahi kufanya biashara ya daladala. Safari za Mwananyamala-Ubungo; Tandika-Gongo la Mboto na Kariakoo-Ubungo. Sasa kuna nyakati gari zilikuwa hazitulii barabarani yaani kila mara majanga. Mara trafiki, mara inasumbua hiki, mara ajali. Daah, basi wale madreva kwa kuwa nilikua na umri mdogo na wengi wao watu wazima ikabidi siku waniite waniweke chini na kuniambia masuala ya shirki wakidai kampuni ishaingiliwa na "mdudu". Daah nikawakatalia. Lastly nikaona wanazingua tu. Nikauza mabasi yote 10. Nilianza na daladala moja hadi 10 ndani ya miaka 3 tena si kwa kukopa.