Nafuga kienyeji, ukitoa running costs zote per month sikosi Tshs 1,200,000 kama faida.
Binafsi nauza mayai Tshs 15,000/trei na kwa siku nauza mpaka trey 3 kwa wastan jumla kama 45,000/day. Natotolesha vifaranga around 600 kwa mwezi na kila kifaranga nauza Tshs 2,000 hapo ni wastani wa 1 mpaka 1.2 m.
Ukitoa gharama za chakula, dawa (vitamins, chanjo etc) kwa mwezi sikosi 1.2 mpaka 1.3 m kama faida.
Soko la vifaranga pamoja na mayai ya kienyeji liko wazi. Ni kuweka mkakati pamoja na kusimamia mwenyewe kama unaweza.
Kinachokubeba ni uuzaji wa vifaranga na si nyama wala mayai...na fauda ya vifaranga ni swala la muda tu pia iyo biashara itakufa..unaless uwe unaifanya kwa udogo sana.
I am speaking this from experience
Utagaji wa kuku wa kienyeji ni mdogo, utagaji wao ni almost 45% ukilinganisha na layers ambao utagaji wao unafika 90%>
Kwa maana iyo unahitaji uwe na matetea 100 ili upate mayai 45 (tray moja na nusu) kwa siku. So kwa trays tatu unazopata kwa siku naamini unamatetea yenye umri wa kutaga 200. (Only matetea 90 yanataga kwa siku huku matetea 110 yakiwa yamepumzika) ikumbukwe kuna majogoo pia kati yao.
Kwa idadi iyo ya kuku huna faida ya maana unayoipata. Wanachozalisha ni kidogo kuliko wanachotumia. So kwenye upande wa mayai mkuu hunaunachovuna.
UPANDE WA VIFARANGA:
This is the best business..nimekuwa mzalishaji wa vifaranga kienyeji na chotara kwa takribani miaka 10 kabla sijaachana na iyo biashara.
Nilikuwa capacity yangu ilikuwa ni vifaranga 2000-2500 kwa week. Faida ni kubwa sana hata ukiuza kifaranga kwa 1200 tu.
Ila iyo ni swala la muda tu. Kuku wa kienyeji na chotara hutumia miezi 4-6 ili kufaa kwa nyama. Na endapo mfugaji akiamua kuwatunza kwaajili ya mayai, hutumia miezi 24 mpaka kuzeeka.
Kwaiyo ukiwa mzalishaji mkubwa, atleast from vifaranga 1000 na kuendelea kwa week, unatakiwa kila week ya uzalishaji uwe na mteja mpya. Maana mteja wako wa leo usimtegemee kesho..maana anahitaji miezi kadhaa kuphase out stock aliochukua.
Haiwezekani kupata mteja mpya kila week. Hapo utalazimika kuanza kutumia madalali ambao watakuja na bei zao wanazoona zinfaa....ukisema ubaki nao, huwezi kumudu kulisha vifaranga 2000 kila week..unless uwe giant sana na unamiundominu ya kutosha.
Ukifika level hii ndipo tunapostalk. Business model ya uzalishaji wa vifaranga inakuwa imefia hapo
AWAY FORWARD:
Kuku wa kisasa ndo the only feasible busines kwenye angle zote.
Ukiwa mzalishaji wa vifaranga vya broiler, mteja wako atarudi kila baada ya wiki 4-6. Ukishakuwa na base ya wateja 50 tu wa vifaranga 1000 kwa batch..inatosha kabisa. Maana kila in 4 weeks unategemea kurudi. Hii inafanya hata mzalishaji wa vifaranga ukue as the market grows.
Mayai... way forward ni mayai ya layers tu. Ambao production yao ni mpaka 90%. Kwenye kuku 100. Ni kuku 10 tu wanakuwa wamepumzika kwa siku. So gharama ya kulisha kuku 10 waliopumzika haikuumizi. Na hata ukiuza mayai kwa bei nafuu bado inalipa kwa vile utagaji ni mzuri.
Niko tayari ukiwa na swali