Faida na Hasara za DRC kujiunga EAC

Faida na Hasara za DRC kujiunga EAC

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
Wadau wapendao Utukufu kwa Mungu juu na AMAN dunian tuangalie mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yatakayotokana na nchi kubwa yenye migogoro ya muda mrefu na siasa ngumu zenye mkono wa kuibiana, na dhulma za walioko nje ya nchi muhanga, itakapopata washirika wa africa masharik wenye mlengo wa kufanya ukanda wa maziwa makuu sehem salama kuishi.

Binafsi naona ni pigo kwa Kigali na Kampala ambao ripot nyingi zinawatuhumu kudistabilise DRC kwa ajenda zao za siri. Pia nafikiria washirika wao katika hujuma dhidi ya DRC watareplace huu mkabo na nini!

DRC kuwa salama na kutawalika ni pigo kwa mataifa kadhaa hasa wanufaika wa maliasili zake.

Je, rwanda, beloved son wa washington atastawi vip bila mali za DRC? Au ndo mwanzo wa mwisho wao! Au wameshashiba!
 
Hiyo EAC naona imekuwa vurugu tu siku hizi, wananchi wake wanazidi kuwa masikini huku wakiendelea kuongeza nchi wanachama, sijui hao wengine ndio wanajiunga ili tuwe masikini kwa pamoja hata sielewi.
 
Kwani Kujiunga EAC ndio kusema Mwana wa Marekani afrima Mtu Mrefu ndio ataenguliwa?
 
Hiyo EAC naona imekuwa vurugu tu siku hizi, wananchi wake wanazidi kuwa masikini huku wakiendelea kuongeza nchi wanachama, sijui hao wengine ndio wanajiunga ili tuwe masikini kwa pamoja hata sielewi.
EAC kwa faida za wanasiasa tu.
 
Tunajiunga EAC ili tukiingiza/kusafirisha bidhaa ndani/nje ya jumuiya tupate unafuu wa gharama nasio vinginevyo
 
Tunajiunga EAC ili tukiingiza/kusafirisha bidhaa ndani/nje ya jumuiya tupate unafuu wa gharama nasio vinginevyo
Kwahiyo hatutashiriki kuhakikisha aman iko kwa kila mwanajumuiya? Mtafanyaje mikakat ya biashara kama hakuna utulivu! Naamin drc haitakuwa tena tembo anayeliwa bila kuchinjwa kwa kukatwa nyama kulingana na mlo!
 
Kama wamekubaliana kudhibiti migogoro ya kisiasa na kiusalama katika nchi washirika, bas drc kujiunga eac kutakuwa na maana kubwa kwao. EAC ni lazima wawe na nguvu ya kumlinda member anapokuwa kwenye migogoro
 
Kwahiyo hatutashiriki kuhakikisha aman iko kwa kila mwanajumuiya? Mtafanyaje mikakat ya biashara kama hakuna utulivu! Naamin drc haitakuwa tena tembo anayeliwa bila kuchinjwa kwa kukatwa nyama kulingana na mlo!
Kwan african union haipo au Aman sio kipaumbele chake?

Aman n jukumu la mwanachama nasio jumuiya.

Sie batu ba Kongo tunasema shukuru tanzanie kwa kutusaidia kuwa EAC sasa tutaanza lipia kidogo kutoa mizigo yetu kwa bandari ya daresalam hata zile gold zetu tukitaka peleka Europe au Asia Sasa hatutalipia mabesa mengi tena
 
Kwahiyo hatutashiriki kuhakikisha aman iko kwa kila mwanajumuiya? Mtafanyaje mikakat ya biashara kama hakuna utulivu! Naamin drc haitakuwa tena tembo anayeliwa bila kuchinjwa kwa kukatwa nyama kulingana na mlo!
Sudan kusin walipojiunga vita vao vimeisha?
 
Ngoja tuone. Muda utatuambia ila njaa kwa Rwanda, shida kwa Uganda ni mambo yanayoweza kutokea
 
Back
Top Bottom