dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,423
- 1,987
Hapo hapo na Dr. Kivugo ndio ticha wao. Ye ana Harrier hajaweka gesi.
Awali ya yoyote, hakuna sheria, katazo wala muongozo kwamba ukiwa unatengeneza kitu shurti ukitumie,
hiyo ni mosi. Pili, unadhani kumjua au kumtaja huyo Prof. ndio kukubalika kwa hoja yako isiyokuwa ya ukweli?
Nadiriki kusema kuwa huna taarifa sahihi na kama huyu uliyemtaja yupo pale unadhani anajua ya pale pengine kwa faida yako ungemdodosa ili uwe na uhakika kuliko kupotosha.
Kwanza Jua tu, sikukuuliza kwa bahati mbaya iwapo unajua wamejifunzia wapi hao uliowaita 'Vijana wa DIT'.
Ukakurupuka tu na kusema 'hapahapa Dar'. SIO KWELI.
Ukweli ni huu;
Ilisafirishwa na-serikali, timu ya watu ambao tayari walikuwa ni Mafundi kutoka DIT KWENDA KUJIFUNZA SWALA HILO TU HUKOOO JAPAN.
Hawa watu wakasoma, wakamaliza mwishowe wakafanya mitihani.
Haikuishia hapo, ni kwa wale waliofaulu vizuri tu ndio waliodhinishwa kuwa watafanya hiyo kazi na hayo ni maoni kutoka Japan (Kwa wenye Mfumo wao)
Nikushike Sikio kidogo, wapo kati yao walionda huko Japan wakasoma na bado hawakufanikiwa kuidhinishwa kama MAFUNDI. Hii sijui kwako itakupa picha gani lakini kwa mwenye kujielewa ni kuwa hii sio ishu ya kipuuzi.
ANGALIZO:
Mimi si msemaji wala sipo ndani huko lakini angalu najua hilo na sizushi.
Hivyo ukitaka chukua usipotaka acha.
Kingine;
Kuna vitu vinafundishwa pale DIT na baadhi ya sehemu nyingine za mafunzo ya Ufundi stadi.
Kimuonekano kwa asiejua Dunia ilipo na inapokwenda ataona kama havina mpango.
Lakini sasa, thamani yake 'Huko Duniani' kwa anaejua tukilinganisha mapato yake baadae ama huko 'mbelembele' kibongobongo,Hata mtu mwenye Msc. anaefanya Kazi hapa Bongo ni kama anapoteza muda.
Nimechomekea kidogo tu hapo lakini uwanda wa Somo hili ni mpana mno.
Kuna siku nikipata muda nitafungukakadiri ya ninavyojua.
Nawasilisha.