Faida na hasara za kutumia mafundi maiko kwenye ujenzi

Ilikuwa Bahati mbaya Fundi Maiko walikosea!
Walizingua nilimleta injinia mmoja akapima ule mwiniko wa paa ulikua mkubwa na usio na uwiano mzuri kwa sasababu bila kufunga gata maji ya paa yalikua yanamwagika ukutani kabisa πŸ€”
 
Walizingua nilimleta injinia mmoja akapima ule mwiniko wa paa ulikua mkubwa na usio na uwiano mzuri kwa sasababu bila kufunga gata maji ya paa yalikua yanamwagika ukutani kabisa πŸ€”
Pole sana mkuu!
 
Ma Engineer mimi siwezi fanya nao kao kwanza wao wanajionaga ndo wajumvi wa kila kitu. injinia hata ukimleta akutengenezee zizi tu basi atakuomba uwe na tape nk
Ni kweli wana ujuzi, sio kwamba wanajifanya. By the way Engineer anasimamia kazi (quality na quantity), anayofanya fundi, wakati fundi maiko anajisimamia kienyeji
 
Ni kweli wana ujuzi, sio kwamba wanajifanya. By the way Engineer anasimamia kazi (quality na quantity), anayofanya fundi, wakati fundi maiko anajisimamia kienyeji
Kabisa mkuu lkn Kuna mafundi maiko ni zaidi ya engineer ni vile hawana mavyeti tu. Kuna watu wanakipaji(kipawa) yaani akikuambia kitu ni mle mle hata umletee injinia wawapi atapita mle mle. Kuna mjomba wangu Huwa anatembea na engineer Kila sehemu kumpa nondo na huyo injinia kashakuwa na jina kubwa lkn kiuhalisia anapitia Kwa anko.
 
Hasara yao ni kwenye kukupiga,mahali pa bati 150 atakwambia bati 200,hizo hamsini zitakazozidi za kwake,labda kama utaamua kuacha shughuli zako ushinde naye site mpaka amalize......
kwenye kupiga ni hulka ya mtu alivyo. yoyote tu anaweza kukupiga tena huyo mvaa reflekta na gambuti ndo atakupiga pakubwa zaidi maana ni kama unalipia gharama za izo reflekta na gambuti alizovaa yeye🀣

tabia zingine ni za mtu mweusi tu alivyo bila kujali ana shule au la. weusi tunajuana.

kuna mmoja tulimuita hom kazi ya kawaida tu eti anadai eti leba tu ni milioni 3 tukachokaπŸ˜“ tukamuacha achape lapa
 
Design hio na Nyumb yenyew ni hii.
Mpak hapo tulipofikia nilitumia engineer watatu na mafundi maiko hata kumi nazan.
Nilifanikiw sabb engineer nilisoma nae so namuwez San Yan kwny kumlipa haijaniumiz San Ila kuna baadhi ya vitu nilikuw navipinga San sbb Mie mwenyew Nina uzoefu kidog. Shimo la foundation 150m adi tulivurugan San site Mim 150 nikakataa sabb ni Gorofa moja Tu shimo lote la nn. Na vyengn Kam mfano kwny ratio pia resho zake Kali kiseng hat majengo ya serikal hawawek izo pia nilipinga San Tu ye anatoa maelekez kw mafund na mim pia nawap maelekez. Kam sio ivyo ningeumia San.
Mafund maiko Nd natimua san hat sikumbelezi kuna fundi Mbao mmoj aliniibia Mbao 3 nikajua nikamtimua na uzuri. Mie sijauza kaz kw MTU mmoja Yani natoa kw penye fundi Chuma naelewan nae kwny fundi Mbao naelewan nae kwny fundi tofali naelewan nae. Fundi umeme naelewan nae unakuta site heshima na adabu hakun WA kumvimbia mwnzie na ukiwa nyum ya muda nakuchimbia mkwara vzr. View attachment 3165274View attachment 3165275
 
kongole sana mkulu🀝🀝

hilo shimo la foundation la mita 150 ndo standard iyo auπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜€??
 
kongole sana mkulu[emoji1666][emoji1666]

hilo shimo la foundation la mita 150 ndo standard iyo au[emoji2297][emoji2297][emoji56][emoji56][emoji36]??
Sio standard 75 Tu ilitosha mpk 100 sabb nyumb ni ya gorofa moja Tu. Maybe gorof 5 au 4 Nd 150 Sawa. Shimo moja walichimb 150 adi walikutan na jiwe aloo niligoma nikasem hapan ebu musichime ten Kam Ivo maan shimo lilikuw lefu balaa na haikuw na ulazim huo
 
Mita 150 kwenda chini, serious?.
 
kongole sana mkulu🀝🀝

hilo shimo la foundation la mita 150 ndo standard iyo auπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ˜‡πŸ˜‡πŸ˜€??
Mita 150 kwenda chini?? Hii balaa sasa. Au mnamanisha cm?
 
150cm ni standard kabisa hata kama ni nyumba ya ghorofa moja, hiyo ni sawa na futi 5 tu, inaonekana ni kubwa kwa sababu ipo katika sentimita

Katika hiyo 150cm, kuna nchi 2 ya blinding, 30cm ya kitako (base), ambapo mpaka hapo inakuwa imebaki kama futi 4 kutokea juu ya kitako cha nguzo

Tunachimba chini zaidi kwa sababu soil bearing capacity huongezeka kadri unavyozidi kwenda chini kwa hivyo inatafutwa soil strata ambayo atleast itakuwa na bearing capacity ya kuweza kuhimili uzito wa jengo bila kuleta shida
 
Fundi wazuri ni wale wamefanya kazi kwenye kambi za jeshi wale wanazingatia kila Detail maana kule akijaribu kazi matilio ya kurudia kazi ni juu yake . Kuna mmoja namjua na ameshapewa miradi mikubwa kuisimamia hasa tiles na ujenzi wa jengo ,plasta na zege
 
Kiongozi, au umesahau? Shimo la urefu wa mita 150??? Zaidi ya kiwanja cha mpira????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…