Nitachangia kidogo na wenzangu wataongezea.
Magadi yale ya kienyeji (Huko kilimanjaro huyaita mbala/ikati) ni mojawapo ya chumvi-chumvi asili na yana mchanganyiko wa Sodium bicarbonate,magnesium hydrophoshate na madini/vitu vingine. Yanapoyeyuka kwenye maji, maji hayo yanakuwa ni alkaline. Ndo maana watu huyatumia kutibu kwa haraka sana tatizo la kiungulia (heartburn) kwani hu-neutralize acid (tindikali) tumboni.(ref.maharage yaliyopikwa kwa kutumia magadi hayaleti kiungulia).
Yakitumika vizuri (Kwa kuzingatia maelekezo ya wazoefu) hayana hasara ktk. mwili wa binadamu ila faida yake ni husaidia sana kuimarisha mifupa na ndo maana mtu aliyevunjika akitumia vyakula vyenye magadi hupona mapema i.e.mfupa /mifupa huunga mapema zaidi. Mifugo hulamba na afya yao huimarika.
Kinachofanya meno yawe ya kahawia ni kule kuwepo kwa kiasi kilichozidi kiwango cha madini yaitwayo Fluorine/Fluoride. Lakini meno hayo (kwa utani wanayaita meno ya mbao) ni imara zaidi i.e. ni magumu zaidi kuliko yale meno meupe.
Hicho ndicho ninachafahamu.