Faida ya unallocated shares (nadhani terminology inayotumika ni unalloted shares) ni kwamba inakupunguzia paper work na gharama zingine unapotaka kuongeza mtaji wa kampuni yako. Maana yake ni kwamba unakuwa na mtaji ulioidhinishwa (Authorised Share Capital) lakini wenye hisa wanatanguliza sehemu tu ya huo mtaji (Issued Share Capital) kulingana na mahitaji ya wakati huo. Ile sehemu uliyobaki ndiyo Unalloted Share Capital. Siku utakapohitajika kampuni itaupata kwa haraka kutoka kwa wanahisa waliopo au kutoka kwa wanahisa wapya. Vinginevyo kampuni ingebidi kubadilisha katiba yake (i.e. Memorandum and Articles of Association) ili kuongeza kiasi cha mtaji ulioidhinishwa. Mchakato huu unachukua muda mrefu pamoja na gharama.