Wana Jukwaa Hongereni kwa Kazi.
Ningependa kujua unapoanzisha kampuni ni wakati gani unahitaji kuacha unallocated shares. Faida yake nini na hasara zake ni zipi.Kazi njema
watu wapo Kwenye siasa na mapenzi.
hizo Ndio habari zinazopendwa zaidi Jf na Tanzania kwa ujumla. ccm wameharibu kabisa hii nchi, wameliangamiza taifa.
Faida ya unallocated shares (nadhani terminology inayotumika ni unalloted shares) ni kwamba inakupunguzia paper work na gharama zingine unapotaka kuongeza mtaji wa kampuni yako. Maana yake ni kwamba unakuwa na mtaji ulioidhinishwa (Authorised Share Capital) lakini wenye hisa wanatanguliza sehemu tu ya huo mtaji (Issued Share Capital) kulingana na mahitaji ya wakati huo. Ile sehemu uliyobaki ndiyo Unalloted Share Capital. Siku utakapohitajika kampuni itaupata kwa haraka kutoka kwa wanahisa waliopo au kutoka kwa wanahisa wapya. Vinginevyo kampuni ingebidi kubadilisha katiba yake (i.e. Memorandum and Articles of Association) ili kuongeza kiasi cha mtaji ulioidhinishwa. Mchakato huu unachukua muda mrefu pamoja na gharama.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.