Mkuu
charminglady, nadhani ningesema kwanza maji yanaweza kuwa ya moto(joto kali), vuguvugu(joto la wastani), no baridi( joto dogo)..na ninadhani katika thread/kwa ujumla watu husema maji ya "uvugu vugu" wakimaanisha maji ya "moto", kitu ambacho si sahihi sana.Uchaguzi wa kuoga kwa maji ya baridi au yenye joto kiasi hutegemeana na "utashi" lakini pia hutegemea;
Umri: Wazee na watoto wadogo maji ya uvuguvugu ni mazuri zaidi, na baridi kwa vijana.
Magonjwa: Baadhi kama Ini, wenye matatizo ya burning sensation maji ya baridi hufaa na wale wenye mafua, allergy, maumivu ya vifundo, kikohozi kwao ya uvuguvugu ni bora zaidi.
Msimu: Wakati wa baridi ni vizuri kutumia maji ya uvuguvugu, na wakati wa joto kutumia maji yenye ubaridi.
Tabia: Yaani wale wanaofanya mazoezi na wasiofanya mazoezi.
Lakini hata hivyo, kiafya hakuna madhara kwa watumiaji wa maji ya uvuguvugu...hata hivyo kwa maji ya MOTO unaweza kupata madhara kadhaa.
1. Kuharibika kwa ngozi: Mwili huweza kuhimili joto na kwa wenyewe(mwili) kujitbadilisha ili kujihifadhi(regulate) katika mazingira tofauti, hata hivyo joto likizidi na mwili ukashindwa kustahimili, ngozi huharibika mf. kuungua, kubabuka n.k
2. Magonjwa: Katika ngozi, vinyweleo husaidia sana katika "kubadilisha" joto kulingana na mazingira(regulate), na hivyo basi endapo maji ya moto(si vuguvugu) yataendelea kutumika mara kwa mara huweka kuharibu sehemu ya vinyweleo na ngozi kuonekana ipo nyekundu, muwasho,na huweza kupasuka( Hot tub/bath Folliculitis)...hii ni kutokana na joto kali(Heat rash)..mf. mzuri ni watu watokapo sehemu ya baridi wakijaribu kuishi sehemu ya joto..au hata sehemu zenye joto mf. Dar na joto likaongezeka watu hapata "Heat rash" pia...Tatizo hili huisha lenyewe ndani ya siku saba hadi kumi hivi.
3. Madhara kwa mtoto: Kwa wakina mama wajawazito, kutumia maji ya MOTO si vyema sana, kwani wakati wa ujauzito msukumo wa damu wa mama, huweza kubadilika kwa urahisi sana na kwa kutumia maji ya moto husababisha jotomwili kupanda,(overheated), huleta mapigo ya moyo kwenda kasi, kufanya msukumo wa damu kuwa mdogo na damu kidogo kutolewa hivyo kuhatarisha maisha ya mtoto aliye tumboni.(mtoto ana kuwa in a stressful condition.)
Hivyo basi, kwa kutegemeana na sababu nilizokwisha sema hapo juu, uamuzi unaweza kufanya kwa kutumia maji ya ubaridi au uvuguvugu..na si maji ya MOTO.