Uchaguzi 2020 Faida tutakazopata Watanzania NCCR Mageuzi atakapokuwa chama kikuu cha upinzani baada ya Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Faida tutakazopata Watanzania NCCR Mageuzi atakapokuwa chama kikuu cha upinzani baada ya Oktoba 2020

Huyu mtoa post nae vipi? Naona umeibuka kama jua la leo la alasiri ambalo hata hatuelewi ni ishara gani.

Na yule anaesema tufanye maombi anasahau kwamba kuna mambo muhimu ya kuchukulia serious
 
Tunajua NCCR Mageuzi Ndio chama ambacho upepo unakivumia vizuri baada ya kupita kwenye mawimbi mengi kwa miaka kumi mfululizo!

Kuna kila dalili hawa jamaa ndio wataunda kambi ya Upinzani wakishirikiana na Cuf au ACT Wazalendo

Faida ya NCCR Mageuzi kuwa Chama kikuu cha upinzani

1. Itaharakisha maendeleo kwani hawa watu wanasiasa za kistaarabu na hawana matusi tofauti na upinzani uliopo

2.Hawana historia ya kutumiwa na Mabeberu kuisaliti Nchi tofauti na chama Kilichopo ambacho kimekuwa kikiwatetea Mabeberu badala ya kuwapigania Watanzania

3.kina idadi kubwa ya wasomi refer Masumbuko Lamwai anatajwa kuwa mwanasheria bora kuwahi kutokea kwa Siasa za Upinzani, hivyo watashirikiana na serkali katika kuijenga Nchi

4 Vurugu na lugha mbaya zitaisha bungeni, tutakumbuka kuwa NCCR mageuzi Ndio chama chenye rekodi ya kuwa na wabunge Wengi bungeni kwa wakati moja Lakini hawakuwahi kufanya vurugu bungeni kama Wapinzani waliopo wanaofanya

5.NCCR Mageuzi ina makao makuu bora kabisa hawa waliopo Chama kimepanga kwenye nyumba ya mtu tena ndogo

6.Hakikuwahi kuwadhihaki makaada wake alipoondoka Mrema, Marando hawakumtukana Walisema ni siasa ila wasasa mwanachama akiwakimbia anatukanwa kila aina ya Matusi

7. NCCR Mageuzi kilikuwa chama cha kitaifa Watanzania wote walikiheshimu


Karibuni NCCR Mageuzi Katika ujenzi wa Taifa letu la Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa hawamo kwenye list ya korona?

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Baada ya zoezi la kununua wapinzani sasa mmeanza kununua vyama.
Hizo hela mgewekeza kukabiliana na corona kuliko kununua wapinzani na vyama vyao.
Sasa ngoja corona iwatafune,na kuwafata huko mafichoni mliko.
 
Huo ni wivu kwa Nccr mageuzi Baada ya Chadema kufubaa kisiasa
Baada ya zoezi la kununua wapinzani sasa mmeanza kununua vyama.
Hizo hela mgewekeza kukabiliana na corona kuliko kununua wapinzani na vyama vyao.
Sasa ngoja corona iwatafune,na kuwafata huko mafichoni mliko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom