Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Dunia nzima, hakuna nchi inayomiliki makundi ya wapiganaji ndani ya nchi nyingine, isipokuwa nchi ya Iran pekee. Makundi ya wapiganaji yanayomilikiwa na Iran ni pamoja na Hezbolah, Hamas na Houthi. Makundi haya yamepandikizwa kwenye nchi za kiarabu zenye serikali zinazoongozwa na wasunni, huku kukwepo Washia.
Iran ndiyo nchi pekee iliyowahi kutangaza hadharani mara kadhaa kuwa Wayahudi hawastahili kuwepo Duniani, wanastahili kuangamizwa, wapotee kabisa.
Kutokana na sera za ajabu za Iran, nchi karibia zote za Mashariki ya kati ama zina uhasama au zina uhusiano wenye mashaka na Iran.
Makundi ya wapiganaji ya Iran, yameifanya Mashariki ya Kati, wakati wote kuwa katika vita. Na kwa baadhi ya mataifa, makundi haya yamezifanya Serikali za nchi hizo kuwa dhaifu na kutoweza kufanya chochote dhidi ya makundi hayo kutokana na ukweli kuwa Iran inayatumia makundi haya kuzidhoifisha serikali za mataifa hayo.
HAMAS, kwa msaada wa Iran, waliamua kuupiga utawala halali wa mamlaka ya Palestine, na kuchukua maeneo ya Gaza na kuyaweka chini ya mamlaka yake. Na kisha kuanzisha mapambano dhidi ya Israel, wakidai kuwa wayahudi (wazayuni) wanatakiwa kuangamizwa.
HEZBOLAH huko Lebanon wameifanya Serikali ya Lebanon kuwa dhaifu. Na Hezbolah imekuwa serikali ndani ya Serikali.
"Hezbollah has been described as a "state within a state", and has grown into an organization with seats in the Lebanese government, a radio and a satellite TV station, have military deployment of fighters beyond Lebanon's borders"
Hezbolah wanashikilia falsafa ya Iran, kuwa wayahudi hawastahili kuwepo Duniani.
HOUTHI, kwa msaada wa Iran, mwaka 2017, walimwua Rais wa Yemen Ali Salehe kwa madai kuwa ni msaliti. Mpaka sasa wameyawafanya maeneo mengi ya Yemen kuwa chini yao, huku serikali ikiwa haina uwezo wa kuwafanya lolote.
Makundi haya, yana ofisi zao, maghala ya silaha, na maficho yao yamewekwa katikati ya makazi ya watu au kwenye majengo ya taasisi za kiraia kama shule na hospitali. Hivyo wanashambulia kutokea katikati ya makazi ya watu. Na wanayepambana nao, akiyajibu mashambulio yao, lazima maafa ya raia yatokee. Na wakiweka miundombinu yao chini ya nyumba yako au karibu na makazi yao, ukitaka kuhama, wanakuua kwa madai kuwa wewe ni msaliti.
Swali kuu, hivi haya makundi ya kigaidi ya Iran kwenye mataifa ya kiarabu, yana faida gani kwa wananchi? Kwa vile makundi haya, yanasababisha maafa makubwa kwa raia, kuna yeyote anayeweza kuyafuta? Kwa vile nchi ya Iran, nchi yenye akiba kubwa ya mafuta, lakini hakuna mwananchi au kampuni inayoruhusiwa kuwa na kisima cha mafuta, isipokuwa Serikali pekee yake;
Imeamua kuyafadhili makundi haya ya kigaidi wakati wote, haya mataifa maskini ya kiarabu yaliyopandikiziwa makundi ya kigaidi, yana dalili yoyote ya kuuona mwanga wa amani? Je, mataifa tajiri ya kiarabu, yanaweza kuyasaidia mataifa ya kiarabu maskini ili yaondokane na haya makundi ya kigaidi ya Iran? Kama Iran itaendelea na sera zake za mauaji kwa kutumia makundi ya kigaidi, na ikaendelea kuyapanua au kuongeza makundi haya ya kigaidi, nini hatma ya usalama na amani ya mataifa ya Mashariki ya kati?
Inaelezwa kuwa mataifa mengi ya kiarabu na waarabu wengi hufurahia Israel inapoyaangamiza makundi haya kwa sababu ndiyo nchi pekee hapo Mashariki ya kati yenye uwezowa kupambana na makundi haya, na hata Iran.
Ndiyo maana mataifa haya pamoja na baadhi ya Serikali zilizodhooifishwa, kwa siri, zinatoa taarifa za kiintelijensia kwa Israel ili ifanikishe maujai dhidi ya haya makundi ya kigaidi. Je, Israel itafanikiwa dhidi ya uharamia huu wa Iran?