Faida ya kilimo cha miti

Faida ya kilimo cha miti

Kigorohe

Senior Member
Joined
May 21, 2019
Posts
160
Reaction score
255
Habari zenu wana JF! Namshukuru Mungu kwa kunipa nasafasi hii ya kuongezeana maarifa na ujuzi ya kulijenga taifa letu.
Bila kupoteza muda naomba niende kwenye mada.

Mimi ni mwanafunzi lakini pia huwa najishugulisha na maswala ya kilimo. Nimelima takribani misimu mitatu bila ya kupata mazao ya uhakika.

Hii huenda inasabishwa na kutokuwa na nguvu za kutosha katika kuhudumia mazao pindi yapo shambani.

Lakini kulingana na mavuno hafifu ktk misimu yote hiyo, nimeamua kubadili mawazo ya kuhamia katika kilimo cha miti aina ya mikaratusi.

Maana hii nahisi hainahitaji huduma kubwa sana ukilinganisha na mazao kama mahindi, karanga au viazi.

Jamani unajua humu kuna wataalam wa kilimo nipeni ushauri wa ziada.
 
Mikaratus inanyonya maji sana, na inaenda mdog mdog sana....nenda iringa kapande miti huko, sehemu zingine miyeyusho miti inadumaa sana
 
Eneo unalo ila hujasema upo wapi, kama ni nyanda za juu kusini, Mbeya Tukuyu, Njombe, Pwani, Kagera, Kigoma Kibondo, Panda tu usiogope ila zingatia mbegu bora.İpo mbegu ya miaka saba tu unavuna waone wakala wa misitu.

Kama ni maeneo hayo nakushauri upande na parachichi huzaa miaka 3-4 hutasubiri sana.
 
Mi nipo Mara wilaya ya Tarime. Asante sana kwa ushauri wako ila nkuulize kitu, kwani nikinunua hii miche wanayouza gardeners ni vibaya?
 
Sio vibaya ila huna uhakika kama ni mbegu nzuri za kukomaa haraka, ni vizuri ukajiandalia mbegu za uhakika, kumbuk muda ni mali kuna mikaratisi inakaa miaka mingi sana mpaka kukomaa.
 
Mikaratus inanyonya maji sana, na inaenda mdog mdog sana....nenda iringa kapande miti huko, sehemu zingine miyeyusho miti inadumaa sana
kuna aina 700 za mikaratusi. Aina nyingi zilizopo Tanzania siyo zinzonyonya maji. Lakini pia Kilimo cha miti ya mikaratusi ndo kilimo rahisi kuliko aina yeyote ile ya miti. Wewe kazi yako ni kupanda tu na kuiacha huko huko. baada ya miaka mitano uoto wote chini yake umekufa. Mikaratusi inakua katika mazingira yote magumu. Cha msingi uchague ardhi yenye rutuba kiasi na kina kirefu cha udongo, ndani ya miaka 15 hadi 18 unakuwa na miti yenye kutoa hadi mbao kati ya 60 na 80 kwa kila mti kwa mbao za 2"x4" kwa urefu wa kuanzia futi 12.
 
Back
Top Bottom