Faida ya mauzo ya luku kwa mawakala kutoka 2.5 hadi 0.5

Issuna

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,203
Reaction score
7,628
Katika hili ki ukweli sioni hata faida ya Haya ma mashine ya SELCOM na MAXMALIPO maana mawakala wote hapa walikua wanategemea kwa 80% faida ya kamisheni kutoka kwenye Mauzo ya luku.

Leo hii unaniambia eti kwenye 100,000 ya mauzo ya luku Faida nitayopata ni 1000 Khaaaaaaaaaaaaa..hadi kinyaaa Laki moja yangu nikiuza karanga si napata mara 4 na zaidi ya hiyo Faida?? πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

Yani serikali ilianza kama utani ikafuta FAINI ZA TRAFFIC kwa mawakala saivi ukipigwa faini lazima uende bank au ulipie mwenyewe kwenye simu ila sio kwa SELCOM wala MAXMALIPO,watu wametulia tu saivi tena wamehamia kwenye LUKU aseeee kwa mwendo Huuuu haya Ma mashine ni UOZO.😑😑😑😑😑

Yani faida ya LUKU ni sawa na Ku recharge mwendokasi?? sasa serikali kama hamtaki WATU WAHUDUMIWE fanyeni bhasi huduma zote wenyewe.😎😎😎😎

Kama tangazo lae wanavyodai kuanzia Tarehe 02 kamisheni ya LUKU itakua 0.5 na Mawakala tunaseMA kUANZIA Tarehe 02 umeme watu wakanunue TANESCO...shEnziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiπŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰
 
Mmmhh. Kumbe ?? Haya tusubiri save the date
 
kwani before mlikuwa mnapata faida kias gani? kwenye umeme wa 100k .
 
kununua kwa tigo pesa hiyo bado ipo au nayo wamefuta?
Sijajua ila nadhani haijafutwa Ipo bado..SIJAJUA SASA ITAATHIRI VIPI UNUNUZI WA hUKO NAKO tUSZIDI KUTEGA SIKIO.
 
Dah...!! Ni kuhamia kwenye business nyingine tu
 
Tulioshtuka mapema kutoka chanzo makini MANGE KIMAMBI tuliziuza mashine na kuweka fedha mfukoni, kiukweli kilichofanyika si sawa kabisa mliobakiwa nazo amueni kugomea kuzitumia wakanunue TANESCO. Huwezi ambiwa faida itoke 2.5% hadi 0.5 ujinga huo. Bora ukachome mahindi au uweke matuta ya mchicha utaambulia.
 
Sijajua ila nadhani haijafutwa Ipo bado..SIJAJUA SASA ITAATHIRI VIPI UNUNUZI WA hUKO NAKO tUSZIDI KUTEGA SIKIO.

Sina uhakika sana na sio mtaalam ila nijuavyo, makampuni ya simu hayawezi kufanya muamala moja kwa moja na tanesco ili kupata umeme, wanapita kwa muwezeshaji kama selcom na wengine.

Kama tanesco wamefanya maboresho ya mifumo tao inaweza kuwezekana miamala ya moja kwa moja.
 
Nadhani shida yao ni kushika kila kitu wao (serikali) Sasa kama ndo dhumuni na lengo lao Waseme tu watu tujue kua kuna vitu vinafanywa na serikali tu Mbona itaeleweka,ila sio kuingiwa na Tamaaa za kipumbavu wanaona watu wanafanya kazi wao wanakuja wanaingia kati na kuharibu Mifumo.

Haya sasa ngojea watu mashine zikae pembeni tuanze kwenda kujipanga Mistari alafu tuone kama wataweza kutuhudumia watanzania wote maana shida yao ni kutuweka Foleni kama Mwendokasi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…