Uchaguzi 2020 Faida ya Prof. Kitila kwa Ubungo, Dar

Uchaguzi 2020 Faida ya Prof. Kitila kwa Ubungo, Dar

Juma Katolila

New Member
Joined
Jun 1, 2020
Posts
4
Reaction score
10
UJIO wa Profesa Kitila Mkumbo katika siasa za Dar es Salaam umeleta nguvu mpya na msisimko katika siasa za Mji Mkuu wa zamani wa Tanzania.

Kwa takribani miaka 15 sasa, Dar es Salaam ilikuwa na bahati mbaya ya kuwa na wabunge machachari wa upinzani na waliopoa kidogo; walau ndani ya Bunge kutoka jiji hilo.

Majina mashuhuri bungeni miongoni mwa wabunge wa Dar yalikuwa kama Halima Mdee, John Mnyika na Mwita Waitara wakati ule. Wabunge wa CCM kama vile Mussa Azzan, Zuberi Mtemvu, Mangungu wa Mbagala na wengine walikuwepo lakini si wabunge walioweza kuzungumza mambo yaliyobaki kwenye mijadala ya watu kwa muda mrefu.

Kitila amebadilisha hali hiyo. Katika mikutano yake ya hadhara na katika maisha yake ya kisiasa - kwa muda mrefu, mgombea huyu wa CCM Jimbo la Ubungo amejipambanua kama mmoja wa wajenga hoja mahiri.

Ingizo la Kitila linaweza kubadili kabisa namna wabunge wajao wa CCM watakavyokuwa. Pengine watu wa Dar es Salaam sasa watajua ni aina gani ya wanasiasa wanafaa kuwawakilisha bungeni.

Akina Halima walikuwa wazuri kwa harakati lakini kwa sababu chama chao hakikuwa madarakani, walikosa connection ya kutimiza majukumu yao vizuri.

Uwezo wa Kitila wa kujenga hoja utamfanya asikilizwe kila anaposimama lakini kwa sababu anatoka chama tawala cha CCM, kuna uwezekano mengi wa atakayosema yatafanyiwa kazi.

Akina Mnyika na Kubenea waliopewa nafasi ya kuwa wabunge walihama majimbo yao baada ya kipindi kimoja kwa sababu ingawa watu wanajua hali ilivyo, ni vigumu kwenda kuomba kura kwa watu unaojua huna cha maana ulichowafanyia zaidi tu ya kuzungumza bungeni.

Mji kama Dar es Salaam ni muhimu kuwa na walau mbunge mmoja mwenye hadhi ya kitaifa. Ndivyo ilivyo kwa miji yote mikubwa duniani.

Raila Odinga alikuwa Nairobi, akiongoza Jimbo la Lang'ata. Erias Lukwago kwa muda mrefu alikuwa Kampala. Rais wa sasa wa Senegal, Macky Sall, alijipatia umaarufu akiwa Meya wa Dakar.

Dar, kwa muda mrefu, ilikuwa inalilia kuwa na mbunge mmoja wa kitaifa ambaye akizungumza, unaweza kabisa kusema Wana Dar es Salaam wamezungumza.

Mbunge huyo sasa anaelekea kupatikana; Kitila Alexander Mkumbo PhD.
 
Profesa kitila Ni moja kati ya mazao ya upinzani, mtindo wa CCM mpya kununua wabunge na viongozi wa upinzani ndio matoeo ya kitila mkumbo.

Ni kweli kitila ni mjenga hoja mzuri sana lakini akiwa ndani ya CCM hawezi kuzungumza kitu wala kuwa na mchango wowote kwa jamii.

Nadhani alikuwa akiheshimika sana alipokuwa UDS kuliko hata huko wizarani aliko.

Boro angeenda kwa Mwigulu kuliko hapo Ubungo, Ubungo hatuwezi kuipa kura CCM.

JIWE OUT CCM OUT.
 
Kwangu ni uzi bora kbs siku ya leo kubwa naomba tuvumiliane iwe Hoja kwa Hoja kwangu Prof ilikuwa kheri kwake kuilinda heshima yke na Utu wake kwa kubaki Chuo Kikuu japo amenisaidia kujua kwamba Hawa ndugu zetu wanaharakati shida yao kubwa na wao ni kupata nafasi ya kula keki ya Taifa sio kutusemea au kutetea Raia wa kawaida sasa huyu ndio msomi Prof vp mie Mzaramo mmoja kutoka Yombo Lukinga.
 
Hapa Ubungo hatutaki wajinga wachumia tumbo , waliokotwa jalalani , Boniface Jacob niyeye

Mtoa mada Mkumbo kamchugue wewe na sio sisi.
Acha mihemko, ujinga wa professor upo wapi? Una elimu ganii kumshinda yeye?, Kuchumia tumbo unamaana ganii? Huyo unaye mhisi ni Bora kuliko mkumbo yeye haendi kuchumia tumbo? Au pesa atazigawa mtaani? Jenga hoja, kejeli matusi na dharau hazifai isipokua uwe juu ya huyo unaemsema au kuyathibitisha mabaya yake, hoja hushindanishwa kwa hoja mkuu.
 
Kitila mkumbo ni chaguo sahihi kwa ubungo na siasa za Sasa.
Katika wakati ccm imefanya maamuzi sahihi kwa mazingira sahihi ,ni kipindi hiki walipopitisha majina kama Kitila Mkumbo kwenda bungeni
 
..Boniface Jacob atawafaa zaidi wananchi wa ubungo.

..alifanya vizuri ktk nafasi ya udiwani na umeya.

..anazifahamu changamoto za jimbo la ubungo.

..akichaguliwa ataanza kuzishughulikia changamoto hizo mara moja.

..Kitila itabidi aanze kujifunza changamoto za ubungo kabla hajaanza kuzishughulikia.
 
Yuko wapi ndugu yako Ally Katolila? Alikua winga matata sana enzi za ufalme wa Pan Africa
 
Mimi Ni mpiga kura Jimbo la ubungo kata ya kimara kura yangu hapati huyu propesa kitila tena na hivi walivyokuwa wanatukatia katia maji huku kimara hivi karibuni ninahasira naye hiyo tarehe 28 namchinjia baharini
 
Huyu ni aina ya watu ambao jamii ya tanzania inahitaji kuwa nao ili kusonga mbele,ni hazina ya kidumu na zao bora la mfumo wa elimu wetu..
Binafsi nimepata kupita kwenye mikono yake,ni mwalimu mzuri.ni mshahuri mzuri lakini zaidi ni mchapakazi mzuri mwenyw fikra za kizalendo na kimaendeleo.in short ni tunu au tuseme ni dhahabu mchangani.

Wana ubungo wamepata mtu bora katika historia ya Jimbo hilo.

Plz UBUNGO MSIFANYE MAKOSA.KITILA NI MTU SAHIHI KUWAWAKILISHA
 
Boniface Jacob bado hatoshi kwenye uwakilishi,sababu yeye ndio alikua meya na diwani lakini miundo mbinu ya mitaa ilizidi kuharibika na kuwa mibovu kipindi chake.
Hakua kiunganishi kizuri Cha utendaji Kati ya halmashauri na serikali kuu,kwa kuweka harakati binafsi mbele kuliko maendeleo ya Jimbo na watu wake..
 
Hakuna.phd uchwara hiyo...wizara ya majj amefanya nini nzega hakuna maji kote huku ni balaa hata kijiji alikojenga nyumba yake Puge kwa kingagwala wala chembe chembe ya maji masafi hakuna...maji ya tope huko...
shida tupuuu amefanya nini...prof uchwara ..
Mastermind/strategist wa ccm 2020 mpya..…
 
Hakuna.phd uchwara hiyo...wizara ya majj amefanya nini nzega hakuna maji kote huku ni balaa hata kijiji alikojenga nyumba yake Puge kwa kingagwala wala chembe chembe ya maji masafi hakuna...maji ya tope huko...
shida tupuuu amefanya nini...prof uchwara ..
Mastermind/strategist wa ccm 2020 mpya..…
Wakati nyie mnatumia hizo personal attacking kufanya propaganda za siasa,wananchi wengi siku hizi ni waelewa na wanaona ukweli..wanataka facts, information na data kamili sio utopolo kama huo unaotuambia kuhusu Profesa Kitila...
 
Watanzania wa Sasa ni waelewa,wanatumia vyema akili zao,na wanajua vyema wanataka nini,kwa ajili ya maisha yao,ndugu zao na taifa lao..
Profesa Kitila Mkumbo anajulikana vyema ni mtu wa aina gani,wala usingepata tabu ya kuandika haya yote,kwamaana Wana ubungo watampitishia kwa nguvu moja.
 
Profesa kitila Ni moja kati ya mazao ya upinzani, mtindo wa CCM mpya kununua wabunge na viongozi wa upinzani ndio matoeo ya kitila mkumbo.

Ni kweli kitila ni mjenga hoja mzuri sana lakini akiwa ndani ya CCM hawezi kuzungumza kitu wala kuwa na mchango wowote kwa jamii.

Nadhani alikuwa akiheshimika sana alipokuwa UDS kuliko hata huko wizarani aliko.

Boro angeenda kwa Mwigulu kuliko hapo Ubungo, Ubungo hatuwezi kuipa kura CCM.

JIWE OUT CCM OUT.
Kwa MANTIKI hii unahitaji sana darasa la siasa za maendeleo,unahitaji darasa kufungua hizo fikra zako zilizolala baada ya kumezeshwa rubish tupu
 
Back
Top Bottom