Juma Katolila
New Member
- Jun 1, 2020
- 4
- 10
UJIO wa Profesa Kitila Mkumbo katika siasa za Dar es Salaam umeleta nguvu mpya na msisimko katika siasa za Mji Mkuu wa zamani wa Tanzania.
Kwa takribani miaka 15 sasa, Dar es Salaam ilikuwa na bahati mbaya ya kuwa na wabunge machachari wa upinzani na waliopoa kidogo; walau ndani ya Bunge kutoka jiji hilo.
Majina mashuhuri bungeni miongoni mwa wabunge wa Dar yalikuwa kama Halima Mdee, John Mnyika na Mwita Waitara wakati ule. Wabunge wa CCM kama vile Mussa Azzan, Zuberi Mtemvu, Mangungu wa Mbagala na wengine walikuwepo lakini si wabunge walioweza kuzungumza mambo yaliyobaki kwenye mijadala ya watu kwa muda mrefu.
Kitila amebadilisha hali hiyo. Katika mikutano yake ya hadhara na katika maisha yake ya kisiasa - kwa muda mrefu, mgombea huyu wa CCM Jimbo la Ubungo amejipambanua kama mmoja wa wajenga hoja mahiri.
Ingizo la Kitila linaweza kubadili kabisa namna wabunge wajao wa CCM watakavyokuwa. Pengine watu wa Dar es Salaam sasa watajua ni aina gani ya wanasiasa wanafaa kuwawakilisha bungeni.
Akina Halima walikuwa wazuri kwa harakati lakini kwa sababu chama chao hakikuwa madarakani, walikosa connection ya kutimiza majukumu yao vizuri.
Uwezo wa Kitila wa kujenga hoja utamfanya asikilizwe kila anaposimama lakini kwa sababu anatoka chama tawala cha CCM, kuna uwezekano mengi wa atakayosema yatafanyiwa kazi.
Akina Mnyika na Kubenea waliopewa nafasi ya kuwa wabunge walihama majimbo yao baada ya kipindi kimoja kwa sababu ingawa watu wanajua hali ilivyo, ni vigumu kwenda kuomba kura kwa watu unaojua huna cha maana ulichowafanyia zaidi tu ya kuzungumza bungeni.
Mji kama Dar es Salaam ni muhimu kuwa na walau mbunge mmoja mwenye hadhi ya kitaifa. Ndivyo ilivyo kwa miji yote mikubwa duniani.
Raila Odinga alikuwa Nairobi, akiongoza Jimbo la Lang'ata. Erias Lukwago kwa muda mrefu alikuwa Kampala. Rais wa sasa wa Senegal, Macky Sall, alijipatia umaarufu akiwa Meya wa Dakar.
Dar, kwa muda mrefu, ilikuwa inalilia kuwa na mbunge mmoja wa kitaifa ambaye akizungumza, unaweza kabisa kusema Wana Dar es Salaam wamezungumza.
Mbunge huyo sasa anaelekea kupatikana; Kitila Alexander Mkumbo PhD.