Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mara nyingi timu inaposhinda nyumbani, ikienda ugenini hujipanga kutafuta sare ya aina yoyote na kwa maana hiyo, hucheza zaidi mchezo wa kujihami na si kutafuta magoli.
Hali hii huzigharimu timu nyingi kwani hupelekea kushambuliwa huku yenyewe hushambulia kwa kukabiliana zaidi badala ya kufanya mashambulizi ya kupanga.
Kinachotokea ni mara nyingi timu inayoshambulia muda wote kufanikiwa katika kuanza kufunga na hatimaye kuibuka na ushindi huku timu inayocheza mchezo wa kujihami kuanza kushambulia mara nyingine ikiwa wameshachelewa huku kisaikokjia wakiwa tayari wameshaathirika na hivyo inakuwa rahisi kupoteza mchezo wa marudiano.
Hivyo, kwasababu Yanga haijapata ushindi nyumbani, hawawezi kwenda kucheza mchezo wa kujihami na badala yake watacheza kutafuta magoli kama ambayo Al Hilal nao watacheza ili washinde.
Kwa msingi huo, mechi ya marudiano itakuwa ni ya ushindani na si mchezo wa upande mmoja kama ambavyo ingekuwa iwapo Yanga angeshinda nyumbani na hii ndio faida ya Yanga kutoa sare na wapinzani wao.
Kwasababu Al Hilal inafungika, Yanga wakirekebisha makosa yao madogo madogo huku wakicheza kutafuta ushindi na wanaweza kuandika historia mpya katika hii mchezo.
Naomba niishie hapa tusubiri siku husika iwadie.