Kimwakaleli
JF-Expert Member
- Apr 16, 2018
- 15,331
- 22,307
Kukulia Vijijini kuna Faida zake Nyingi sana.
Nilianza shule mjini Arusha Kaloleni shule ya msingi kwa Sasa hivi nasikia ni shule ya sekondari.Nilisoma pale hadi Darasa la Tatu(3),Nikiwa na Wazazi wangu,.
Mwezi wa Sita tulienda likizo Mbeya kwa Babu na Bibi, tukiwa huko Babu yangu alinitaka nibaki huko kwa nguvu zote,maana hakuwa na mjukuu yoyote,maana wenzake aliona kama wanamtambia kwa kuwa na wajukuu zao hasa nyakati za jioni kwenye mabalaza Yao na pia kwenye uchungaji wa mifugo nk .
Wazee wakamkubalia shingo upande,ingawa hata Mimi sikupenda kukaa huko! Nilichojifunza huko Kwa Sasa ni Faida kwangu pia na kizazi changu na wengine pia.
Nilimaliza huko kijijini shule nikaendelea mjini na shule na vyuo na kupata kazi mjini.
Maisha ya kijijini yalinifunza mambo mengi,naanza na haya:
1.Uvumilivu,shule zilikuwa mbali na nyumbani,wakati mwingine unashinda na Njaa kwa kwenda kula Mchana,kuhofia kuchelewa masomo ya Mchana.pia kutokuwa na hela ya kujikimu haikuwa shida,kwa maana wengi walikuwa hawana,ukiacha walimu.
2.Upendo kwa watu wengine,Wazee wa vijijini na watu wengine kwa ujumla Wana upendo wa dhati kama vile mmezaliwa pamoja,hawahangaiki kujua wewe ni nani unapokuwa na shida yoyote.
3.Kazi za mikono,Nilijifunza kulima,kukata kumi kwa weredi mkubwa sana, pamoja na kuwa mjini kwa Sasa,najitahidi sana kulima hata Bustani, mbogamboga si shida kwangu.
Na mengine mengi sana.Nawashukuru sana Babu na Bibi kwa kunilea vyema,Maisha yanasonga,hapo walikufa,wangali wakinena moyoni mwangu.