Faida za kula mayai ya kuku wa kienyeji

Faida za kula mayai ya kuku wa kienyeji

Somo zuri kaka Mzizi Mkavu....nimetoa uzi kuhusu kunywa maji ya limao asubuhi...utata ni kua je inafaa kuchanganya na asali? tusaidie mkuu wana jamvi
 
Somo zuri kaka Mzizi Mkavu....nimetoa uzi kuhusu kunywa maji ya limao asubuhi...utata ni kua je inafaa kuchanganya na asali? tusaidie mkuu wana jamvi
Mbona nimesha kujibu hakuna madhara kuchanganya Asali na limau na ikiwezekana weka pamoja na mji ya Uvuguvugu itakuwa bora zaidi kunywa pamoja.
 
There is cholesterol present in eggs but this does not usually make a great contribution to your level of blood cholesterol. "If you need to reduce your cholesterol level it is more important that you cut down on the amount of saturated fat in your diet from foods like fatty meat, full fat dairy products and cakes, biscuits and pastries."
Source: British Heart Foundation (BHF)
 
Fahamu kuhusu MAYAI

Je, unafahamu kuwa yai hulainisha koo?




Kama ilivyo kwa baadhi ya vyakula, yai hupoteza virutubisho linapopikwa iwe kwa kukaangwa ama kwa kuchemshwa.Yai lina Vitamin D ambayo hupungua pindi lipikwapo. Hupungua kwa asilimia 90 likichemshwa sana hivyo kupoteza umuhimu wake kwa mwili wa binadamu. Sasa basi, ili kupata virutubisho vyote vya yai ni muhimu kulila likiwa bado bichi.


Mayai mabichi ni mazuri kwa kula ili kupata lishe sahihi lakini kwa wale wenye aleji (allergy) mayai mabichi si sahihi kwao kwani inaongeza athari zaidi. Mayai pia huweza kuwa na vijidudu (bacteria) waitwao Salmonella enteritidis (SE) ambavyo vinatokana na ndege mwenyewe mfano kuku. Ni vizuri kuchunguza yai kabla ya kula ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza. Epuka kula mayai mabichi yaliyotagwa na kuku mgonjwa kwani ndio mwenye uwezekano mkubwa wa kuwa na SE.

Pata yai moja hadi mawili kwa siku. Yai halina shombo sana kwa hiyo ni rahisi kulinywa haraka likiwa bichi. Hizi ni faida za kula mayai kwa mwili wa binadamu:-
  • Mayai hupunguza athari ya tatizo la moyo kwa kiwango kikubwa sana.
  • Ni chanzo kizuri cha kupunguza protini iliyozidi mwilini.
  • Husaidia kuupa mwili mafuta kiasi yanayohitajika mwilini.
  • Huunguza na kupunguza kiwango cha mafuta yasiyohitajika mwilini.
  • Huondoa sumu iliyojificha mwilini.
  • Husaidia katika kuzifanya kucha na nywele kuwa ngumu.
  • Husaidia katika kuifanya mishipa na damu kufanya kazi kwa uzuri kabisa.
  • Mayai yanasaidia kutunza kumbukumbu.
  • Mayai yanavirutubisho aina ya foleti (folate) ambayo imetengenezwa vidonge, navyo vinashauriwa kwa wajawazito kuvinywa ili kupata chembe hai za damu.
  • Huleta kinga nzuri ya mwili ambayo hupunguza uwezekano wa kupata kansa kwa kiwango kikubwa.
  • Ni chakula bora chenye virutubisho vingi na vyenye kulingana (balanced diet).
  • Hufanya mfumo wa ubongo kufanya kazi vizuri.
  • Huleta usawa katika homoni (hormones).
  • Hulainisha misuli.
  • Huupa mwili nguvu zaidi.
  • Kwa wale wanywaji, mayai mabichi ni kiungo kizuri kuondoa hangover.
  • Inapunguza, kama sio kuondoa ngozi iliyoungua
Haishauriwi kutunza mayai katika friji ila yawekwe katika sehemu iliyopoa yaani ambayo haina joto kali wala baridi lililozidi. Ni muhimu kukagua yai kabla ya kulitumia hasa likiwa bichi; lakini sio tu kukagua mayai lakini kutumia mayai ya kienyeji kwani ndiyo yenye lishe zaidi.

Usile yai:-
  • lililopata ufa
  • lililotoboka
  • lenye harufu kali ama kidogo
  • lisilo na harufu kabisa ya yai
  • lililojepesi yaani halizami kwenye maji mfano kwenye bakuli
Njia nzuri ya kupata yai salama ni kwa kufuga kuku mwenyewe na kama hutaweza kwa sababu mbalimbali basi nunua mayai kwa mtu anayefuga mwenyewe ili kuwa na uhakika wa usalama wa afya yako.
 
Kuchanganya kwa Asali na Yai la kuku wa kienyeji ni Dawa ya nguvu za kiume unachanganya kiini cha yai bichi pamoja na Asali safi mbichi ya nyuki ukiipata ukikosa japo Asali tu pia itasaidia. Unakula kila siku asaubuhi mara moja halfau fanya vitu vyako kwa shemeji yangu utaona maajabu.
Nikichemsha tuu bila kula bichi
inafaa?
 
Kuchanganya kwa Asali na Yai la kuku wa kienyeji ni Dawa ya nguvu za kiume unachanganya kiini cha yai bichi pamoja na Asali safi mbichi ya nyuki ukiipata ukikosa japo Asali tu pia itasaidia. Unakula kila siku asaubuhi mara moja halfau fanya vitu vyako kwa shemeji yangu utaona maajabu.

Je unaweza changanya yai zima na Asali haitakua tatizo kimatumizi? au lazima iwe kiini tu?
 
Je unaweza changanya yai zima na Asali haitakua tatizo kimatumizi? au lazima iwe kiini tu?
Ndio unaweza kuchanganya yai zima na Asali ukakoroga na kula pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa wale wenjye upungufu wa nguvu za kiume ila upate yai la kuku wa kienyeji sio mayai ya kizungu hayafai kuliwa.
 
Ndio unaweza kuchanganya yai zima na Asali ukakoroga na kula pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa wale wenjye upungufu wa nguvu za kiume ila upate yai la kuku wa kienyeji sio mayai ya kizungu hayafai kuliwa.

Asnte sana.
 
Back
Top Bottom