Faida za kupitia JKT kwa wahitimu

Faida za kupitia JKT kwa wahitimu

Nitakujibu vizuri endapo utanipa faida tano za kujuwa kutumia silaha zote hizo ulizotaja kwa mwalimu au mwanafunzi wa chuo kikuu. Hii hela iliyotumika kuwapeleka wanafunzi hawa huko je huoni kama ingeweza kurumika katika kuleta faida kubwa zaifi ya hiyo? Hebu tuangalie tena je! Kupelekwa huko jeahini ndio kuwa wazalendo? Hamjaona jeshi likiasi??? Ukakamavu mnaousema pia siuoni kwani wanajeshi wa sasa hawana lolote hata kilometa kadhaa hawapendi kutembea na hata wakiwa na kazi nyingine ni bure tuu. Kama una mtazamo wa kuku kuangalia mwisho unapo kula basi tazama miaka 6 baadae utapata Jibu.

khs hela huu ni uwekezaji wenye faida za muda mrefu, pia kumbuka sisi tuliapa kama wanajeshi wa akiba wa jeshi letu hivyo faida ya kuzijua silaha ni pindi utakapohitajika kulitumikia taifa utumie uelewa huo kulingana na ulichoitiwa uwe ni mwalimu, dokta, mzururaji n.k
 
Hizi ni baadhi ya faida za kupitia jkt kwa wahitimu hasa kwa wale wanao shiriki kikamilifu.
Kwanza wana uvumilivu mkubwa ktk kila jambo pili ni wepesi wa kupokea amri zinazotolewa juu yao tatu ni wakakamavu na wana uwezo wa kupambana na mazingira magumu nne wana uelewa mkubwa juu ya silaha kama vile SRA56, SMG56 na G3, tano wana uwezo na uelewa juu ya shughuli mbalimbal za uzalishaji mali sita wana ujasiri mkubwa saba imewasaidia kujua reality(tabia) za mwenzao wanapokuwa ktk mazingira magumu hasa kwa madem nane wana heshimu mamlaka n.k
NB: ni kwa wale wanaoshiriki kikamilifu. Hivyo hili ni moja kati ya mambo ninayompongeza nayo Raisi wetu

Naomba kujua na hasara za kupita huko??
 
Baada ya mwaka, unarudi palepale. Experience ya jkt inakuwa kama ndoto flani tu. Wa mwaka jana uki-interact naoutafikiri hawakwenda. Miezi mitatu is nothing!
 
Mi nadhani hiyo hela inayotumika kupeleka vijana jkt ni bora wawekeze kwenye elimu ili vijana wa elimu ya juu waweze kuendelea na masomo yao kuliko wengine wanapata mkopo wengine hawapati hii inakatisha ndoto za watu hatakama umeenda jkt usipopata mkopo wakukuendeza elimu yako hiyo jkt ulioenda itakusaidia nini nadhan hiyo hela itumike kwenye elimu ili wale watoto wa wakulima waweze kuendelea na masomo yao
 
Yaani hapo mkuu unaingilia masirahi ya watu, hujui kama watu wanapiga ela kubwa kupitia huo mradi wa jkt? Ni hao viongozi wetu wanajiongezea mianya ya kula ela kwa kupata tenda ya kushona hizo sare, buti na mengine alafu kwa pesa iliyopitiliza alafu na hao madogo hata ela yao ya posho inakatwakatwa badala ya kupewa elfu hamsini wanapewa 30 kwa mwezi
 
jkt.makomando ohooooooo makomando.jkt makomando ohoooooo makomando!!!!!!da! nakumbuka mtabila 825KJ.jkt idumu inaanda vijana kwa mengi mema.
 
jkt.makomando ohooooooo makomando.jkt makomando ohoooooo makomando!!!!!!da! nakumbuka mtabila 825KJ.jkt idumu inaanda vijana kwa mengi mema.

natamani hawa wanaoiponda jkt waende halaf warud wawaelimishe mwenzio, yaan raha sana ukifungua moyo na ukanywa maji mengi moyo ukaelea
 
SAR haina tofauti na gobole kila ukipga lazima ukoki mkuu

hapana, SAR ukishaweka risasi kwenye magazine ukakoki mara moja una uwezo wa kupiga moja moja hadi ziishe bila kukoki tena tofaut na SMG ambayo ukifungua nusu usalama ukakoki ina weza kupiga zote kwa mfululizo rapidly
 
wote wanaopinga umuhmu wa jkt hawajapita huko "siri ya mtungi aijuae kata"
 
Ukakamavu ni swala endelevu vijana waliopita huko ndo kwanza siku hizi wanalala sana,ata push up hawapigi,na kujua silaha hizo(za kizamani) ni kituko!,pale unafunzwa kuvumilia hali zinazosababishwa na wengine mf. mshahara mdogo!,uvumilivu wa kizamani wakati the world is so sophisticated nowadays!,jeshi la akiba au frontier?,wewe jeshi la akiba huwa ni special force(yani makomandoo wa kunusuru nchi),nyie ni kujenga taifa hahahaaa wakati wajanja wameisha kula vyao mf BMK!
 
Hapana SAR unakoki kila baada ya kupiga risasi moja.
 
wote wanaopinga umuhmu wa jkt hawajapita huko "siri ya mtungi aijuae kata"

atujapita huko ila tunajua matatizo yake,wengine wazazi,ndugu marafiki walipita huko sifa kubwa ya huko ni kujisifia mafunzo(ambayo mimi nayaita ya kudhuru mental ability) mtu ukipitishwa jkt unaanza kuwa less sophisticated unaweza kula kwenye sufuria,wakati elimu inataka ule kwenye sahani!
 
Hapana SAR unakoki kila baada ya kupiga risasi moja.

Semi Automatic Rifle.

Ukijua maana ya hayo maneno huwezi kuandika ulivyoandika.

Semi automatic inamaanisha unabonyeza trigger kila unapotaka kupiga (baada ya kwisha kukoki mara ya kwanza).

Gobole (rifle) ndiyo unakoki (kupeleka risasi chemba) kila unapotaka kupiga pigo moja

Automatic rifle na Machine guns ndo ziko Fully Automatic....zina option za mapigo mengi kwa kila mminyo wa trigger au mminyo mmoja pigo moja.

Natumai nimeeleweka.
 
mkuu nashukuru kwa kumuelewesha maana alitaka anitoe roho
 
Ukakamavu ni swala endelevu vijana waliopita huko ndo kwanza siku hizi wanalala sana,ata push up hawapigi,na kujua silaha hizo(za kizamani) ni kituko!,pale unafunzwa kuvumilia hali zinazosababishwa na wengine mf. mshahara mdogo!,uvumilivu wa kizamani wakati the world is so sophisticated nowadays!,jeshi la akiba au frontier?,wewe jeshi la akiba huwa ni special force(yani makomandoo wa kunusuru nchi),nyie ni kujenga taifa hahahaaa wakati wajanja wameisha kula vyao mf BMK!

nani kakudanganya komando ni wanajesh wa akiba, sasa ujue komando anatangulia vitan hata mwaka mmoja kabla ya vita kuanza
 
Back
Top Bottom