Hata hii huduma ya JF hupitia Marekani pia. Asilimia 70 ya huduma za intaneti duniani hupitia Marekani.
Kama upo Mahaha, Dumila, Sumve, na Biharamulo na unakunywa Coca Cola au Pepsi au vinywaji vingine vinavyotengenezwa na hayo makampuni, ishukuru Marekani.
Kama unapenda Bongo Fleva, Afrobeats, au Amapiano, basi ishukuru hip hop [iliyovumbuliwa na Foundational Black Americans] ambayo ina ushawishi mkubwa sana katika hizo tasnia.
Angalia tu jinsi wanamuziki wake wanavyovaa, swaga zao, namna waongeavyo, na utagundua kuwa Wamarekani weusi wana ushawishi mkubwa sana.
Hata mfumo wa uongozaji wa urais, ishukuriwe Marekani maana huko ndiko ulikoanzia.