Hebu twende taratibu, uchunguzi wa anga si ugunduzi wa Marekani, na wala NASA si invention. Uchunguzi wa anga umeanza maelefu ya miaka.Ni kweli marekani imesababisha maafa na hasara katika angle mbalimbali za dunia na wote tunajua lakini pia kila nchi ina mazuri na mabaya yake hili hakuna wa kupinga
Sasa leo tuwape maua yao hawa marekani kwa gunduzi zilizofanywa kuisaidia dunia
Mimi nitaanza hapaa
1. Internet kagundua yeye leo hii tunaconnect bara kwa bara nchi kwa nchi
2. Personal computer PC
3. GPSS
4.Smartphone na OS (iOS, Android)
5.Uchunguzi wa Anga (NASA)
6.Mitandao ya Kijamii (Facebook, Twitter, YouTube)
7.Huduma za Mtandaoni (Cloud Computing)
haya mdau shuka na gunduzi za marekani wasiozijua wazijue
Cloud computing japo wazo limetoka marekani, ila nchi kibao zimehusika ikiwemo Germany ambayo ilitengeneza miundombinu ya usalama wa data na kanuni za faragha.
Uingereza nayo imehusika katika teknolojia hii.
Ukija kuangalia kwa umakini, utagundua vitu huwa vinagunduliwa nchi fulani na kuendelezwa nchi mbalimbali.
Mfano, gari iligunduliwa Germany, lakini Henry Ford akaleta mapinduzi katika uzalishaji wa magari kwa wingi baada ya kutembelea kiwanda cha kuchinja ng'ombe.
China ndipo printing na karatasi imegunduliwa, lakini ni WAjerumani waliofanya mapinduzi katika printing.
Ni kama sasa hivi ambavyo china ina patents nyingi zaidi za 5G kuliko nchi yoyote.