Faida za ulaji wa pilipili kwa mwili wa binadamu

X-PASTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
11,605
Reaction score
1,843


Faida ya Afya ya Kula Pilipili
Japokuwa Pilipili inaliwa na watu wa jamii mbalimbali, watu wengi hawazijui faida ya kiafya za kula pilipili.

Kwenye pilipili kuna kemikali iitwayo Capsaicin, ambayo ndio inayo sababisha muwasho na joto la pilipili.

Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu

Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.

Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili

Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!

Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)
Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.

BAADHI YA MICHANGO KUTOKA KWA WADAU:

-------------
-------------
-------------
-------------
--------------
 
Asante sana mkuu ni habari njema kwa walaji pilipili kama mimi na kweli mara nyingi nikipataga mafua huwa naweka pili pili nyingi kwenye supu ya kuku na husaidia sana.

kitu kingine kinaweza ku-support ni wahindi wengi naona wembamba japo kuwa vyakula vyao vina mafuta mengi, nadhani ni pilipili inawasaidia kwani vyakula vyao vina pili pili sana.
 
Ahsante kwa hii topic yako, mie mwenyewe iko penda sana kula pilipili.Tena sipendelei ya unga na penda ile pilipili fresh kuitafuna.
 
Ahsante kwa hii topic yako, mie mwenyewe iko penda sana kula pili pili.Tena sipendelei ya unga na penda ile pilipili fresh kuitafuna.

Nilivyoiona tu hii thread nikakumbuka wewe kumbe umeshatinga jamvini lol! Mimi ni mpenzi sana wa pilipili yaani hata chakula kiwe kitamu namna gani bila pili pili sikifurahii sana lol! na kukiwepo na pilipili tena ile kali basi hapo ndiyo utamu huongezeka. Kumbe zina faida yake mwilini! wacha tuzitafune tu.
 
asante kwa habari njema, mi nilifikiri najiumiza bure, kumbe inanitibu kiaina!!
 
lakini ni hatari kwa wenye matatizo ya vidonda vya tumbo kwani huongeza kiasi cha tindikali inayozalisha na tezi za tindikali tumboni
 
Lakini walaji wa pilipili hatuwaoni kwenye kula staftahi ya chai asubuhi au jioni.
 
Lakini walaji wa pilipili hatuwaoni kwenye kula staftahi ya chai asubuhi au jioni.

Mkuu fafanua hapo kwenye staftahi ya asubuhi na jioni. Nijuavyo mimi staftahi ni asubuhi tu...au kuna nyingine ya jioni pia?
 
ingekuwa tamu wengi tungeiweza but lol!
 
ingekuwa tamu wengi tungeiweza but lol!

hahahahahahah si mnaogopa kuwashwa! sasa wengine hapo ndiyo tunasikia raha za kupita kiasi na zinapokosekana msosi haupandi vizuri ati!
 
Mkuu fafanua hapo kwenye staftahi ya asubuhi na jioni. Nijuavyo mimi staftahi ni asubuhi tu...au kuna nyingine ya jioni pia?
Staftai ni kifungua kinywa, sasa kwa wale wanao funga si kifungua kinywa chao ni jioni mkuu?
 
Staftai ni kifungua kinywa, sasa kwa wale wanao funga si kifungua kinywa chao ni jioni mkuu?

Mkuu X-PASTER si wapenda pilipili wote wapenzi wa kukamata masanga na si wapenda masanga wote walaji wa pilipili na nimeshakutana na wengi katika makundi hayo mawili. Kwa hiyo unaweza kumkuta mpenda pilipili ambaye staftahi ni kama kazi hawezi kuikosa siku yoyote labda kama ni mgonjwa na chakula kimegoma kabisa kupita.
 
Asante sana X-P mie nakula pilipili kama Baniani mpaka watu wanasema nitapata madhara ...kumbe kuna faida
 
Pilix2 tamu ikiingia mwilini lakini ikitoka blaa!! Pia ni silaha ya kuzuia majambazi usiku, unawatupia machoni hafu unasikilizia muziki wake!!! Thenks sana
 
Have a look on the following publication


[QUOTE]Effects of red pepper on appetite and energy intake.

Yoshioka M, St-Pierre S, Drapeau V, Dionne I, Doucet E, Suzuki M, Tremblay A.

Physical Activity Sciences Laboratory, PEPS, Laval University, Ste-Foy, Québec, Canada.

Abstract

Two studies were conducted to investigate the effects of red pepper (capsaicin) on feeding behaviour and energy intake.

In the first study, the effects of dietary red pepper added to high-fat (HF) and high-carbohydrate (HC) meals on subsequent energy and macronutrient intakes were examined in thirteen Japanese female subjects.
After the ingestion of a standardized dinner on the previous evening, the subjects ate an experimental breakfast (1883 kJ) of one of the following four types: (1) HF; (2) HF and red pepper (10 g); (3) HC; (4) HC and red pepper. Ad libitum energy and macronutrient intakes were measured at lunch-time.

The HC breakfast significantly reduced the desire to eat and hunger after breakfast. The addition of red pepper to the HC breakfast also significantly decreased the desire to eat and hunger before lunch. Differences in diet composition at breakfast time did not affect energy and macronutrient intakes at lunch-time. However, the addition of red pepper to the breakfast significantly decreased protein and fat intakes at lunch-time.

In Study 2, the effects of a red-pepper appetizer on subsequent energy and macronutrient intakes were examined in ten Caucasian male subjects.
After ingesting a standardized breakfast, the subjects took an experimental appetizer (644 kJ) at lunch-time of one of the following two types: (1) mixed diet and appetizer; (2) mixed diet and red-pepper (6 g) appetizer.

The addition of red pepper to the appetizer significantly reduced the cumulative ad libitum energy and carbohydrate intakes during the rest of the lunch and in the snack served several hours later. Moreover, the power spectral analysis of heart rate revealed that this effect of red pepper was associated with an increase in the ratio sympathetic: parasympathetic nervous system activity.

These results indicate that the ingestion of red pepper decreases appetite and subsequent protein and fat intakes in Japanese females and energy intake in Caucasian males. Moreover, this effect might be related to an increase in sympathetic nervous system activity in Caucasian males.

[/QUOTE]

ncbi
 
Black pepper
Health Benefits

source

Mimi sio mpenzi sana wa pilipili,ila siku moja nilikuwa Jakarta International Airport on transit,dah..nili enjoy sana aisee zile recipes zao.
Cha mno ilikuwa ni ile balance ya pilipili,nikaondoka na instant noodles....zilisaidia kuondoa dalili za awali za flu
 
Mh! Nilikuwa siyajui haya.
Basi wahindi wananufaika sana kiafya kwani wao wanongoza kwa kutafuna pilipili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…