Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️
Leo ngoja nikupe faida za UMASKINI,.
Unaambiwa katika dunia kila kitu kina hasara na faida. Hivyo kabla kufikilia kufanya unashauliwa kuanza kuangalia pande zote mbili yaani (ADVANTAGE na DESADVANTAGE ) kimombo changu changu kinaweza kisiwe sawa ni kutokana na kiwango chagu cha elimu.
Pia kama wewe ni mpambanaji na unapambana juu ya umaskini na hali ya maisha uliyonayo kwasasa basi nikutie moyo pambana sana, kwamaana FAIDA za umaskini si lolote si chochote ukilinganisha na hasara zake.
Sina sababu za kumuelezea sana maskini kwa maana maskini wenyewe mnajijua na matajiri pia mnajijua.
Faida kubwa za UMASKINI
1. MASKINI HANA SIKU YA HUKUMU
maskini ukifa umekufa, maskini haukumiwi maskini ni laana ambayo Mungu alishakupa duniani na mahangaiko yako. Kama unahisi kuwa utahukumiwa ukifa wewe sio maskini labda wale matajiri.
Maskini haambiwi atoea sadaka wala haambiwi aende kuiji makka wala haulazimishwi kwenda ibadani wewe ibada yako ni kuhangaika. Nenda kahangaike na kulipia watoto ada, nenda kahangaike na pango za nyumba nenda kahangaike na kula maswala ya kwenda kuimba ibadani waachie walio jipata, na Mungu atakuwa pamoja na wewe.
2. MASKINI HAFIRISIKI
Maskini hawazii sijui kufirisika, sijui kushuka kiuchumi,.
Maskini akipata poa akikosa poa pia.
3. MOYO WA MASKINI NI WENYE UTULIVU
Ndio maskini hupata tabu ya mwili, ila kapewa amani ya akili na mwenye moyo mtulivu na amani.
Maskini haitaji ulinzi wa mabaunsa mlangoni kwake, wala haitaji kupima chakula kabla ya kukila. Maskini huokota tunda na kulila bila kuwaza, tena bila kuzulika.
4. MARA NYINGI ANAKUWA HURU
mara nyingi anakuwa jamiiforum, mara nyingi anakuwa kijiweni kwenye vijiwe vya kawaha nk, mara nyingi hupenda kuzunguka zunguka na kuranda mitaani huku na kule na ndio wengi wao tunawaona facebook instagram na X.
5. KUNYWA POMBE ZA KIENYEJI
Kati ya vitu maskini huwa anafaidika navyo ni pombe za kienyeji, pombe ambazo zimejaa mambo mengi mazuri na yenye furaha.
6. UMASKINI HUFA JASIRI
Maskini haachi majumba makubwa , magari wala viwanja.
Huchumia tumbo lake mpaka mwisho wa pumzi yake.
Huyu ndio mwamba, anakuja kwenye dunia na kuondoka bila kuacha ushahidi. Mr silent