Faida za Yanga na Simba kuingia nusu fainali

Zouzoutz

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
1,883
Reaction score
2,732
Ukiacha Usimba na Uyanga pembeni kuna faida kubwa ya timu zetu kuingia nusu fainali kuliko unazi wetu

a) Kwanza Simba atapanda kiwango na rank toka point 39 mpka 54
Hiyo ni regardless kama Es Tunis atafuzu

b) Hivyo hata msimu ujao wa kwenye upangaji wa makundi atapanda Toka pot 3 kwenda pot 2 au pot 1 kabisa kutegemeana kama atafika fainali

c)Yanga naye atapanda rank na kiwango toka point 31 mpka 46 regardless kama TP Mazembe na Petro de Luanda nao watafuzu

d) Hivyo hata msimu ujao kwenye upangaji wa makundi atapanda Toka pot 4 kwenda 3 au hata pot 2 kutegemeana kama atafika fainali

e) Uwezekano wa kombe kubaki Bongo ni mkubwa

Kwani Simba akipita atakutana aidha na Mazembe au Petro de Luanda huku Yanga akikutana na aidha Asec Mimosas au Es Tunis

Hapo tayari Uwezekano wa WOTE kwenda fainali ni mkubwa kwani hizo timu siyo ngumu kivile ukilinganisha na Al Ahyl na Mamelodi Sundowns

f) Ni sifa kubwa kwa mpira wetu na nchi yetu

Maadmnin WOTE wa page za CAF iwe X, Insta, FB na Threads wanalijua vibe la wabongo kwenye page zao

Najua wanaomba Simba na Yanga ziendelee kuwepo Ili mashabiki wao waendelee kuongeza engagements kwenye pages zao

Hata yule mickyjr anajua umuhimu wa wabongo mitandaoni ndo maana haishi kutugombanisha wanasimba na wanayanga kwenye kurasa zake Ili tu tujibizane apate engagements

All in all, ningependa WOTE twende nusu.

Halafu tukutane fainali tukate mzizi wa fitina wa nani mbabe.

Screenshot_20240405-112027_1.jpg
 
Marekebisho:

Ukivuka hatua moja kwenda hatua nyingine unaongeza point 5 hivyo kama Yanga itafuzu nusu fainali basi watakuwa na point 36 kutoka kwenye 31 alizokuwa nazo awali.
Simba pia kama watavuka kwenda nusu watakuwa na point 44 kutoka point 39 alizokuwa nazo awali.
 
Marekebisho:

Ukivuka hatua moja kwenda hatua nyingine unaongeza point 5 hivyo kama Simba itafuzu nusu fainali basi watakuwa na point 36 kutoka kwenye 31 alizokuwa nazo awali.

Ebu nipe mchanganuo wa Yanga toka point 20 za msimu uliopita mpaka 31 za sasa
 
Yanga alipata point 20 kwasababu alifika fainali ya kombe la shirikisho CAF ila hakubeba kombe hivyo alijikusanyia point 4 ambazo zinazidishwa na msimu husika ambapo ndio ilikuwa msimu wa 5. Hivyo 4x5 = 20

Kwa msimu huu Yanga mpaka sasa inacheza robo fainali hivyo ameshajichukulia point 3
Hivyo huu ndio utakuwa ndio msimu wa tano na ule wa mwaka jana utahesabika msimu wa 4 hivyo itakuwa 4x4= 16 utajumlisha na msimu huu hadi sasa ni 3 x5= 15 ndio utapata jumla ya point 31.

Kama Yanga ikifuzu na kuingia nusu fainali ina maana atakuwa na point 4
Hivyo utachukua zile 16 za msimu uliopita utajumlisha na 4 x 5 za msimu huu utapata jumla point 36.

Kama Yanga atafanikiwa kucheza fainali msimu huu ina maana atakuwa na point 5 kisha zidisha kwa 5 utapata 25 kisha jumlisha point 16 za msimu uliopita uliopita utapata jumla ya point 41 na kwa Simba ni hivyo ni kwamba hadi sasa wameshafuna point 15 msimu huu na misimu minne nyuma walikuwa na point 24 ndio maana wana point 39.
Wakifuka hatua hii ya robo watakuwa wamefuna point 20 ndani ya msimu huu (4 x5)
 
Asante kwa ufafanuzi
 
Simba kupangwa pot namba 2 haitomuhitaji afike nusu fainali.

Pot namba 2 inapangwa kuzingatia consistency ya misimu mitano ya CAF.

Simba kwa sasa ni namba 5 kwa ubora maana yake katika zile timu 4 zinazokaa pot 1, Simba atakuwa chini ya hao tu kwasababu wako juu yake kwenye ranks.

Nje na hapo vinabo wengine wote watakuwa chini ya Simba kwenye group stage.
 
Marekebisho:

Ukivuka hatua moja kwenda hatua nyingine unaongeza point 5 hivyo kama Simba itafuzu nusu fainali basi watakuwa na point 36 kutoka kwenye 31 alizokuwa nazo awali.
Simba pia kama watavuka kwenda nusu watakuwa na point 44 kutoka point 39 alizokuwa nazo awali.
Hapa naona umekuwa kama Rais wa TFF wakati anazungumzia uzalendo wa kuvaa jezi😜
 
Uwezekano wa kombe Gani litabaki Tanzania Champions leauge hii au kuna kombe jingine kwa kuongezea leo nimetoa sadaka kuombea Yanga watoke kwenye ligi ya mabigwa
 
Marekebisho:

Ukivuka hatua moja kwenda hatua nyingine unaongeza point 5 hivyo kama Yanga itafuzu nusu fainali basi watakuwa na point 36 kutoka kwenye 31 alizokuwa nazo awali.
Simba pia kama watavuka kwenda nusu watakuwa na point 44 kutoka point 39 alizokuwa nazo awali.
Hawa makolo wanapenda sana kuchezea takwimu
 
Kombe pekee linaloweza kubakia nchini ukiana NBC Premier League ni MAPINDUZI.
 
Back
Top Bottom