Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

nionyeshe sehemu ilipoandikwa uislam ni kujisalimisha na unyenyekevu
Ni nini maana ya Uislamu?

Jibu:
Maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumpwekesha na kufuata maamrisho yake kwa utii na kuepukana na shirki kama Allaah Anavyosema:

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyeuelekeza uso wake kwa Allaah naye ni mtendaji mema na akafuata Dini ya Ibraahiym haniyfaa (aliyejiengua na dini potofu akaelemea Dini ya haki). Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni khaliyl (kipenzi).[1]

Anasema pia:

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗوَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾

Na anayesilimisha uso wake kwa Allaah, naye ni mtenda wema, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. Na kwa Allaah ni mwisho wa mambo (yote).[2]

Na Anasema pia:

فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ ﴿٣٤

Basi Ilaahu[3] wenu ni Ilaahun Waahid (Mungu Mmoja Pekee); basi kwake Pekee jisalimisheni. Na wabashirie wanyenyekevu.[4]

[1] An-Nisaa (4: 125)
[2] Luqmaan (31: 22)
[3] Mungu Anayestahiki kuabudiwa kwa haki.
[4] Al-Hajj (22: 34)

Chanzo: 013 - Ni Nini Maana Ya Uislamu? | Alhidaaya.com
 
hapo umetoa maana ya uislam au umesema muislam anatakiwa afanyanye nini
 
Faiza ni kweli kuwa kipindi hiki hapa nyuma kidogo ulipoadimika hapa jamvini ulikua Afghanstan na kikundi cha Islamic State ukipata mafunzo ya kigaidi?
Ugaidi ni haram katika Uislam. Hutopata mafundisho hayo katika Uislam. Kumbuka hilo.
 
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.

Update 1:
Tafadhalini tuulize maswali kiheshima . Heshima ni kitu cha bure na hii JF yetu pendwa inasomwa na wengi, tujiheshimu.

Update 2:
Siku kadhaa zimepita toka tuanzishe uzi huu na nimesikitishwa na aina ya maswali yanayoulizwa kwenye huu uzi.

Tumetowa fursa ya kuulizana na kila niwezapo kujibu au kutafuta majibu muafaka kutokana na hayo maswali na fursa ya wachangiaji kujibu maswali yatakayojitokeza ya "general knowledge" lakini hadi hii leo ni maswali machache sana yenye faida kwa wengi yameulizwa. Maswali yaliyojaa ni amma ya kutaka kuanzisha ubishi "ligi" na amma yamelenga mtu binafsi, hususan amelengwa mleta mada. Ni masikitiko makubwa sana.

Nnawashauri wote waliouliza maswali yenye kulenga binafsi na wale waliouliza maswali yenye kubomoa badala ya kujenga wabadilike na waanze kuuliza maswali yenye kujenga, kuelimisha, kutujaza hekima na maarifa.

Nilipoweka aina ya elimu niliyoisomea nilidhani ntakumbana na kibano kikali kuhusu hilo na nijibu ili iwe faida kwa wengi lakini kwa bahati mbaya au nzuri hakuna hata mmoja aliyeuliza swali lolote kuhusu hilo.

Isitoshe, mna fursa ya kuuliza kuhusu chochote. Ndege, mimea, dunia, sayari, nyota, maajabu, maswali yasiyokuwa na majibu, viumbe kwa ujumla vinavyojulikana na visivyojulikana, maajabu ya duniani, elimu na vitu vingi kama hivyo na vinginevyo.

Nnauhakika wale walioleta maswali ya kiajabu ajabu ya ubishi wana mengi sana ya kuuliza yanayoweza kuwapa faida wengi na kuna wengi kati yao wana mengi wanayajuwa na wanaweza kuchangia kwenye majibu kwa faida ya wengi.

Ombi langu kwa wote ni tuboreshe aina ya maswali na majibu.

Karibuni.
uke una urefu gani /kina gani kwenda ndani?
 
Naam, ni kweli ni Muislam na wanaomfahamu na wasio mfahamu hilo lipo wazi, sijdah haipatikani bila ya kuswali na yake ipo wazi kabisa. Ma shaa Allah.
Assalam aleykum warahmatulla

Mama yangu mpenz i FaizaFoxy mimi ni kijana mdogo ambae unaweza kunizaa na kunihandle kama mwanao kiukweli nakuheshimu kama mama yangu.

Mimi nataka ushauri hapa hadharani,kuna uzi wangu huu kutaka ushauri kwa watu,ila bado sijapata kutoka kwako naomba nawe unishauri mama yangu.

Ushauri wenu,nimefikiria nimeona nirudi shule kusoma,nisomee nini wakuu? - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom