Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Imeandikwa wapi muislam mpaka ukubali hadithi??
Kwahyo wewe unakunywa mkojo wa ngamia?
Unasafisha pua asubuhi kumfukuza shetani?
Unazamisha nzi bawa zote akiangukia kwenye chakula?
Unakojoa na kunya ukiitizama kibla?
Unakunywa hata maji ya mtoni kwakuwa maji hayawezi kuwa machafu?
Unaua makafiri mpaka wasilimu?
Unafadhili magaidi?
N.k n.k n.k n.k ??
 
Unaamini kuwa kuna hadithi za Mtume japokuwa hauzikubali?

Unaamini kuna hadithi za Mtume anayeitwa Muhammad?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadith zote ni hadithi na zitabaki kuwa hadith kwa maana halisi ya neno hadith.

Naamini, hakuna hata moja ambayo ni "hadith ya mtume" kama wengi wanavyotaka ifahamike. Hizo ni hadith (riwaya) za watu wengine walioelezea wanavyodhani au wanavyofikiri ilivyokuwa wakati wa Mtume au waliokuwa karibu na Mtume, zinaweza kuwa kweli au uongo. Zote za kuokoteza okoteza miaka takriban 200 baada ya Mtume Kufariki.

Mfano, Mimi nikwambie "Magufuli kasema hasaidii mtu ataesombwa na mafuriko Rufiji", hiyo hadith ni ya Magufuli au yangu namuongelea Magufuli?

Au Mimi nihadithie " nilimuona Nyerere kashuka kwenye gari anasalimiana na watu Lumumba", hiyo hadith ya Nyerere au yangu naelezea ya Nyerere?

Mimi nasema hizo ni hadith zangu si za Magufuli wala Nyerere.

Ingawa naamini kuwa hizo hadith zote si za Mtume Muhammad na kwa kuwa hizo hadith zote zipo na waliozikusanya na kuziandika wamejitahidi na hakuna kati yao aliyeandika kuwa hizi "hadith za mtume" (kama yupo basi kakosea) bali wanaandika "kahadithia fulani...". Waliandika kama historia tu, miaka takriban 200 baada ya Mtume Muhammad na masahaba (marafiki) zake kufariki.

Katika hizo hizo pia zote zinazopingana na mafundisho ya Qur'an sizikubali.

Zote zenye lugha isiyokuwa na adabu sizikubali.

Zote zote ambazo hukuti maudhui yake kwenye Qur'an sizikubali.

Umeelewa? Wajulishe na wenzako wanaojiita Zurri na safuher.
 
Acha porojo wewe. Weka hizo hadith tukufundishe...
 
Nimekuelewa vzr sana

Ni heri wewe uliyeamua kubaki na Quran pekee .
 
Nakubali hadith zote za ndani ya Qur'an. Kumbuka hilo. Nyinyi ndiyo wale ambao mnazuwa kuwa huwezi kuielewa Qur'an mpaka usome "hadith", Soma Allah anawaambia nini...

Qur'an 41:

44. Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni wangeli sema: Kwanini Aya zake haziku pambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur'ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.
44
 
Hiyo "vitabu vya Mungu" ni vipi?tuvichambue, maana unaweza kuwa umedanganywa.
 
Si weka tuwafundishe.

Unataka kujifunza Uislam kutoka kwa
asiye Muislam?
Usitake kusema uislamu hatuujui, Mimi binafsi nimezaliwa familia ya kiislamu na nili ritard , na wakanitenga , Na madrasa nimesoma

Hadithi umesema huzikubali ,tukiweka hapa utaanza kuzipinga au kuzikataa


HAYA TUFUNDISHE KUHUSU HIZI HADITHI



Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa: Mtume (s.a.w) amesema, "Ye yote mwenye kutukana, basi huyo amejambiwa na Shetani katika Mdomo wake." (Fat'hul Baary J. 10, Uk. 176)


SHETANI ANALALA KWENYE PUA ZA WAISLAMU:

Amesimulia Abu Huraira (r.a) Mtume (s.a.w) alisema “Mmoja wenu anapoamka kutoka usingizini, basa atawadhe na apandishe maji puani, na apenge mara tatu, kwa sababu shetani alilala ndani ya tundu za pua yake” (Bukhari, Hadithi na. 516, juzuu ya 4)



Kasema Mtume (s.a.w) “Anamwijia mmoja wenu shetani katika sala, basi anapuliza (anampuliza) katika matako yake, basi yule mtu inamwijia fikiria ya kuwa umemtoka upepo (kajamba) nae haukumtoka, basi akiona hali hiyo asiondoke kwenye sala mpaka asikie sauti ya kumtoka huo upepo au anuse harufu yake”. (KITABU CHA MKWELI MWAMIU, JUZUU YA 1 -2 HADITHI NA. 74, UK 42)



MUHAMMAD AMTUKANA NA KUMLAANI MTOTO YATIMA
Nabii Muhammad alimtukana na kumlaani mtoto yatima aliye kuwa na Umm Sulaim (Ambaye ni mana ya Anas). Sahih Muslim, Book 032, Number 6297)
 
Anababaisha tu huyu mama.hizo sheria za mwizi kukatwa kiganja anaikataa anasema qurani imesema mkono tu.
Kiufupi anakataa mambo mengi ya uislamu kazi yake kunukuu aya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Unataka nikunukuu wewe peke yako? nisiinukuu Qur'an?

Hakikatwi kiganja kijana, kinachokatwa ni mkono au huelewi kiganja kinaishia wapi na mkono unaanzia wapi?
 

Uislam hauujuwi.

Hakuna "hadith" za kiswahili weka kama zilivyoandikwa (original) ambatanisha na hiyo "tarjama" (tafsiri) yako. unaweka "tarjama" unasingizia "amesimulia Abu Huraira"? Abu Huraira lini alijuwa Kiswahili? Nani aliyeandika hiyo tarjama?
 
Siujui kivipi ,wewe unadhani kwa kuwa sasa sipo kwenye uislamu basi siujuwi , hayo ni mawazo mfu

Mimi kwa taarifa nimezaliwa humo na kukulia humo na madrasa nimesoma ,

Siku ya kuukana uislamu niliukania msikitini kwa kuhojihana maswali na sheikh

Hizo hadithi hutaki zitafsiriwe? Kwa hiyo lugha ilizoandikwa hazitafsiriki?

Au ndio vichaka vya kukataa ukweli?
 
Naomba ufafanuzi wa maana alama ya nyota na mwezi juu ya misikiti tafadhali.
Uislam hauna alama yoyote kiitikadi.

Kihistoria hiyo ni alama (symbol) iliyotumiwa na utawala wa Himaya ya Othman (Ottoman Empire) ambao ulitawala kwa misingi ya Kiislam popote ulipokuwepo.

Misikitini (mengine si yote) wakaweka kujulisha hapa ni pahala pa Waislam.

Ingawa Uislam hauna ishara inayohusishwa nayo kielimu, ishara ya mwezi na nyota (hilal katika Kiarabu) Kwa sasa hutumiwa sana kuashiria Uislam.

Miale mitano ya nyota zinazowekwa huwakilisha nguzo tano za Uislam, Mwezi huwakilisha mbingu (Outer Space) kote ufalme wa Allah umetanda.

Ikiwepo isiwepo hiyo alama haina umuhimu zaidi ya kujulisha tu huu ni msikiti. Haihusiani na ibada yoyote ya Kiislam.
 
Kuzaliwa na Waislam hakumaanishi unaujuwa UISLAM.

Ungeujuwa Uislam usingethubutu kuritadi.

Sasa rudi ulete hadith siyo porojo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…