Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

habari faiza foxy....kuna mtu kitaan kwetu anaweza kumsomea dua mwanamke anayemtaka kwa kuchukua jina la mama yake na huyo mwanamke akawa aambiwi asikii kwa huyo jamaa..je kuna ukweli wowote juu ya hili au mchizi ana dawa zake za ziada
 
HARUFU umenikumbusha mbali sheikh Wangu.
Mwenye EZ Mungu akuzidishie Elmu Na Akuruzuku Hekma ili utufundishe Na sisi.
Kwa kweli nalifurahia Hilo darsa la dadaFaiza foxy Na wachangiaji wote.
AAMIIN.

Labda kwa kukazia nikazie kwa hivi,

QAALA RASUULULLAHI SWALLA LLAHU A'LAYHI WASALLAM:-

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Amani iwe juu yake).

IDHAA MAA TAA IBNU AADAMA INQATWA'A AMALUHU ILLAA MIN THALAATH,

Pindi Akifa/Anapokufa Mwanaadam, Amali zake zote zinapotea isipokuwa mambo matatu.

Ambayo,

1. SWADAQATUN JAARIYA.

2.AW ILMUN YAN TAFIUBIH.

3.AW WALADUN SWAALIHUN YAD'ULAH.

Nikiwa na maana,

1.SADAKA inayoendelea/ya kuendelea. Yaani kiuchache ni kama vile, Kumfundisha Mtu Swallah/Sala, Kumfundisha Mtu QUR'AAN, Kumuelekeza Mtu kutoa ZAKA. Haya machache niliyoyataja nikisema niyachambue, DARSA lake ni kubwa mno na ni refu mno, nimejatihidi kutaja kiufupi ili nieleweke.

2.ILMU yenye kunufaisha/Manufaa. Kivipi? ILMU ambayo imewawezesha Watu. Na hapa napo DARSA lake ni kubwa pia, najitahidi kufupisha.

3.Au Mtoto Mwema ambae anakuombea DUA. Kivipi? Nikiwa na maana, Mtoto mwenye kujua/kuijua DINI.

Yule Mtoto ambae atakuwa Mwema, atakuwa anamuombea/anawaombea DUA Mzazi wake/Wazazi wake.

Hapa napo pana DARSA lake ila najitahidi kufupisha.

Kiufupi Sheikh wangu mgogoone, lengo langu hapa ni kukumbusha na kutiliana mkazo kwenye ILMU, ikiwemo Vizazi vyetu. Kumbuka Mimi na Wewe tusipokuwepo hapa Ulimwenguni, Watoto wetu, wao ndio watakaotukumbuka Sisi (Watakaotuombea SISI) Muhimu tuwaandalie mazingira mema na bora ya ILMU.

Kwa mfano hai wa hapa Bibie FAIZA, ILMU anayoitoa anajiwekea Akiba mbeleni, kwa watakaoifanyia kazi itawasaidia, na hapo kipengele namba Mbili, kipengele cha Pili kinamuhusu Bibie FAIZA, ambacho kinasema:-

AW ILMUN YAN TAFIUBIH
 

Akhsante sheikh HARUFU Kwa darsa Na Kwa kuongezea kuhusu sadak ya Tabasamu maana hiyo NI sadak ambayo unatoa nabado unayo.
Kila la kheri
 
Wahabb inatokana na jina la babu yake na muhammad ibn abdul wahhabb, uislam utabaki kuwa hivyo ila mengine ni changamoto tu. Tusome quran na mafundisho ya mtume, huyu muhammad ibn abdul wahabi kuna baadhi ya waislam wanamkubali kutokana jinsi anavyozingatia sunna pia kuna wengine wanampinga
Mama unawatambuaje WAHHAB ni waislam halisi na itikadi zao Zinamashiko kwenye dini.? Hata kwa dondoo fupi .
 
nami naomba histori fupi ya muhamad toroha na simba ulanga
 
Jazakallah kheyra
 

MgungaMiba unanifurahisha unavyo mjibu
Kama nakuona Vile.Majibu NI mazuri sana Na nimejifunza Mambo mengi.
Darsa la Faiza Foxy lidumu
 
Habar zenu wakubwa, mm ni mgeni humu naomba mnifahamishe how to creat and posting thread. Najua kua hapa sio mahali pake nisaidie
 
kwa hiyo wewe kwenye form za kiofisi ambazo wanauliza date of birth unawajibugi hivi ulivyojibu hapa?
Kuna tofauti kati ya kujibu/kuwajibu na kujaza.

Ujue hapo ni vitu viwili tofauti.

Kujaza fomu unamalizana kimyakimya, na wala hauUtangazii uma ulichokijaza.

Ila kwa hapa akisema ajibu itakuwa anautangazia uma na pengine yeye mwenyewe muhusika mkuu hayuko tayari.

Je hapo huoni mantiki yoyote?
 
Je, nchi gani zingine zina huu utamaduni wa utani, hususan katika Africa kama tufanyavyo sisi.

Asante!
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Kamari ni dhambi kubwa nafikiri watambua hili sijui kwanini wajiendekeza nalo.


Unaniambia mimi, au sijakuelewa?

Kama ni mimi, hapana, mimi sichezi kamari "unless" uwe na maana nyingine ambayo sijaielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…