Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Uzi upo usome. Una mengi sana, usingoje kila kitu kufanyiwa.

Ungeisoma post namba moja, ungeelewa kuwa maswali humu hayajibiwi na mtu mmoja tu.

Kumbuka, kiwango cha elimu hakipimwi kwa madarasa, uelewa, ujuzi na muono wa uhakika haupatikani kwenye kuta nne.
Asante mama.Je una maoni gani kuhusu kifungo cha mh.Mbunge wa Kilombero?Je bado kuna haki katika nchi yetu au tunafanya siasa za uonevu na kibabe?
 
Je, hilo swali lilikuhusu wewe? Kama jibu ni "hapana"...kwa nini umejibu? Au huko ndio kujipendekeza? Je, una tabia za kujipendekeza? Je, tabia hizi ndizo zilikufanya uolewe ukiwa na miaka 14? Kama jibu ni ndio fafanua kwa kina.

Kasome post namba moja.

Hii ni open forum, kama hutaki kujibiwa na wengine jifunze kuwauliza kwa pm.
 
Kasome post namba moja.

Hii ni open forum, kama hutaki kujibiwa na wengine jifunze kuwauliza kwa pm.
Je, kujifunza ndo kulikufanya uolewe ukiwa na miaka 14? Ulihitaji kujifunza nini kupitia ndoa ya utotoni? Au yale mambo ya wakubwa? Ina maana ulishobokea dushelele? Kama jibu ni hapana fafanua kwa kina.
 
Hiyo ni "controversy" ambayo binafsi kwa kuwa ni Muislam siioni kama ina faida yoyote kwa yeyote.

Rangi na muonekano wa mtu si ubora wake, mbora kati yetu ni mcha Mungu na nnaamini Yesu alayhi salaam alikuwa ni Mtume wa Mungu na tunachotakiwa tupate ni ujumbe wake aliotumwa kutufikishia na si rangi yake.

Jaribu ku Google kidogo kuhusu hilo uone jinsi watu walivyoacha kufuata mafundisho ya Yesu alayhi salaam na kuanza kubishana kuhusu rangi yake.
mbora-ubora
 
Ni ipi hukmu ya mwanamke ambaye yupo kwenye hedhi pindi yupo hija na bado hajafanya twawafu?
 
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.

Update 1:
Tafadhalini tuulize maswali kiheshima . Heshima ni kitu cha bure na hii JF yetu pendwa inasomwa na wengi, tujiheshimu.

Update 2:
Siku kadhaa zimepita toka tuanzishe uzi huu na nimesikitishwa na aina ya maswali yanayoulizwa kwenye huu uzi.

Tumetowa fursa ya kuulizana na kila niwezapo kujibu au kutafuta majibu muafaka kutokana na hayo maswali na fursa ya wachangiaji kujibu maswali yatakayojitokeza ya "general knowledge" lakini hadi hii leo ni maswali machache sana yenye faida kwa wengi yameulizwa. Maswali yaliyojaa ni amma ya kutaka kuanzisha ubishi "ligi" na amma yamelenga mtu binafsi, hususan amelengwa mleta mada. Ni masikitiko makubwa sana.

Nnawashauri wote waliouliza maswali yenye kulenga binafsi na wale waliouliza maswali yenye kubomoa badala ya kujenga wabadilike na waanze kuuliza maswali yenye kujenga, kuelimisha, kutujaza hekima na maarifa.

Nilipoweka aina ya elimu niliyoisomea nilidhani ntakumbana na kibano kikali kuhusu hilo na nijibu ili iwe faida kwa wengi lakini kwa bahati mbaya au nzuri hakuna hata mmoja aliyeuliza swali lolote kuhusu hilo.

Isitoshe, mna fursa ya kuuliza kuhusu chochote. Ndege, mimea, dunia, sayari, nyota, maajabu, maswali yasiyokuwa na majibu, viumbe kwa ujumla vinavyojulikana na visivyojulikana, maajabu ya duniani, elimu na vitu vingi kama hivyo na vinginevyo.

Nnauhakika wale walioleta maswali ya kiajabu ajabu ya ubishi wana mengi sana ya kuuliza yanayoweza kuwapa faida wengi na kuna wengi kati yao wana mengi wanayajuwa na wanaweza kuchangia kwenye majibu kwa faida ya wengi.

Ombi langu kwa wote ni tuboreshe aina ya maswali na majibu.

Karibuni.
Hali Yako.. swali langu.. muislamu mwanaume anaruhusiwa kuowa msichana WA Dini nyenginge?? Na je msichana WA kiislamu anaruhusiwa kuolewa na mwanaume WA Dini nyengine?
 
Ni ipi hukmu ya mwanamke ambaye yupo kwenye hedhi pindi yupo hija na bado hajafanya twawafu?
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Mwanamke mwenye kwenda Makkah kwa nia ya kutimiza fardhi ya Hijja, akapata hedhi yake, anatakiwa aendelee na ibada zote nyingine wanazofanya mahujaji isipokuwa kutufu Ka’abah ambayo ni sawa na Swalah. Kwa hiyo ataacha pia kuswali kama ilivyo kawaida ya wanawake wanaopata hedhi kuwa wamezuilika kuswali na kufunga.

Dalili ni kutoka Hadiyth ifuatayo:

عن عائشة -رضي الله عنها- أن رسول الله -صلى الله عليه وسلم- دخل عليها وهي تبكي، فقال ((أنفست؟))" (يعني: هل جاءتك الحيضة؟) فقالت: نعم، قال: ((إن هذا شيء كتبه الله على بنات آدم، فاقضي ما يقضي الحاج، غير ألا تطوفي بالبيت حتى تغتسل))" رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa bibi 'Aishah (Radhiya Allahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia (katika hema lake) akamkuta analia akasema: ((Je umepata hedhi?)) akasema: "Ndio". Akasema: ((Hii ni amri Allah Aliyowaandikia wasichana wa Adam, fanya yote wanayofanya mahujaji isipokuwa kutufu Ka’abah hadi utoharike)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Ibada nyingine zote zinazofanyika katika msimu wa Hajj ni zifuatazo:

- Kufanya Sa'ay (Kutembea Asw-Swafaa na Al-Marwa) mara saba.

- Kwenda Minaa kulala huko kwa ajili ya kutimiza nguzo nyingine.

- Kusimama 'Arafah

- Kulala Muzdalifah

- Kufanya jamaraat (kupiga mawe nguzo)

- Kuchinja

Na katika nyakati hizo zote anaruhusiwa kufanya dhikr za aina yoyote kama kuomba du'aa, kusoma Qur-aan, kusoma vitabu vya Dini, kufanya dhikr za tasbiyh (Subhaana Allaah) tahliyl (Laa ilaah Illa Allaah) tahmiyd (AlhamduliLLaah, takbiyr (Allaahu Akbar) na aina yoyote nyingine zilizothibitika katika Sunnah.

Atakapomaliza hedhi yake akakoga josho (ghuslu) atakwenda kufanya Twawaaf alizoshindwa kuzifanya, ikiwa ni Twawaaf ya 'Umrah au Twawaaf ya Ifaadhwah.

Na Allaah Anajua zaidi

Mwanamke Mwenye Kupata Hedhi Akiwa Katika Hajj Afanye Nini? | Alhidaaya.com
 
Kwa nini waislamu mkaamua kuwanyanyapaa wanawake wenye hedhi? Kwani wao kosa lao ni nini haswa mpaka wasiruhusiwe kufanya sawa ya jumla kama watu wengine?. Na pia mbona mkisali mnawaweka nyuma?? Au ndio hivyo tena mnaogopa kuu face mzigo
 
Nna shahada ya kwanza ya Electronics Engineering, Major in (Tele)communications (Canada, 1982).
Kwa nini hukuamua kujiendeleza na Elimu ya Masters au ziada?? Kwa nini ukaamua kubakia na hiyo shahada moja tu kwanzia mwaka 1982??
 
Kwa nini hukuamua kujiendeleza na Elimu ya Masters au ziada?? Kwa nini ukaamua kubakia na hiyo shahada moja tu kwanzia mwaka 1982??

AlhamduliLlah ndipo nilipojaaliwa.

Isitoshe, familia na majukumu ya wanangu yalikuwa ndiyo kila kitu kwangu and I had to give them my whole self.
 
Back
Top Bottom