Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa


screpa

Nilikuuliza swali baada ya kukujibu swali lako huko juu, hujanijibu.
 
Hapana sijaolewa. Kwetu kuolewa ni mwiko.

AlhamduliLlah, mimi na mume wangu tumeoana kwa zaidi ya miaka 35 hivi sasa.



Kwa hyo vipi hauwezi kuwa mchepuko wangu aiseee, coz ni siku nyingi huwa nakulia mingo
 
Tesla alikuwa ni mvumbuzi si mfanya biashara.

Wametengeneza gari sasa hivi za umeme kwa kutumia teknolojia yake ya betri na super charger aliyoivumbuwa miaka mingi sana iliyopita , zinafanya kazi vizuri na zinauzika sana kuliko gari yoyote ya umeme na imepewa jina hilo hilo Tesla:


Source na soma zaidi: Tesla Motors | Premium Electric Vehicles
 


Hayo ni mambo ya 'X and Y chromosomes' na wala sio sijui kufikaaa .... kuwahi kufikaa blah blah blah!
 
Assalam alaykum,

Natanguliza shukran kwako kwa kujitolea ku ulizwa maswali na utatujibu kwa ufasaha.

swali langu ni kama lifuatalo,
1)ningependa kujua mpaka kati ya nchi ya zanzibar na tanganyika ki jographia?


Swali zuri sana hili, ni dogo lakini ni mjadala unaoweza kuwa mrefu kihistoria na kijiografia, kama sikosei.

Tusubiri wajuzi kwani nielewavyo Zanzibar ilikuwa ni dola kubwa kihistoria ambao utawala wake ulifika hadi sehemu sehemu za Somalia kwa Kaskazini na hadi Oman kwa Kaskazini Mashariki na hadi sehemu sehemu za Mozambique kwa Kusini Mashariki na hadi sehemu sehemu za Congo kwa Magharibi.

Baada ya Mkutano wa Berlin, "Berlin Conference" au uliojulikana pia kama "Congo Conference" wa mwaka 1884-85 uliohitimisha Wauropa kugawana mapande ya Afrika na kuweka mipaka wapendavyo, nini kilitokea baada ya hapo kuhusu dola ya Zanzibar na mipaka yake? Iliishia hapo tu au na wengine wakaja kuigawa tena?

Siku za karibuni niliwahi kusoma pahala kuwa mipaka ya mwisho ya Zanzibar imeishia maili 10 (kilomita kama 16) ndani ya Tanganyika, kwa mtazamo huo na kama haijarekebishwa kwa makubaliano, kuna uwezekano kuwa hata baadhi ya maeneo ya Dar., hususan katikati ya jiji kuwa ni Zanzibar?

Tunaomba wajuzi wapitie hapa kutowa darsa kuhusu hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…