Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Nilipomaliza masomo yangu sikuwa na mpango wowote wa kuja kufanya kazi Tanzania kwani nilikuwa tayari nnaishi Canada kwa miaka mingi kabla na baada.

Mimi sikuolewa, tumeoana na mume wangu.

Sijawahi kutokufanya kazi toka tuoane na mume wangu mpaka nilipostaafu kazi za kuajiriwa labda breaks za hapa na pale za maternity na kuhama nchi, kazi za mume wangu zilimfanya ahamishwe mara kwa mara nchi nyingi duniani.

Nnaona hapo kwenye kuolewa na kutokufanya kazi umewa single out "wanawake wa Kiarabu" pekee. Binafsi nnawajuwa wengi wasio Waarabu ambao hawafanyi kazi baada ya kuolewa. Na kila niwaonapo nnatamani sana nami ingekuwa hivyo, kuwapa family yangu 100% ya attention yangu. AlhamduliLlah haikuwa hivyo lakini sasa najaribu kulipiza kwa wajukuu.

Kuhusu Bi Samia Suluhu ntakujibu baadae.
Shukran, nasubiri la Samia

Sent from my GT-S7580 using JamiiForums mobile app
 
endeleen kufundishana judo na karate mdhan kuwa kuna div one za judo
Unachokisoma unakielewa? Maana mwenzangu ukiniuliza nnakujibu lakini wewe nikikuuliza hutaki kunijibu na unaleta mengine.

Rudia, nimekuuliza swali, nnaomba lijibu kabla hujaniuliza lako. Ndiyo raha ya mjadala.
 
Nnaogopa kuvunja sheria za nchi.

Nimeshawahi kuruka urefu wa zaidi ya meters 100 (kama sikosei ni 111) kwa kutumia kamba maalum (bungee jumping ) katika daraja la reli la Victoria, mto Zambezi mpakani mwa Zambia na Zimbabwe.

Sitosahau maisha yangu na niliapa sitorudia tena.

Nimependa hilo jibu... kumbe ni jasiri hivyo...itabidi nikutafute unisimulie mengi. Unaweza kuwa biography moja matata sana ya kutia moyo
 
Naam, ni huyohuyo mmoja.

Unaweza kumsoma zaidi kwenye Qur'an kujihakikishia: Quran Index - Jesus
Hapa umepotosha ni watu wawili tofauti. Yesu wa kwenye biblia kama biblia ilivyoandikwa alizaliwa kwenye holi la ng'ombe. Na issa bin mariam alizaliwa chini ya mtende. Pitia Biblia na Quran utaona. Kama ulivyotangulia kusema kwenye huu uzi ni vizuri ukauongelea uislamu unaoujua vizuri kuliko kuongelea ukristo usioufahamu.
 
Vigezo vya kuoana kwetu ni:

-Kwa mali zao
- kwa uzuri wao
- kwa nasaba zao
- kwa dini zao

Jee, unakidhi vigezo hivyo ?
Na mtume akaweka msisitizo wa hili la dini
Kwani ukioana na mwanamke kwa uzuri wake inaweza kuwa fimbo ya kukupigia au kwa ajili ya mali zake inaweza kuwa inampa kibri lakini kama ni mchamungu hilo halitawafika ndio maana ikasisitizwa dini.Fadhfalu fii dhati dini.
 
Hapa umepotosha ni watu wawili tofauti. Yesu wa kwenye biblia kama biblia ilivyoandikwa alizaliwa kwenye holi la ng'ombe. Na issa bin mariam alizaliwa chini ya mtende. Pitia Biblia na Quran utaona. Kama ulivyotangulia kusema kwenye huu uzi ni vizuri ukauongelea uislamu unaoujua vizuri kuliko kuongelea ukristo usioufahamu.


Jiulize, katika lugha aliyokuwa anaongea mama'ke Yesu kuna herufi "J"?

Anapowekwa ng'ombe hapawezi kuwa na mtende? Fikiri.

Pitia hapa: Jesus' name is Eesa. See detailed proofs from Aramaic, Hebrew and Arabic.
 
FaizaFoxy naomba unipatie majibu mujarab ya maswali haya:

- Uligraduate 1982, Bsc in electronic engineering, specialised in Telecommunications.

Naamini kwa wakati huo kulikuwa na wasomi wachache sana wa course hiyo hapa nchini.

JE: uliwahi kufikiria kuanzisha Firm yako au kuisaidia Tanzania kwa elimu yako kwa namna yoyote?

Au ulipoolewa ukaamriwa na mumeo utulie ndani na kumpikia pamoja na kumtunzia watoto kama wanawake wengi wa kiarabu wanavyoishi baada ya ndoa?

JE, Unazungumziaje uongozi wa Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania?

Huoni kama kwa Elimu, hekima yake na huruma angefaaa kabisa pia kuwa Rais wa URT?

Je huyo Mheshimiwa ameolewa? Unaweza kutuwekea picha ya Mumewe (I also understand about privacy but she is an icon)


Sent from my GT-S7580 using JamiiForums mobile app

Kuhusu "uongozi wa Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania?". Kwanza napenda uelewe, ni fahari kubwa kwa kila mwanamke wa Kitanzania na Bi Samia Suluhu amekuwa ni chachu ya wanawake kujiamini, si kwa Tanzania tu, bali hata nje ya mipaka yetu. Bi Samia ni mfano wa kuigwa.

Uongozi na umahiri wake nilianza kuushuhudia nilipomuona akiongoza bunge. Alikuwa anavutia jinsi anavyoliongoza bunge kwa umakini na ueledi wa hali ya juu, utafikiri aliumbiwa kuwepo pale kwenye kiti cha spika, nilikuwa nnajiuliza "kwanini huyu Bi Samia asiwe ndiye Spika wetu". Lakini ni mipango ya Allah.

Naam, kuwa Makamu wa Rais pia ni Rais. Title ya Urais ipo hapo tena kikatiba, kilichoongezeka ni "Makamu" tu.

Soma hapa kuhusu wasifu wa Bi Samia: Wasifu wa makamu wa rais wa Tanzania Samia Hassan - BBC Swahili
 
Isa alifufuka baada siku ya tatu?


Hakufa atafufukaje? Jisomee:

Biblia inasema hivi,

"Yesu alipokuwa akiishi duniani, alitoa dua na maombi kwa kilio kikuu na machozi kwa Mungu ambaye angeweza kumwokoa na kumtoa katika kifo, naye Mungu alimsikia kwa sababu alikuwa mnyenyekevu na mtiifu" (Waebrania 5:7)

Bible inatuambia kila aliyetundikwa msalabani amelaaniwa na mungu.
Katika kumbukumbu la Torati 21:23, Mungu anamwambia Musa kwamba mtu " aliyetundikwa katika mti amelaaniwa na Mungu".

MSIKILIZENI MUNGU.
Katika kumbukumbu la taurati 24:16, anasema nini:"mababa wasiuwawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya dhambi za baba zao.KILA MTU AUWAWE KWA DHAMBI ZAKE MWENYEWE"

Biblia pia inasema:

Numbers 23:19"God is not a man, so He does not lie. He is not human, so He does not change His mind. Has He ever spoken and failed to act? Has He ever promised and not carried it through?"

Quran tukufu inasema hivi,"Na kwa kauli yao kuwa: ‘Tumemuua Yesu mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu’. Hakika ni kuwa hawakumuua wala hawakumsulubu, lakini walishabihishiwa kwao. Wale wanaotofautiana katika hilo wako katika shaka wala hawana ilimu ya uhakika kuhusu hilo, wanafuata tu dhana. Hakika ni kuwa hawakumuua".
"Bali Mwenyezi Mungu Alimnyanyua Kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima". [An-Nisaa: 157-158]

Soma zaidi: Wakristo Njooni Kwa Mungu: Yesu hakusulubiwa, Mwenyezi Mungu alimwokoa.
 
Kuhusu "uongozi wa Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania?". Kwanza naoenda uelewe ni fahari kubwa kwa kila mwanamke wa Kitanzania na Bi Samia Suluhu amekuwa ni chachu ya wanawake kujiamini, si kwa Tanzania tu, bali hata nje ya mipaka yetu. Bi Samia ni mfano wa kuigwa.

Uongozi na umahiri wake nilianza kuushuhudia nilipomuona akiongoza bunge. Alikuwa anavutia jinsi anavyoliongoza bunge kwa umakini na ueledi wa hali ya juu, utafikiri aliumbiwa kuwepo pale kwenye kiti cha spika, nilikuwa nnajiuliza "kwanini huyu Bi Samia asiwe ndiye Spika wetu". Lakini ni mipango ya Allah.

Naam, kuwa Makamu wa Rais pia ni Rais. Title ya Urais ipo hapo tena kikatiba kilichoongezeka ni Makamu tu.

Soma hapa kuhusu wasifu wa Bi Samia: Wasifu wa makamu wa rais wa Tanzania Samia Hassan - BBC Swahili
Sio wewe tu ila Watanzania waume kwa wake tunamkubali sana kwani ni talented.

Hiyo ndiyo sababu ya kukuuliza swali hilo.

Mumewe (kama yupo) atakuwa anajivunia sana aicee.
 
Back
Top Bottom