Kocha ana UEFA Tano, utasemaje si kocha!, ni kocha Bora sana carlo...mpira ni matokeo, matokeo ni zao la mbinu, walioanza kumshuhudia Carlo toka akiwa Milan watathibitisha hili, nadhani ni kocha pekee aliyeweza kwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali ya soka hasa utendaji, mifumo nk.
Bahati zipo katika maisha , wachezaji wa madrid wenyewe wanakubali city ni timu yenye uwezo kuliko wao hivyo ilibidi wasifunguke ili wapate matokeo ya kufuzu nani bora hapo kati ya kocha wa city na wa madrid?
Binafsi nimeishuhudia MILAN ya CARLO ilikuwa nzuri mno Kakà akiwa mchezaji wa kutegemewa mbele kabisa akiwepo Philpo Inzaghi ile ndo timu ambayo ilinifanya nikubali Carlo ni kocha mkubwa.
Lakini tukisema ni bora sana tunakosea kiasi maana Carlo alikaa miaka 7 bila UEFA na zote kazipatia Madrid hizo 3 .
Wana upepo kama club kubeba taji hilo tu ndiyo maana Zidane katoka Castila kaja kabeba mara 3 yaani fikiria kwamba leo ukimpima Zidane kwa mataji ya UEFA analingana na Guardiola wakati kwenye football hana hata misimu minne ya kufundisha timu so naona kismati tu cha UEFA
KWANGU NI KOCHA MZURI ILA KUNA WATU WANA UBORA KULIKO YEYE KWA MTAZAMO WANGU
Carlo jana anatwaa taji la 28 Guardiola ana mataji 39 ikumbukwe wakati Guardiola anacheza mpira Carlo alikuwa kocha tayari , hii inamaanisha kuwa overall Kocha bora zaidi hadi sasa kwangu ni Guardiola ambaye kabakiza mataji 10 tu kumfikia Ferguson na for sure Guardiola ndiye kocha atakayekuja kuwa kocha mwenye mataji mengi zaidi katika historia ya soka miaka mitano ijayo
Kuna wapuuzi watakuja kusema kuwa hana tactics nzuri, wakati ameshamng'oa Bwna wao Guardiola mara 3 kwenye Champion League huku Pep akiishia kupigwa na butwaa.