Hivi ndo kusema mtiti wa 2011/12 Bayern Munich Vs Chelsea mmeusahau? Au ni hasira zenu na chuki tu dhidi ya Chelsea?[emoji12]
Ngoma imeenda hadi 120 kwa header la kiroho mbaya lililotandikwa na mmatumbi, Robben ananoa penalti ndani ya extra time, watu wanahema vya hatari, game inaisha kwa mbinde la matuta, wanaume wamepambana hadi mwisho ndo bingwa anapatikana!
Mnatuletea habari za game ambazo mtu anakufa 4-1! Fainali unapigwa mabao manne? Imekuwa rede? Fainali tamu mchezee kwenye 1-0, 2-1, 3-2 mwisho, zaidi ya hapo ni NBA.
Mada yenyewe inasema within 10yrs, mnafosi kwenda hadi 1990's huko ili tu msiisifu hii burudani[emoji16]
Semeni kiliumana!!!!