Fainali Uzeeni!....

wazee husema ujana maji ya moto

na wataalamu wanasema,ukitaka kuishi vizuri,
yatazame maisha yako kuanzia mwishoni kuja mwanzoni...

weka picha siku unayokufa,nini umeacha,nani atakulilia?
halafu rudi taratiibu mpaka leo ulipo

...na ulichotanguliza pia,...maana tuendako giza! Tunasikia tu kuna moto...!
Anyway, nahisi sie wabantu tulio wengi hasa huku kusini mwa jangwa la sahara
tuna ulemavu wa kutokuwa na upeo wa kuona mbali na kujipangia maisha yetu.

Kabla hamjaanza kunitwanga 'mawe,' ...jiulize umeupangilia vipi muda wako kuanzia leo mpaka
Ijumaa ijayo? ...au ndio mmemuachia Mungu? LOL!
 

mkuu hatukupigi mawe
but siri nyingine ya maisha ya furaha ni kutoyapaanga saana
acha nature pia ifuate mkondo

ndo maana watu wasio na elimu na kipato cha chini huwa na furaha zaidi
kuliko matajiri na maprofesa....

kumbuka tulivyokuwa watoto,
kitu kama pilau kinakupa furaha ya wiki nzima lol
 

hha ha ha!...hapo kwenye sana ndipo tunapotofautiana baina ya mtu na mtu.
Kuna wanaopanga 'kuonana jumapili,'
na kuna wanaopanga 'kuonana jumapili mchana.'
Hao wawili wanatofautiana na wanaopanga 'kuonana jumapili saa nane nanusu mchana.'

Kule unyamwezini, kipindi cha kulima kinategemeana na msimu wa kiangazi na masika, au sio?
Wale wakulima stadi, wana mahesabu hata miezi gani waanze kutayarisha mashamba, wakati gani wapande mbegu
wakati gani wa mbolea, palizi mpaka mavuno. Wanajua kuna majanga kama Nzige, kiangazi kikali, magugu, nk...lakini wanalima hivyo hivyo, au sio? Maisha ndivyo yalivyo.

...wewe unavuta kumbukumbu za pilau ya utotoni, mwenzio hapa napiga hesabu
ya pilau ya Eid mwaka huu nikaivizie wapi. Yote maisha.
 
Mi naona tulifunge tu hili sredi kwakuwa halina kuchakachua wala maofu topiki..........Hii inaashiria watu wanaogopa sana uzee.

Kwangu mimi uzee ni kama nchi ya "kusadikika"..... Uzee ni maandalizi ya kufa, ni kulipigia kaburi hodi. Of which kila mtu lazima mauti yamkute. Mie hapa naamini katika "hapa na karibu na hapa" zaidi kuliko "mbali kule". Maadam sijampigia Mungu simu anihakikishie ntakufa lini, nimedhamiria kujitosheleza kwa sasa zaidi badala ya kufikiria kusikokuwa na uhakika.
Leo mwanangu anakula nini na kesho kuna cha kumpa?
Leo mke wangu ntampa nini ntamfurahisha na nini na kesho je itakuwaje?
Leo naishi wapi navaa nini najitoshelezaje, na je kesho napo itakuwaje
Sasa biashara ya keshokutwa mtondo na mtondogoo inategemea kesho imekuwaje siyo? Kama kesho itakuwa poa, eventually mipango ya mtondo na mtondogoo itaendelea kutaradidi..... Ila sasa kama hata hiyo kesho hakieleweki itakuwaje uanze kupanga ya mtondogoo? Si waweza kufa kesho?

Ndo maana nlimuuliza mbu uzee anaozungumzia hapa ni umri gani hasa?
Kwa mtu mwenye miaka 20 atahisi uzee ni miaka 50. Na wa miaka hamsini anaona uzee ni miaka 70 huko..... Sijui kama naeleweka lakini kwangu mie kwa kijana wa miaka 22 kuanza kupanga mikakati ya namna atakayoishi baada ya miaka 65+(2) ni kutojitendea haki na kujizeesha kabla ya muda.... Wa miaka 22 anapaswa kufikiria maisha yatakuwaje atakapotimiza lets say 40. Ntakuwa nimeoa? na watoto? Ntawamudu? Ntakuwa na kagari kangu? je ka kiwanja au kakibanda?

Tuacheni sisi wenye miaka 60 tuwaze namna tutakavyoishi tukifikisha 70+...Hatuna cha kupoteza tena na muda ndo ushatamalaki....

Ushauri wa babu ODM ni huu:
Vijana wadogo fikirieni na kuwaza maisha yenu yatakavyokuwa mtakapofikisha umri wa makamo..... say 41+
Watu wa makamo fikirieni mlipokosea kwa kuyakosa yale mliyoyawaza kuwa mgekuwa nayo katika umri huu.... Bado hamjachelewa....pambaneni.... Maisha haya ya 41+ ndo kioo cha hali halisi utakayokuwa nayo utakapoingia kwenye uzee (60+)

Ukishaingia kwenye umri wetu huu ...60+ ndo muda sasa wa kuyafurahia/kusononeka kwa kuyafikia/kushindwa kuyafikia yale malengo ambayo ulipaswa kuyawazia na kuyafanyia kazi ukiwa na 41+.

Otherwise......karibuni kitandani huku, babu nimepumzika.
Samahani kwa ambao hawajanielewa, babu na ungwini wapi na wapi bana?
 
Uzee ni noma sana, na hasa kama hukukumbuka kujiwekea hazina yako....wako wengi tunawaona wanaadhirika mtaania tu, wamebaki kulalamikia watoto wao oooo mmetutupa, hamtutunzi, sababu walisahau kujiwekea akiba uzeeni, thanx mbu umefanya jambo la busara kutukumbushia hili
 
[TABLE="width: 110"]
[TR]
[TD="width: 55"][/TD]
[TD="width: 55"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: Ten, colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="width: 690"]
[TR]
[TD="width: 50, align: left"] [/TD]
[TD="width: 600"]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

OLD AGE?
What old age?
Enjoy Life Bwana before it is too late.
Kata mti panda mti, mwaga nyuki!
 
...lol, no wonder sisi kama taifa tunakaribia miaka 50 baada ya uhuru na matatizo yanatuzidi. Umeme tabu, maji safi tabu, magonjwa, umasikini, ujinga, njaa, ufisadi, mismanagement ya viwanda na mashirika ya umma, mmomonyoko wa maadili, yaani kila kitu tabu, tabu, tabu...

Kama umri, taifa limepoteza dira. Taifa bila watu ni pori tu au kisiwa. Kama wenyewe hatuna discipline ya kujipangia maisha, lawama za nini kwa hao wanaoendesha serikali? Tatizo sugu hili, tatizo la taifa, aka "ujinga wa mwafrika"..
 
Uzee ndio fainali...

Kujiandaa ni muhimu ili usijeaibika baadae.

Ila ukweli ni kwamba waAfrika wengi bado tunaamini kwamba ‘jukumu la kumlea MTOTO ni la WAZAZI‘ na ‘jukumu la kulea WAZAZI kipindi cha uzee ni la WATOTO.‘ Ndio maana wazee wengi (achana na mafisadi) wanafanya kazi sana na kuhangaika kuwasomesha na kuwaweka watoto wao kwenye mstari wakijui kwamba mahangaiko yote hayo yatakuja kulipa hapo baadae atakapokua hana nguvu tena ya kuhangaika na mwanae atakapokua katika nafasi nzuri kumsaidia mzazi.

Huko magharibi ambapo akiba ni kitu muhimu sana hawana hii nidhamu ya mtoto kumlea mzee wake sana kama ilivyozoeleka kwetu.Wengi wao wakiona mama/baba hawawezi kufanya mambo yao wenyewe tena wanaenda kuwatupa kwenye nyumba za wazee na kuwatembelea mara moja/mbili kwa mwezi basi.

Hamna ubaya wowote wenye kujiwekea akiba....ila tujaribu na sisi tusije tukaishia kuwa kama hawa ndugu zetu ambao wanawakimbia wazee wao kipindi ambacho wanawahitaji zaidi maishani mwao.Kama hawakukupeleka wewe kwenye nyumba ya “watoto“ wakati huishi usumbufu usichukulie uzee wao kama usumbufu kwao.
 
Mbu hilo neno limeniingia kwenye damu ahsante sana.manake usipo jipanga sasa utajikuta unasema peke yako.
 
Reactions: Mbu

Mkuu hapo umenena..kama tunashindwa kujipangia discipline ya maisha sisi wenyewe tunategemea nani atusaidie. Kuna ule msemo kabla ujaona ujiti mdogo kwenye mboni ya jicho la jirani toa kwanza boliti kwenye jicho lako. Kila siku sredi nyingi ni watu tunaomba msaada kupooza na wala sio kutatua matatizo yetu.. wangapi tunaomba ushauri wa maisha ya baadaye? Mimi nadhani jinsi tunavyochelewa ku-settle kiakili sasa basi ule muda wa kujipanga unakimbia na pumzi zinatuishia kwani uzee unakaribia.. Na kwa ajili ya panic hiyo tunalaumu watu wengine na serikali...

kuna vitu ni kweli siasa inachukua mkondo wake na lawama zake..lakini kuna vitu vya chumbani serikali haiwajibiki...Kwani kupanda mwembe ili baadaye wajukuu wako wale maembe na wewe upumzike kivulini..tunasubiri tuambiwe..

Kuna suala la kufa..lazima tufe..kwa ajali, maradhi, etc.. kutayalisha maisha ya baadaye ya watoto kama ikitokea mmoja kati ya mume au mke akifa ni uchuro au ujinga? kuna jamaa alianzisha topic kama hiyo wengi wakamwambia awahi Angaza kupima..Jamani,,nani asiyejua Nature ya binadamu... Mababu zangu hawakuacha urithi..wazazi wangu wakakosana.. Wazazi wangu hawakuacha urithi..ndugu sasa tumeanza kutosalimiana... Je hata mimi nashindwa kujua ni fanye nini ili watoto wangu waepuke na balaa hili? wangapi tuko kwenye majaribu haya? ..Je tukikaa kimya tutakuwa welevu kuwa kuogopa uzee; kifo na uchuro au tutakuwa wajinga?
 
Reactions: Mbu
Kujiandaa ni muhimu ili usijeaibika baadae.

Ila ukweli ni kwamba waAfrika wengi bado tunaamini kwamba ‘jukumu la kumlea MTOTO ni la WAZAZI‘ na ‘jukumu la kulea WAZAZI kipindi cha uzee ni la WATOTO.

Ni kweli..tumshukuru Mungu kwa hili..na pia tuwape pole kwa wale asilimia chache ambao wazazi wao waliwekeza akiba zao kwa watoto halafu watoto wakaishia kuvuta unga na wazee kucheza pata potea.. Lakini kwa Afrika bado ni asilimia chache..


Ni kweli kabisa..ila labda wazee sasa tuamke na tuwe pia na option B..ili kama watoto wetu wataishia kwenye unga au kubadilika kwa kukumbatia tamaduni za uko magharibi ulaya kwa kutupeleka kijijini kwa wazee wenzetu tupate mtaji wa kufungua kilabu ya pombe za kienyeji au kuuza kahawa.
 

Babu hapa uko sawa kabisa, haya mambo ni ya kuyazingatia sana leo waishije na kesho yapitaje............but ni stepping stone ya future hii.kwa sababu unaishi leo ukifikiria ya kesho, ikifika kesho utafikiria ya kesho kutwa maisha yanaendelea lakini kwa kuwa huna miadi na MUNGU lini anakuhitaji.huna budi kuwaza yajayo what if ukianguka ghafla leo..umejiandaandaaje? unamwachaje Mama Matesha na Matesha? Kuna akiba kiasi gani, watajisitiri wapi?? na kwa namna gani?? Uzee ndio huu.unapoifikiria kesho ni kufikiria uzee wako indirectly!! HONGERA kwa hilo.


hicho kitanda chako ni futi ngapi Babu? Tukija wajukuu wote tutatosha?
 

Gaga aksante umenikumbusha Babake rafiki yangu he used to tell his kids..hii mali mnayoiona hapa ni yangu na mama yenu.yaani nyie hakuna wta kijiko chenu hapa.and it helped, my friend (Ni mdada akakua na notion hiyo sasa hivi she is one of the well recognized "watu wa Mahesabu" in South Afrika.

Kijiandaa ni muhimu kwa kweli
 
Reactions: Mbu
Mkuu i salute!!!!!!!! this is good message congratulation!! keep it up on posting good message
 
Reactions: Mbu
Wifi ungefafanua kidogo hapa ingeleta utamu!!
Kaka hajambo?

sote hatujambo kabisa mpendwa, tunamshukuru Mungu.

hoja yangu ni kwamba kufunga ndoa na mtu sio mwisho wa kujenga mahusiano. tuna kazi ya kuendelea kujenga mahusiano na watu wote wakiwemo wenzi wetu siku zote hata mwisho wa maisha yetu. unaweza kuchagua mke/mume ambaye wa maoni ya baadhi ataonekana si match wako lakini kadiri mnavyoishi, mnaweza kuzoeana taratibu na kufahamiana zaidi na hivyo hofu ya kukimbiwa uzeeni au kuwa mpweke kwa namna nyingine haina nguvu.

kwangu mimi, fainali ni LEO! iwe ujanani au uzeeni. uzeeni kuna maisha kama yalivyo ujanani ama utotoni. kuna vijana wengi wapweke kama ilivyo kwamba kuna wazee wengi vilevile wapweke. vilevile kuna hata watoto amabo ni wapweke pia. kwa hiyo, tusipomtegemea Mungu, kila siku tutakuwa tunajiandaa na maisha ambayo hatutakuja kuyafikia na ambayo Mungu kwa rehema zake tayari kishatuandalia na daima hutuwazia mambo mema na makubwa akitupa tumaini katika siku zetu za mwisho.

kwa majaliwa yetu wanadamu ni ngumu sana kufahamu kwa hakika yatakayotokea hata kesho tu, sembuse huko uzeeni? tunaweza kuwa makini kuchagua wenzi wa maisha, tukaridhika na assessment zetu za kibinadam tukiongozwa na macho na akili za nyama laini mwisho wake hatuwezi kuujua lolote na kwa kweli hatuwezi kitu!

nakubaliana na wanaosema akiba itakayotufaa uzeeni na huduma kwa watoto wetu ni muhmu ili kuwajengea uwezo wa kuyamudu maisha, lakini zaidi sana kumtumaini Mungu ndio muhimu zaidi kwani yeye ajua tunachohitaji hata kabla hatujaomba. kama tunataka kuziona siku njema za uzeeni, basi tuzuie ndimi zetu zisinene hila na mioyo yetu isitawaliwe na tamaa. huku tumkumiomba Mungu bila kukoma tukiamini kuwa sisi tu watumishi tu na kondoo wa malisho yake.

tukifaya hayo tutashukuru daima kwa kila jambo kwa maana yote (mazuri kwa mabaya, matamu kwa machungu nk) ni mapenzi ya Mungu na tukisimama kwa imani katika yote hata mwisho, ndipo tutakapopata kushinda na zaidi ya kushinda kwake yeye atutiaye nguvu na Mungu atajipatia utukufu

nawatakieni wote baaka za Bwana

Jina la Bwana libarikiwe
 

...Tupo msitari mmoja kiongozi. Mpaka hapo, tunaongea lugha moja...
Pse note hizo nilizo highlight red,....hasa hapo kwenye
...60+ ndo muda sasa wa kuyafurahia/kusononeka kwa kuyafikia/kushindwa kuyafikia yale malengo ambayo ulipaswa kuyawazia na kuyafanyia kazi ukiwa na 41+.


Ms Judith,...tumtamainie mungu nasi tujishughulishe. Kushinda kutwa kucha kwenye nyumba za ibada i.e kanisani, msikitini... hakutatusaidia lolote, hata Mungu hapendi... ndio maana hata Ibada zina muda wake maalumu ili muda mwingine tuutumie kwenye mipangilio mingine ya maisha, ikiwamo kujenga familia zetu.
 
Mbu post yako imenipa mawazo mengi sana,nipo late 20s naamini sijachelewa kufanyia kazi unayosema.
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…