sote hatujambo kabisa mpendwa, tunamshukuru Mungu.
hoja yangu ni kwamba kufunga ndoa na mtu sio mwisho wa kujenga mahusiano. tuna kazi ya kuendelea kujenga mahusiano na watu wote wakiwemo wenzi wetu siku zote hata mwisho wa maisha yetu. unaweza kuchagua mke/mume ambaye wa maoni ya baadhi ataonekana si match wako lakini kadiri mnavyoishi, mnaweza kuzoeana taratibu na kufahamiana zaidi na hivyo hofu ya kukimbiwa uzeeni au kuwa mpweke kwa namna nyingine haina nguvu.
kwangu mimi, fainali ni LEO! iwe ujanani au uzeeni. uzeeni kuna maisha kama yalivyo ujanani ama utotoni. kuna vijana wengi wapweke kama ilivyo kwamba kuna wazee wengi vilevile wapweke. vilevile kuna hata watoto amabo ni wapweke pia. kwa hiyo, tusipomtegemea Mungu, kila siku tutakuwa tunajiandaa na maisha ambayo hatutakuja kuyafikia na ambayo Mungu kwa rehema zake tayari kishatuandalia na daima hutuwazia mambo mema na makubwa akitupa tumaini katika siku zetu za mwisho.
kwa majaliwa yetu wanadamu ni ngumu sana kufahamu kwa hakika yatakayotokea hata kesho tu, sembuse huko uzeeni? tunaweza kuwa makini kuchagua wenzi wa maisha, tukaridhika na assessment zetu za kibinadam tukiongozwa na macho na akili za nyama laini mwisho wake hatuwezi kuujua lolote na kwa kweli hatuwezi kitu!
nakubaliana na wanaosema akiba itakayotufaa uzeeni na huduma kwa watoto wetu ni muhmu ili kuwajengea uwezo wa kuyamudu maisha, lakini zaidi sana kumtumaini Mungu ndio muhimu zaidi kwani yeye ajua tunachohitaji hata kabla hatujaomba. kama tunataka kuziona siku njema za uzeeni, basi tuzuie ndimi zetu zisinene hila na mioyo yetu isitawaliwe na tamaa. huku tumkumiomba Mungu bila kukoma tukiamini kuwa sisi tu watumishi tu na kondoo wa malisho yake.
tukifaya hayo tutashukuru daima kwa kila jambo kwa maana yote (mazuri kwa mabaya, matamu kwa machungu nk) ni mapenzi ya Mungu na tukisimama kwa imani katika yote hata mwisho, ndipo tutakapopata kushinda na zaidi ya kushinda kwake yeye atutiaye nguvu na Mungu atajipatia utukufu
nawatakieni wote baaka za Bwana
Jina la Bwana libarikiwe