Nimeikubali sana hii.. Naamini moja ya akiba ya uzeeni ambayo ni kubwa kabisa ni jinsi gani ya kupigana na upweke..Hata kama ukiwa na pesa kiasi gani lakini ukiwa mpweke ni kazi bure .. Kama tuna bahati ya kuwa wawili basi inabidi tulee mahusiano yetu..yaani wawili ni wawili hata maandiko yamesema hivyo...
Ecclesiastes (Mhubiri) 4:9-12 Two are better than one, If either of them falls down, one can help the other up. But pity anyone who falls and has no one to help them up. Also, if two lie down together, they will keep warm. But how can one keep warm alone?
Bravo! Kama mtihani nakupa 110% ..yaani umetuchoma mkuki moyoni... Thanks kwa hilo
Ni kweli kabisaaaa!..Tukimweka Mungu mbele daima ..basi tutaona upendo wa kweli.. Tutapenda wake zetu, wake watapenda waume zao, tutapenda watoto na familia zetu, tutapenda majirani zetu na marafiki.. Hatutakuwa wapweke tena..Ni upendo..Love, Love, Love..
"And now these three remain: faith, hope and love. But the greatest of these is love." 1 Corinthians 13:13
ndugu yangu mpendwa Tulizo,
nimekukubali sana na kwa kweli wewe ni TULIZO!! hata pale ambapo sikunyoosha maneno vizuri, umeyanyoosha na KUYATULIZA. ubarikiwe sana mpendwa.
fainali ni LEO!! ya nini kuishi kwa kujidanganya eti uzeeni ndio fainali, wakati Mungu anatutaka tuamue na kuchukua hatua LEO!, wake/waume zetu wanatutaka tuwapende LEO, wanatatutaka tuamue na kuchukua hatua LEO, familia zetu zinatutaka tuishi kwa furaha LEO, jamii yetu inatutarajia tuchangie maendeleo yake LEO, taifa na dunia kwa ujumla vinattarajia kuwajibila LEO!! hata wahenga walisema biashara ni asubuhi ya "LEO" (msisitizo ni wangu) na jioni ni mahesabu!
uzee ni nadharia kama ulivyo ujana na utoto (quote my words please)!! kitu halisi ni wewe, mimi, yule, nk. hizo personalities za "uzeeni" ni nadharia tu lakini katika uhalisia wa maisha hakuna kitu kama hicho!! misemo kuwa ng'ombe "hazeeki maini" na mingine ya aina hiyo inathibitisha kuwa, uzee, ujana na hata utoto ni ARBITRARY!! na hata kuna watu humu wameuliza "uzee unaanzia miaka mingapi? na hata mwenye thread hakuweza kusema kwa yakini umri ambapo uzee huanza!!
hali halisi inategemeana na karama ya Mungu. ibrahimu na mkewe sara walizaa uzeeni wakapata furaha na kuziona siku zao njema. sara alikuwa akijicheka alipojiona ana mimba katika umri ule, yaani hakuamini kuwa naye kawa ka-teenager fulani hivi "kazee", kuna raha kushinda raha itokanayo na hisia kama hizi??
ndugu zangu tusijidanganye, kujihangaisha na mipango, mipango, mipango, wakati maisha yetu yanatutaka tuishi LEO na Mungu wetu anatutaka tuishi LEO!! mipango ni nadharia tu. ndio maana wenye pension na wasio na pension wote wana maisha sawa!! hata wenye pension kubwa kama za ma-rais wastaafu, tena ambao hutunzwa na serikali hadi mwisho wa maisha yao, nao bado wanahangaikia maisha!!
nawaambieni wapendwa, tusipomtumainia Mungu, haya maisha tunayoishi yamejaa ubatili mtupu na kujilisha upepo. unapomcha Mungu ndipo unapopata maana halisi ya maisha na kuziona siku zako zilizo tamu na njema!!
ubarikiwe sana mpendwa Tulizo na wapendwa wote wana JF, nawatakia wote week end njema.
Glory to God!!