Fainali Uzeeni!....

Fainali Uzeeni!....

Jamani nisaidieni,uzee unaanzia miaka mingapi?

...utapoanza kuzeeka.

Babu hapa uko sawa kabisa, haya mambo ni ya kuyazingatia sana leo waishije na kesho yapitaje............but ni stepping stone ya future hii.kwa sababu unaishi leo ukifikiria ya kesho, ikifika kesho utafikiria ya kesho kutwa maisha yanaendelea lakini kwa kuwa huna miadi na MUNGU lini anakuhitaji.huna budi kuwaza yajayo what if ukianguka ghafla leo..umejiandaandaaje? unamwachaje Mama Matesha na Matesha? Kuna akiba kiasi gani, watajisitiri wapi?? na kwa namna gani?? Uzee ndio huu.unapoifikiria kesho ni kufikiria uzee wako indirectly!! HONGERA kwa hilo.

...Dah, Mwj1 wangu...hiyo "what if ukianguka leo...umejiandaa andaaje?" nayo inatubidi tuizingatie kwakweli.
Thanks.
 
hoja yangu ni kwamba kufunga ndoa na mtu sio mwisho wa kujenga mahusiano. tuna kazi ya kuendelea kujenga mahusiano na watu wote wakiwemo wenzi wetu siku zote hata mwisho wa maisha yetu.

Nimeikubali sana hii.. Naamini moja ya akiba ya uzeeni ambayo ni kubwa kabisa ni jinsi gani ya kupigana na upweke..Hata kama ukiwa na pesa kiasi gani lakini ukiwa mpweke ni kazi bure .. Kama tuna bahati ya kuwa wawili basi inabidi tulee mahusiano yetu..yaani wawili ni wawili hata maandiko yamesema hivyo...

Ecclesiastes (Mhubiri) 4:9-12 Two are better than one, If either of them falls down, one can help the other up. But pity anyone who falls and has no one to help them up. Also, if two lie down together, they will keep warm. But how can one keep warm alone?

kwangu mimi, fainali ni LEO!

Bravo! Kama mtihani nakupa 110% ..yaani umetuchoma mkuki moyoni... Thanks kwa hilo

...tusipomtegemea Mungu, kila siku tutakuwa tunajiandaa na maisha ambayo hatutakuja kuyafikia na ambayo Mungu kwa rehema zake tayari kishatuandalia na daima hutuwazia mambo mema na makubwa akitupa tumaini katika siku zetu za mwisho.

kwa majaliwa yetu wanadamu ni ngumu sana kufahamu kwa hakika yatakayotokea hata kesho tu, sembuse huko uzeeni? tunaweza kuwa makini kuchagua wenzi wa maisha, tukaridhika na assessment zetu za kibinadam tukiongozwa na macho na akili za nyama laini mwisho wake hatuwezi kuujua lolote na kwa kweli hatuwezi kitu!

Ni kweli kabisaaaa!..Tukimweka Mungu mbele daima ..basi tutaona upendo wa kweli.. Tutapenda wake zetu, wake watapenda waume zao, tutapenda watoto na familia zetu, tutapenda majirani zetu na marafiki.. Hatutakuwa wapweke tena..Ni upendo..Love, Love, Love..

"And now these three remain: faith, hope and love. But the greatest of these is love." 1 Corinthians 13:13
 
Mbu post yako imenipa mawazo mengi sana,nipo late 20s naamini sijachelewa kufanyia kazi unayosema.
Hali+ya+hewa.jpg
...Chauro mydear, nakuombea hayo mawazo yawe yenye changamoto, siyo msongo utaokufanya upoteze raha.
Ni wachache wetu tunaotumia muda mchache kusikiliza na kuuzingatia "utabiri wa hali ya hewa."
 
Nimeikubali sana hii.. Naamini moja ya akiba ya uzeeni ambayo ni kubwa kabisa ni jinsi gani ya kupigana na upweke..Hata kama ukiwa na pesa kiasi gani lakini ukiwa mpweke ni kazi bure .. Kama tuna bahati ya kuwa wawili basi inabidi tulee mahusiano yetu..yaani wawili ni wawili hata maandiko yamesema hivyo...

Ecclesiastes (Mhubiri) 4:9-12 Two are better than one, If either of them falls down, one can help the other up. But pity anyone who falls and has no one to help them up. Also, if two lie down together, they will keep warm. But how can one keep warm alone?

Bravo! Kama mtihani nakupa 110% ..yaani umetuchoma mkuki moyoni... Thanks kwa hilo

Ni kweli kabisaaaa!..Tukimweka Mungu mbele daima ..basi tutaona upendo wa kweli.. Tutapenda wake zetu, wake watapenda waume zao, tutapenda watoto na familia zetu, tutapenda majirani zetu na marafiki.. Hatutakuwa wapweke tena..Ni upendo..Love, Love, Love..

"And now these three remain: faith, hope and love. But the greatest of these is love." 1 Corinthians 13:13

ndugu yangu mpendwa Tulizo,

nimekukubali sana na kwa kweli wewe ni TULIZO!! hata pale ambapo sikunyoosha maneno vizuri, umeyanyoosha na KUYATULIZA. ubarikiwe sana mpendwa.

fainali ni LEO!! ya nini kuishi kwa kujidanganya eti uzeeni ndio fainali, wakati Mungu anatutaka tuamue na kuchukua hatua LEO!, wake/waume zetu wanatutaka tuwapende LEO, wanatatutaka tuamue na kuchukua hatua LEO, familia zetu zinatutaka tuishi kwa furaha LEO, jamii yetu inatutarajia tuchangie maendeleo yake LEO, taifa na dunia kwa ujumla vinattarajia kuwajibila LEO!! hata wahenga walisema biashara ni asubuhi ya "LEO" (msisitizo ni wangu) na jioni ni mahesabu!

uzee ni nadharia kama ulivyo ujana na utoto (quote my words please)!! kitu halisi ni wewe, mimi, yule, nk. hizo personalities za "uzeeni" ni nadharia tu lakini katika uhalisia wa maisha hakuna kitu kama hicho!! misemo kuwa ng'ombe "hazeeki maini" na mingine ya aina hiyo inathibitisha kuwa, uzee, ujana na hata utoto ni ARBITRARY!! na hata kuna watu humu wameuliza "uzee unaanzia miaka mingapi? na hata mwenye thread hakuweza kusema kwa yakini umri ambapo uzee huanza!!

hali halisi inategemeana na karama ya Mungu. ibrahimu na mkewe sara walizaa uzeeni wakapata furaha na kuziona siku zao njema. sara alikuwa akijicheka alipojiona ana mimba katika umri ule, yaani hakuamini kuwa naye kawa ka-teenager fulani hivi "kazee", kuna raha kushinda raha itokanayo na hisia kama hizi??

ndugu zangu tusijidanganye, kujihangaisha na mipango, mipango, mipango, wakati maisha yetu yanatutaka tuishi LEO na Mungu wetu anatutaka tuishi LEO!! mipango ni nadharia tu. ndio maana wenye pension na wasio na pension wote wana maisha sawa!! hata wenye pension kubwa kama za ma-rais wastaafu, tena ambao hutunzwa na serikali hadi mwisho wa maisha yao, nao bado wanahangaikia maisha!!

nawaambieni wapendwa, tusipomtumainia Mungu, haya maisha tunayoishi yamejaa ubatili mtupu na kujilisha upepo. unapomcha Mungu ndipo unapopata maana halisi ya maisha na kuziona siku zako zilizo tamu na njema!!

ubarikiwe sana mpendwa Tulizo na wapendwa wote wana JF, nawatakia wote week end njema.

Glory to God!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...kumbuka, pensheni yako haitokutosheleza kulipia;

1. kodi ya nyumba/chumba
2. ada ya shule kwa mwanao/wanao.

Ugumu wa maisha unaoupata sasa ni 'ishara' ya huko unakoelekea, na huenda yakazidi ugumu, upweke na ukiwa.

Wakati huo ushapoteza kazi, marafiki, na hata ndugu ulowainua kwa pesa zako za ujana. Wahenga walisema, ' mtumai cha ndugu...' Hala hala usijekimbiwa hata na wanao.

Jiwekee 'akiba'...jenga, nunua hisa kama unaamini, nunua pensheni, jiwekee bima ya afya, jipangie maisha...Muda unakuacha mkono.
Mbu- Ahsante kwa hii topic ambayo inatugusa sisi vijana. Wengi wetu tumejisahau kama uzee unakaribia kwa kadiri unavyolala na kuamka. Tunajiona bado tuna mda mwingi wa kutengeneza maisha bora huko uzeeni na hivyo kipato chetu cha sasa ni cha kutumbuwa kwa sasa na saving ya uzeeni ni baada ya miaka michache ijayo tutaifanya.

Nimeona tofauti kubwa sana kwa vijana wenzetu katika nchi zilizoendelea na sisi tulivyo katika suala zima la saving/investing. Siyo kuwa wao wanavipato vikubwa sana tofauti na vya kwetu bali ni tabia ya kujilimbikizia na kesho pia. Wanayajuwa masuala ya portifolio rebalancing practically siyo tu kusoma vitabuni na kujibia mitihani kama tunavyofanya wengi wetu. Wanaadabu katika matumizi siyo kama sisi tukifika bar tunataka kuzungusha counter nzima au pengine tukiwa nazo tunataka kufunga bar na tunasahau leo haitakuwa sawa na kesho. Starehe hazikwepeki lakini tunapaswa kuangalia hatima ya maisha yetu hapo mwili utakapopungua nguvu za kukimizana kma sasa. Pale ambapo utakuwa ni wewe na mkeo tu marafiki wamebaki wa kuhesabu.

Wengi wetu tunalalamika vipato vyetu havitoshi lakini starehe na vitu vya mpito tunavipa kipaumbele kikubwa. Vinatuchukulia kiasi kikubwa cha vipato vyetu na si vya lazima kihivyo kuwa tukivikosa au tukiishi maisha ya kawaida mambo hayataenda. Wengi wetu tunapenda vitu vya bei kubwa ili mradi tu tuonekane katika jamii inayotuzunguka tukiwa navyo. Hata kama si vya muhimu sana katika maisha yako au utendaji kazi wako wa kila siku
bali tunafuata mkumbo fulani anacho na mimi ngoja nikatafuta kama chake au cha bei kubwa zaidi. Hakiba ya kutosha hauna, nyumba unapanga, hata invesments hauna. Ni ulimbukeni!!!.

Vijana tufunguke macho, hizi pesa tunazopata kuna siku zitakoma kama hatujajipanga sawasawa. Tuwe na hurka ya kusave/ Invest kwa ajiri ya maisha ya leo na kesho pia. Stress za uzeeni ni mbaya zaidi ya hizi tunazopata ujanani. Kwa sasa tuna marafiki wengi hata kama tuna stress tunajichanganya baada ya mda zinaondoka. Tujitengenezee maisha mazuri kwa sasa na uzeeni. Na zaidi tumtangulize Mungu katika yote.

  • Thanks
Reactions: Mbu
Ms Judith,...tumtamainie mungu nasi tujishughulishe. Kushinda kutwa kucha kwenye nyumba za ibada i.e kanisani, msikitini... hakutatusaidia lolote, hata Mungu hapendi... ndio maana hata Ibada zina muda wake maalumu ili muda mwingine tuutumie kwenye mipangilio mingine ya maisha, ikiwamo kujenga familia zetu.

ndugu yangu mpendwa Mbu,

hapo kwenye bold umekimbia hoja kadhaa nilizozungumzia. nani kapendekeza tushindie makanisani/misikitini kutwa kucha?

kwa kweli hata ukishinda mbele ya laptop ukipanga na kupangua utakavyoishi uzeeni nako ni kazi bure!! hata ukitoa sehemu ya damu mwilini mwako uiuze ili kujiwekea akiba ya uzeeni hapa duniani nayo ni kazi bure. watu wengi huvuruga mipango yao kwa sabababu nyingi zikiwemo zile zisizotarajiwa. imagine leo una akiba ya 100m kwa ajili ya kuitumia uzeeni, lakini ukipata maradhi utagoma kuitumia kwa matibabu eti ukiusubiri "uzee" hujaona bado hapo haja ya kumtumaini Mungu?

ninachoongea ni kwamba tusijidanganye tukifikiri "we can control the future!!" na pia tusidangayane kuwa uzeeni tutakimbiwa na marafiki au kuwa ujanani ndio tuna marafiki wengi!! huo wote ni uongo mkubwa. hata leo tuna vijana wengi sana wapweke, wale wenye marafiki wamshukuru sana Mungu na sio wajishukuru wenyewe. hata leo vilevile tuna wazee wengi sana wenye marafiki wengi hata kushinda vijana wa leo, nao wamshukuru Mungu, na sio kujishukuru wao.

tujifunze kumtumaini Mungu na kumshukuru kwa kila jambo analotujaalia maishani. planning is just a theory na theories zote ni mawazo ya kibinadamu tu hata zingekuwa zimenyooka kiasi gani, zina limitations chungu mzima.

lets trust in the Lord wapendwa!

Glory to God!
 
...We cannot control the future Ms Judith, lakini hilo halituondoshei jukumu la ku "plan" for the future.
'Nahisi unanisoma haraka haraka' sana. Mbona ulikuwa muwazi tu kwenye topik ya "siku 30 nzito kwa maisha yangu?"
https://www.jamiiforums.com/mahusia...0-nzito-za-maisha-yangu-ooh-glory-to-god.html Mbona ulituwekea mpaka siku na tarehe, ewe Ms Judith?
"Breath in, Breath Out!"...

F.Y.I thread (Topik) zangu zinaongozana zikizingatiia ujumbe na umuhimu wa ku balance 'gurudumu la maisha.'

Asante, japo hata cha kuweka hakipo kwani hata kwa muda huu hakitoshi vile vile.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Aisee kumbe hili sredi bado linaendelea?

Kweli uzee noma!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Asante, japo hata cha kuweka hakipo kwani hata kwa muda huu hakitoshi vile vile.

...Achana na pesa,...endelea kuwekeza Imani, Mapenzi, Uaminifu, Ushirikiano etc kwa hao wanaokuzunguka.
 
Halafu kile kidude cha thanks kimeenda wapi bana?vingine vinahitaji mathanks yetu kwa Mbu.

Hali+ya+hewa.jpg
...Chauro mydear, nakuombea hayo mawazo yawe yenye changamoto, siyo msongo utaokufanya upoteze raha.
Ni wachache wetu tunaotumia muda mchache kusikiliza na kuuzingatia "utabiri wa hali ya hewa."
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kumekucha jamani, shime tukajiandalie pensheni zetu...fainali Uzeeni.

Tunavyowapiga vikumbo wastaafu wa Jumuiya ya Africa mashariki, na hata wengine kuwadhihaki, ina maana hatukumbuki ipo siku nasi twaweza angukia
kwenye mzunguko huo huo. Mwenye macho haambiwi ona, na mwenye masikio halazimishwi sikiliza.

What goes around comes around.... Usipojiwekea akiba ya uzeeni, ujue unachezea shilingi chooni.
Tujiandae! Ujana ni moshi...unafuka huoooo wenda zake!...kufumba na kufumbua utajikuta marafiki wanapungua
kwa rate ya mafungu ya 10%...na kujikuta mkiwa...

Je, umejiandalia nini uzeeni? Una japo kibanda cha kujistiri? au unabahatisha maisha wewe? wanao ni Insurance, lakini pia usiitegemee 100% ipo siku watakusaidia....Jiandaee...fainali uzeeni!

Old+Age+Sri+Lanka+Daily+Mirror210709.jpg

“Old age is like everything else. To make a success of it, you've got to start young.”

elderly-couple.jpg

“When marrying, ask yourself this question: Do you believe that you will be able to converse well with this person into your old age?
Everything else in marriage is transitory.”

...Maisha ya uzee ni ukiwa!...story zako hazitakuwa na mvuto tena. Twaona wazee wengi wa miaka ile wamepitwa na wakati. hawawezi hata kuwapigia hata hadithi wajukuu sababu ya hizi Big Brother, Egoli, etc... watoto wa kisasa hawadanganywi na hadithi za sungura na fisi...

anza sasa kujijengea mahusiano mazuri na mkeo uwe na mtu wa kujifariji nae miaka hiyo ya ukiwa, ....fainali uzeeni!

Kwani huko uzeeni tutafika? After all kuishi kwingi ni kwa vile mtu una matunzo mazuri, kama hayapo unakitoa soon after........ Why bother on earth!!!!!!!!!!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Miss Judith bana..... Unasemaje huweziicontrol future wakati kwa siku 29 za mwezi waenda kazini kuihangaikia kesho? Kwani future inaanzia lini?
 
Miss Judith bana..... Unasemaje huwezi icontrol future wakati kwa siku 29 za mwezi waenda kazini kuihangaikia kesho? Kwani future inaanzia lini?

Mwj1 nimegundua Wengi ukiwaambia fainali uzeeni wao wanachukulia ni FEDHA pekee,...
AFYA, FAMILIA, etc vyote hivyo wanaona havina maana...

Hii inanipa mtazamo mpana tunavyochukulia future sie wabantu. Ukimwambia mkulima
1/3 ajiwekee chakula, 1/3 auze, 1/3 ajiwekee akiba...anakwambia ya kesho muachie Mungu.
Kiangazi na njaa vikija, Mungu analaumiwa...

Nadhani haipo kwenye DNA (culture) yetu kujiwekea "akiba." Tatizo la kitaifa,
tuna madini, mito, watu, etc ...lakini miaka 50 baada ya uhuru bado ni masikini.
Tatizo letu sio wanasiasa, tatizo letu ni "mismanagement" from root level.
Acha tumshukuru Mungu tu.

-"It will generally be found that men who are constantly lamenting their ill luck are only reaping the consequences of their own neglect, mismanagement, and improvidence, or want of application."-

Mtavuna mlichopanda.
 
mi naona kuna haja ya kuwa na "common definition of terms" mwanzoni mwa kila thread ili kuepuka hii hali inaoendelea hapa,

ni maoni tu jamani, asanteni

Mungu awabariki
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Miss Judith bana..... Unasemaje huweziicontrol future wakati kwa siku 29 za mwezi waenda kazini kuihangaikia kesho? Kwani future inaanzia lini?

mpendwa,
1. wewe unaweza kujua yatakayokuwapo kesho, ama waweza kuidhibiti hiyo kesho?
2. hivi kwa kwenda kazini maana yake unajua litakalokuwapo kesho ama unaweza kuidhibiti hiyo kesho?
3. kwa kulima shamba maana yake unajua litakalotokea mwisho wa msimu, au unaweza kuudhibiti msimu?
4. ukianza kujenga unajua litakalotokea mwisho wa ujenzi, au unaweza kuudhibiti muda wote utakaochukuliwa kwa ujenzi?
5. ukianza masomo maana yake unajua litakalotokea utakapomaliza shule, au waweza kuudhibiti muda wote utakaochukua masomoni?
6. nk.

labda mie ndiye nina matatizo na itabidi niongeze bidii kujifunza maisha,

asante mpendwa na Mungu awabariki wote
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Asante mbu kwa post hii nzuri... but sisi wa afrika tuna changamoto sana... Baadhi ya wazazi wanaamini kuwa wamewekeza kwa watoto wao.. mfano kakusomesha basi weeeeee atabanana na wewe mpaka ukome. Kwa hiyo unakuta kijana ana familia yake, wazazi wake wanamtegemea kwa namna moja au nyingine wakati mwingine hata na wadogo zake. Hii ni changamoto kwa Watanzania tulio wengi kwani asilimia kubwa ya watu tunafanya kazi ili tule, tulipie bili mbalimbali then life goes on ..wakati mwingine kwa kutokujua, kuwa na mahitaji mengi kuliko kipato au kwa kukosa mbinu za kuwa na miradi itakayotuwezesha kuweza kulipia bill za maisha na kuwa na ziada ya kuwekeza kwa Badae. Duh.. mola tusaidie.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom