bacha
JF-Expert Member
- Aug 19, 2010
- 4,282
- 797
hapa tunazungumzia ule kabla ya kuanza kuanikwa juani au kulishwa kama mtoto
kumbe eeeh, kweli ndo maana " kivuli hakina rangi"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hapa tunazungumzia ule kabla ya kuanza kuanikwa juani au kulishwa kama mtoto
Duh sasa nyie mnaosema si rahisi kufikia 'uzee'? Mnataka kusema tukate tamaa?
Mbu hii habari ya kufikiria uzee saa hizi...dau unaweza kuzeeeka kesho boira kula maisha tu..
...lol, wewe mwenyewe umemuona kituko...kuna umri ukifika, inabidi ui control akili na maamuzi yako badala kuachia akili iamue...ndio utakuta akili inakwambia "kojoa" nawe unaachia kwenye suruali mbele ya wajukuu!
Mh Mbu hii kwa kweli inatia huruma kwa jinsi wazee wetu wengi wanavyoishi! Nakumbuka kulikuwa na mkutano mmoja ulioandaliwa na HelpAge International ambao waliainisha kuwa katika wazee wote nchini ni asilimia 4 tu ya waliokuwa covered na hizo pension zao!
But najiuliza hii fainali uzeeni kwa mkulima wa kijijini!! Mbona tutakuwa tunamwonea? Tukumbuke hiyo asilimia 4 ni wale waliokuwa wanafanya kazi za kuajiriwa!! Ambao wanastahili pension!!
Asante Mbu, sasa hapa wazazi wetu ambao ni wakulima tuwasaidie je?
kuna mtu kaniambia life expectancy yetu hairuhusu uzee niache uoga
...kaizer, kuna DNA test kuonyesha mwili wako ushafikia umri gani. Nitakuja na more info later. Mtaani jamaa kibao wa umri wangu tayari wanaonekana wazee kuliko umri wao...sasa sijui tatizo ni matokeo ya miaka 50 tangu uhuru wa Tanganyika, au ni genes...
Mimi nishajiamulia liwalo na liwe, almuradi hawatapitisha ujenzi wa barabara kuu kati kati ya kibanda changu, am safe for the time being. Chumba cha pili napangisha, maisha yanaendelea.
kuna mtu kaniambia life expectancy yetu hairuhusu uzee niache uoga
Good one Mbu, good one.........
when i was getting married (over seven years ago) i wanted a woman who was attractive, smart, a mother to my kids, a lover, a friend, sweetheart.... you name it!! i never factored issue ya maisha yetu after 70 years
Most of us (i believe) marry for the happy moments we dream of and sometimes we forget this important life after 60's
I only started to think of such scenarios last year when i watched a certain movie... and to be honest, so far i am too deep on investing for the kids and quality time
Kids are always a very good energy when couples get old
Sasa nimejua kwa nini vibinti vidogo vinang'ang'ania vibabu
Inside Every Old Man there is a Young Man Wondering, What the Hell Happened....
Mambo ya mafao dah wanawake bana muwage na huruma jamani kababu kanataka kufaidi mafao nyie ndo mnakachuna mpaka ngozi
Fidel sasa unataka Fainali waende na nani?? Lol!!!
...baba enock, iwapo mzee wako alivusha 60yrs, nawe andaa safari. Hayo ya magonjwa, ajali nk ni matokeo tu, hakuna anayeombea.
Nikisema fainali uzeeni ni pamoja na afya yako, ndugu jamaa na marafiki, kazi uifanyayo, uwezo wa kusomesha na kuhudumia familia nk...it's a whole life package.
Mbu ni kweli nakubali kuwa uzee hauna ajira nakubali ila sasa ajira pia inamatter katika kukuwezesha kujiandaa na kuangalia unajiandaaandaaje!
Naangalia mkulima kijijini ambaye kipato chake ni cha tumbo na mahitaji ya lazima, haimruhusu kusave au kuwekeza for the future, yeye ni jembe, jembe ni yeye. The only matumaini ktk kuwekeza ni elimu duni kwa watoto wake (hii ni kilio kingine) sasa mtu kama huyu ambaye miaka yote amekuwa akitumika pasipo faida ya kujiandaa na uzee, fainali yake inakuwaje?
Na isitoshe katiba ya nchi inasema wazee wote wako entitled to be protected ambap tunaamini ingekuwa ahueni kwa hawa wa vijijini au wasiojiweza but bayo ni kilio kingine tu!
anza sasa kujijengea mahusiano mazuri na mkeo uwe na mtu wa kujifariji nae miaka hiyo ya ukiwa, ....fainali uzeeni!
![]()
"When marrying, ask yourself this question: Do you believe that you will be able to converse well with this person into your old age?
Everything else in marriage is transitory."
Mada za Mbu ni kiboko ya akili!!Ilibidi niinakili kisha niwatumie watu wote walio karibu nami. Nimepokea majibu ya ajabu sana nilipouliza miwshowe: Je umejiandaa vipi kwa fainali uzeeni: Nilijibiwa:
Hakuna hata mmoja aliyeonyesha kuwekeza kwenye mahusiano na mwenza wake au hata watoto.
- Nimesomesha watoto kwa bei mbaya sana!
- Nimewekeza kwenye stocks
- Nimejenga na kusomesha
Inabidi kwa kweli tuwekeze sana kwenye MAHUSIANO NA WAUME/WAKE ZETU na hata watoto, au hata wale tulio nao karibu kimaisha.Usipofanya hivi utajikuta uko mpweke sana. Wazungu ambao wana nyumba za kutunzia wazee wanao msemo kabisa " be nice to your children because they are the ones to choose your old people's home"!!Ukiwa mtu mbaya kwao, watakuchagulia mahali pabaya sana na utakuwa huna usemi.Watakuwa hawaji hata kukutembelea Christmas!! Kwa sisi huku nchi za dunia ya tatu, kama watoto wako ulikuwa unawalisha kauzu na ugali wakati wewe ukila kuku na mishkaki ukiteremshia na bia, ujue uzee wako utakuwa reverse ya hiyo.... maana unapozeeka unageuka mtoto na watoto wako wanageuka "walezi" wako! Ukitaka waje kukujali kwa matunzo bora, basi waonyeshe matunzo mazuri ni yepi kimalazi, chakula na mavazi maana utakuwa umewaonyesha kwa mfano!
Vibabu Fidel vinakuwa havikuwekeza kwa wenzi wao, hivyo kwa vile vinakuwa havina company home, bas vinafurukuta huko je na kudakwa na "dakadaka".Usiombe uone kibabu kimeishiwa kinarudi home kufa!! Utaona huruma sana. Mara nyingi wakina mama hupata kampani ya watoto wao uzeeni kwa sababu wao walishikana na watoto enzi baba anakesha viti virefu!! Payback time chungu!
But for those who were prepared materially and socially, they age gracefully with respect
Fundisho ni kwamba jiandae ujanani usijeangukia "dakadaka" uzeeni.
Wataenda na wale vijana wa zamani wenzao.
Hiyo ndio summary y akila kitu ndugu yangu!! Asante sana kwa mchango wako na kutukumbusha kuhusu quality life.
![]()
"When marrying, ask yourself this question: Do you believe that you will be able to converse well with this person into your old age?
Everything else in marriage is transitory."
...anza sasa kujijengea mahusiano mazuri na mkeo uwe na mtu wa kujifariji nae miaka hiyo ya ukiwa, ....fainali uzeeni!
...hapana, hapana, hapana Mwj1 jamani, hapana, uuuuwwwwiiiiiiiiiii!......unless nimekusoma vibaya, lakini kuwekeza kwenye elimu ya mtoto/watoto (ili waje wakufae baadae) hiyo mimi siiafiki hata kidogo!...Ni wajibu wetu wazazi kuhakikisha mwanao unamsomesha na kumpatia kila aina ya msaada ili kumsaidia aweze naye huko mbele ya safari aje ajitegemee na apate na ahueni ya maisha yake, FULL STOP!
Kumsomesha mtoto ili iwe ni deni la kuja kukusaidia binafsi sikubaliani nalo kabisa jamani, hapa mpaka roho inaniuma nikifikiria eti nitakuja gombana na wanangu kisa hawataki kunisaidia. Hiyo ni hiari yao (kunisaidia),...kuwasomesha natimiza wajibu wangu kama mzazi. Wakiamua kutusaidia, nitashukuru Mungu, wakiamua kuuchuna, nitashukuru mungu..,.almuradi niliwapa msingi mzuri wa maisha, inatosha.
Jamani ee...Ole wenu mnaodhani eti kuwasomesha watoto wenu ndio investments za uzeeni hizo,...wao kuwasaidia uzeeni ni hiari, sio lazima.
Mwj1 wewe tutamalizana kwa wakati wetu, lol...!