Fainali Uzeeni!....

Fainali Uzeeni!....

mpendwa,
1. wewe unaweza kujua yatakayokuwapo kesho, ama waweza kuidhibiti hiyo kesho?
2. hivi kwa kwenda kazini maana yake unajua litakalokuwapo kesho ama unaweza kuidhibiti hiyo kesho?
3. kwa kulima shamba maana yake unajua litakalotokea mwisho wa msimu, au unaweza kuudhibiti msimu?
4. ukianza kujenga unajua litakalotokea mwisho wa ujenzi, au unaweza kuudhibiti muda wote utakaochukuliwa kwa ujenzi?
5. ukianza masomo maana yake unajua litakalotokea utakapomaliza shule, au waweza kuudhibiti muda wote utakaochukua masomoni?
6. nk.

labda mie ndiye nina matatizo na itabidi niongeze bidii kujifunza maisha,

asante mpendwa na Mungu awabariki wote

Ms Judith unisamehe tu, labda ni mimi nakusoma vibaya. Labda nikuulize hivi,
Hakuna umuhimu wa kujiwekea akiba kwakuwa huna uhakika na kesho?

Tafsiri yangu ya kujiwekea akiba uzeeni haina maana akiba hizo zitakidhi mahitaji yote, ila
kwa kiwango fulani akiba hizo zitasaidia kupunguza makali kwa yale ambayo tunapaswa kujihadhari nayo.
 

Ms Judith unisamehe tu, labda ni mimi nakusoma vibaya. Labda nikuulize hivi,
Hakuna umuhimu wa kujiwekea akiba kwakuwa huna uhakika na kesho?

Tafsiri yangu ya kujiwekea akiba uzeeni haina maana akiba hizo zitakidhi mahitaji yote, ila
kwa kiwango fulani akiba hizo zitasaidia kupunguza makali kwa yale ambayo tunapaswa kujihadhari nayo.

ndugu yangu Mbu,

mi naona tuko pamoja kwa kila kitu ila labda tunakosa common definition kwa mambo fulanifulani.

hapo juu uliponiquote nilikuwa namjibu MJ1 aliyesema kuwa if i cant control the future, kwa nini naenda kazini na akataka kujua future humaanisha muda gani!! so nilichoandika kilikusudia kumpa mpendwa Mwanajamii na wengine fursa ya kutafakari zaidi juu ya kwamba hakuna binadama anayeweza kuidhibiti future hata kama ni dakika moja tu ijayo. kisha kwa sababu in practice kila tukifanyacho hukifanya kwa matumaini, basi hatuna certainty ya 100% ya yatakayokuwako kesho na tunaishi kwa kumtumaini tu kwa Mungu.

kuhusu akiba hata mimi najitahidi kujiwekea lakini nafanya hivyo kwa kuwa namtumaini Mungu na siitumaini akiba. kwangu mimi naishi LEO na fainali ni LEO! kuhusu mahusiano hata uzeeni kuna kujenga mahusiano. mchukulie mfano mzee mandela alitalikiana na mkewe uzeeni mwake lakini leo amezungukwa na watoto, wajukuu na ana accompany ya uhakika ya graca machel amabye alijenga naye mahusiano uzeeni mwake kwa kuvunja ukimya. huenda mandela anawashinda hata baadhi ya vijana wa leo kwa accompany na wingi wa marafiki. naamini hayo hayakuasababishwa na siasa zake wala akiba yake aliyojiwekea huko nyuma bali kudura za Mwenyezi Mungu, na sisi tumtumaini Mungu zaidi kama tunataka kuziona siku zetu njema zenye furaha na faraja uzeeni.

tuko pamoja na Ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!
 
Back
Top Bottom