Fainali ya ASFC | Yanga SC 3 (4) - 3 (1) Coastal Union | Uwanja wa Sheikh Amri Abeid | Yanga BINGWA

Fainali ya ASFC | Yanga SC 3 (4) - 3 (1) Coastal Union | Uwanja wa Sheikh Amri Abeid | Yanga BINGWA

Hitimisho kwa michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa mchezo wa fainali kupigwa leo Julai 2, 2022 kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha, ambapo Mabingwa wa Nchi kutoka viunga vya Jangwani Yanga SC, wanakwaruzana na Wajuzi wa soka Wagosi wa Kaya Coastal Union kutoka mkoani Tanga.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali mno na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90, kutokana na aina ya uhitaji wa mechi hiyo kwa kila timu, ambapo Yanga SC wakiwa na dhamira ya kuweka historia kutwaa ubingwa ngao ya Jamii, Ligi Kuu na ASFC, huku Coastal Union pamoja na kuhitaji sana ubingwa huu ASFC vile vile wakitaka kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Kimataifa.

Nani kuweza kuibuka na ubingwa wa (ASFC) Kombe hili lenye mvuto na la pili kwa ukubwa nchini Tanzania? Nidhamu ya kujilinda na kushambulia ndo majibu yatapatikana baada ya mchezo kumalizika..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 9: 00 Alasiri, Usikose Ukaambiwa Mwana Kulipewa Wewe..!

Twende pamoja..!


Nyomi ya mashabiki uwanja wa Sheikh Amri Abeid wapo kwenye foleni tayari kwa ajili ya kuingia kushuhudia mtanange wa ASFC.

==========================

Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Timu zote zipo tayari.

05' Naaam mpira umeanza kwa kasi huku kila timu ikichukua tahadhari kubwa, kuepusha makosa dakika hizi za mwanzo.

10' Sopu Goooooooooooaaal goal

Abdul Sopu anaipatia Coastal Union bao la kwanza baada ya Krosi mujarabu kutoka kwa Akpan

15' Yanga wanakosa nafasi mbili mfululizo za wazi kupitia kwa Mayele, kazi nzuri kwa golikipa wa Union

20' Mwamnyeto anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Union, ni Free Kick kuelekea Yanga.

Uwanja umejaa huku Coastal Union wakitakata dakika hizi za mwanzo, wapo mbele kwa bao moja.

Kuna mchezaji Vincent wa Coastal yupo chini baada ya kupata rabsha, mpira unaendelea.

25' Yanga wamepata Kona tatu ambazo hazikuzaa bao, mabeki wa Coastal wapo imara

30' Abubakar wa Yanga anashindwa kutulia na kuweza kuweka mpira kambani, ilikuwa nafasi nzuri kabisa.

35' Coastal wamefanikiwa kudhibiti presha ya Yanga kipindi hiki cha kwanza, labda Yanga waje na mbinu tofauti

40' Shambulizi kali kuelekea Yanga, mpira unapigwa mbele, lakini golikipa Diara anacheza.

Mpira unachezwa kwake Mayele, lakini mabeki wanakataa..Ngoma ni ngumu.

45+3' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo Coastal wapo mbele ya bao moja.

Faisal anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango la Coastal Union.

Kona inapigwa kuelekea Coastal, inapigwa kulee mpira unamkuta Akpan anagonga kichwa na unamkuta Mayele anapiga Tikitaka lakini inakata.

Naaam mpira ni mapumziko, Kumbuka mchezo wa ASFC

HT: Yanga SC 0-1 Coastal Union

Kipindi cha pili kimeanza huku Yanga wakipata Kona ambayo haikuzaa bao

Ametoka Chiko na ameingia Makambo upande wa Yanga SC

50' Yanga wanajaribu kutafuta mpenyezo kwa mabeki wa Coastal, lakini mipango yao inakuwa migumu

Miraji anaonyeshwa KADI ya Njano, ni free kick kuelekea Coastal, inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa

57' Feisal Goooooooooooooaaal.. Feisal anaisawazishia Yanga SC bao akipokea pasi kutoka kwa Makambo

Aucho anapiga shutii lakini linachezwa na kuwa Kona ambayo imedakwa na golikipa Mussa.

61' Mubarak Hamza anakosa nafasi nzuri ya kufunga, yeye na golikipa Diara..!

Mpira umeanza kuamka kwa pande zote mbili kupelekea mashambulizi mazito

Pascal Kitenge ameingia kuchukua nafasi ya mtu, upande wa Coastal Union

70' Coastal Union wanapanga mipango sasa, mpira unapigwa mbele lakini golikipa Diara anacheza mpira ule.

Joseph Ziwa anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya, huku Coastal wakifanya mabadikio ameingia Chambo.

73' Makambo anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea Coastal

75' Feisal Ooooh, anakosa nafasi nzuri ya kufunga, mpira wake umepaa juu ya lango.

Coastal wanakosa nafasi tena, mpira unaambaa ambaa unatoka nje ni wa kurusha, Akpan yupo chini akipatiwa matibabu.

81' Makambo Goooooooooooooaaal gooal.. Makambo anaipatia Yanga SC bao la pili, shuti kali la kimo cha mbuzi linamuacha golikipa Mussa akichumpa bila mafanikio.

Haya mpira ni mkali sana hii ni hadhi ya fainali sasa.

Sopu Goooooooooooaaal goal

Abdul Sopu anaipatia Coastal Union bao la pili, akijitwisha kichwa na kumuacha golikipa Diara akiangalia tu Kijana hatari sana.

Ngoma nzito sana, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, piga nikupige.

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu

Mayele anakwenda, anapiga shutii lakini Ziwa anacheza na kuokoa hatari ile.

Aucho katika ya uwanja, anapiga kumtafuta Makambo, lakini Coastal Union wanakaa imara.

Naaam dakika 90 zinakamilika, sasa ni wakati wa dakika za za nyongeza au mikwaju ya penalty mpaka bingwa apatikane.

FT: Yanga SC 2-2 Coastal Union

Naaam mpira unaendelea dakika za nyongeza, Yanga wanapata Kona ambayo haikuzaa bao.

92' Farid anapiga kona nyingine lakini mabeki wa Coastal wanakaa imara kuondoa hatari ile.

98' Sopu Goooooooooooaaal goal

Abdul Sopu anaweka kambani bao la tatu Hat-trick baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Yanga

Ametoka Mwamnyeto na ameingia Nkane upande wa Yanga SC

Vicente Abubakar anashindwa kutuliza mpira wa Krosi, ilikuwa nafasi nzuri kufunga bao

105' Yanga wanashambulia lango la Coastal, lakini mabeki wanakaa imara kuondoa hatari.

106' Golikipa Mussa yupo chini baada kukumbana na Mayele, anapatiwa matibabu.

110' Mpira unaendelea huku Bangala akimsukuma mchezaji wa Coastal, Yanga wanapigwa baridi hapa.

113' Nkane Goooooooooooooaaal gooal, Nkane anaweka kambani bao la tatu | Yanga SC 3-3 Coastal Union

Akpan anagonga kichwa lakini mpira unatoka nje, ilikuwa nafasi murua hapa,

Ameingia Haji na ametoka Vicente Abubakar upande wa Coastal Union

Diara yupo chini akipatiwa matibabu, ameinuka mpira unaendelea, Kona inapigwa kuelekea Yanga, lakini mpira unatoka upande mwingine.

Sopu anamgeuza Aucho, hatariii anapiga shutii gooo laaaaaa, ilikuwa hatari tunazika kabisa.

120' Unapigwa mbele kuleee kwake golikipa Mussa akichumpa na kudaka

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Timu zote zikitoka sare ya mabao matatu kwa matatu, sasa ni mikwaju ya penalty.

=====

Yanga SC wametwaa ubingwa wa ASFC, baada ya kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalty mabao manne kwa mawili 4-2 baada ya kumalizika dakika 120 mabao matatu kwa matatu 3-3.
Ndio madhara ya kujiamini kupita kiasi, yaani leo bahati ilikuwa yetu. Yaani hii mechi ilinifanya juice ya boksi ya Azam ionekane chungu.
 
Yaani ata magoli ya costal sijaelewa jinsi yalivyo fungwa fungwa, Mpira wa kiswahili ni mgumu sana. Yaani Yanga wanashambuliaaa Kwa nguvu zote lakini goli Ali ingii ila costal wakishambulia wanafunga ki ulaini.
Tunashukuru timu iliyo staili kushinda imeshinda.
 
Daah Nilishakata Tamaa Kabisa ....Kweli Is Not Over Until Is Over !!, Yanga Afrikaa [emoji471][emoji172][emoji169][emoji8][emoji8][emoji8][emoji91]
Hata mimi nilikubali matokeo tangu mchezo unaanza. Kilichowabeba Yanga ni ukomavu tu wa wachezaji wao!

Ila kiukweli mchezo wa leo haukuwa kabisa upande wao.
 
Club le Athletic Internationale dar es salaam Young Africans.
BINGWA
 
Halafu watapiga fataki.
Coastal deserve to be winners.
Yanga kinachowasaidia ni hamasa ya wachezaji ( kwa kulipwa vizuri) na pia mfadhili wao anatumia pesa sana kupata mafanikio.
Vinginevyo anayejua mpira hassa Yanga hamna timu pale. Wana pesa.
 
Halafu watapiga fataki.
Coastal deserve to be winners.
Yanga kinachowasaidia ni hamasa ya wachezaji ( kwa kulipwa vizuri) na pia mfadhili wao anatumia pesa sana kupata mafanikio.
Vinginevyo anayejua mpira hassa Yanga hamna timu pale. Wana pesa.
Mbona unaumia sana? Mpira upo simba.
 
Halafu watapiga fataki.
Coastal deserve to be winners.
Yanga kinachowasaidia ni hamasa ya wachezaji ( kwa kulipwa vizuri) na pia mfadhili wao anatumia pesa sana kupata mafanikio.
Vinginevyo anayejua mpira hassa Yanga hamna timu pale. Wana pesa.
Huwezi kutofautisha Mpira na Pesa Mzee wangu
 
Halafu watapiga fataki.
Coastal deserve to be winners.
Yanga kinachowasaidia ni hamasa ya wachezaji ( kwa kulipwa vizuri) na pia mfadhili wao anatumia pesa sana kupata mafanikio.
Vinginevyo anayejua mpira hassa Yanga hamna timu pale. Wana pesa.
Hamna timu kivipi Sheikh! Yanga ndiyo Mbingwa wa Ngao ya Jamii, Ligi kuu NBC, na sasa Shirikisho ASFC!

Halafu unasemaje hamna timu! Mpira umechezwa, na kila mtu ameona.
 
Back
Top Bottom