Faini bilioni 5/- kampuni ikivujisha taarifa binafsi

Faini bilioni 5/- kampuni ikivujisha taarifa binafsi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kibano dhidi ya kampuni au shirika linalofanya makosa ya ufichuaji wa taarifa binafsi, ikiwamo kuuza taarifa sasa kinanukia baada ya serikali kupendekeza bungeni kutungwa sheria itakayokuwa na adhabu ya faini isiyopungua Sh. milioni moja na isiyozidi Sh. bilioni tano.

Ikiwa ni mtu binafsi atakayebainika kutenda kosa na kutiwa hatiani chini ya kifungu cha 60 (6) (a) cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022, atalipa faini isiyopungua Sh. 100,000 na isiyozidi Sh. milioni 20 au kifungo kisichozidi miaka 10 au vyote kwa pamoja.

Muswada huo wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 ulisomwa kwa mara ya kwanza jana bungeni jijini Dodoma na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi.

Kuhusu makosa ya uharibifu, ufutaji, ufichaji au ubadilishaji wa taarifa binafsi, sheria hiyo inapendekeza atakayetiwa hatiani kwa kutenda makosa hayo, atalazimika kulipa faini isiyopungua Sh. 100,000 na isiyozidi Sh. milioni 10 au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Adhabu ya jumla chini ya kifungu cha 63 (b) cha sheria hiyo inaelekezwa kuwa baada ya mtu kutiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya sheria hiyo, mahakama inaweza kuamuru kukamatwa kwa vifaa vyake vyenye taarifa binafsi vilivyohusika katika kutenda kosa.

Pamoja na mambo mengine, sheria hiyo inaeleza kuwa mkusanyaji ambaye bila sababu za msingi, atafichua taarifa binafsi kwa njia yeyote ambayo haiendani na madhumuni ambayo taarifa hiyo imekusanywa, atakuwa anatenda kosa.

Kwamba, atapata taarifa binafsi au atapata taarifa yoyote inayojumuisha taarifa binafsi bila idhini ya mkusanyaji au mchakataji, ambaye anahifadhi taarifa hiyo, atafichua taarifa binafsi kwa mtu mwingine atakuwa ametenda kosa.

Na mtu atakayeuza taarifa binafsi, ambayo imepatikana kwa ukiukwaji wa kifungu kidogo cha (1) cha kifungu cha 60 cha sheria hiyo, atakuwa ametenda kosa.

Kwenye sheria hiyo inayopendekezwa, mtu ambaye ataizuia au kuikwamisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutekeleza mamlaka yaliyotolewa chini ya sheria hiyo, kushindwa kutoa msaada au taarifa zilizoombwa na tume, endapo atatiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua Sh. 100,000 na isiyozidi Sh. milioni tano au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.

Mojawapo ya mamlaka ya tume hiyo wakati wa uchunguzi ni pamoja na kumhoji mtu yeyote au kuondoka na kifaa chochote chenye taarifa binafsi katika jengo lolote, alimoingia mkusanyaji wa taarifa kwa ajili ya kujiridhisha endapo jengo hilo linakidhi mahitaji ya usalama.

Chanzo: Nipashe
 
Kapuku wewe una taarifa gani binafsi ambazo ni "sensitive" hapo wanaolindwa na Sheria hii ni kwa mfano Msoga kutoa gesi kumkomboa mwanae kutoka mikononi mwa mchina, rais kuwa kimada na sio mke wa ndoa, daktari wa rais kupewa donge na kuvunja kiapo chake, wakuu wa wilaya ambao wanamimba au wamezaa na waume za watu, nk...
 
Itawasaidia vijana waliosoma kupata pesa. Maana unakuta cv zao zimegeuzwa kuwa vifungashio.

Au wanafunzi mithiani yao imegeuzwa kua vifungashio
 
Back
Top Bottom