Faini ya Milioni 350 dhidi ya viongozi wa Chadema itumike kuwalipa fidia wazazi wa Akwilina

Geeque

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2007
Posts
936
Reaction score
319
Hukumu iliyotolewa na hakimu wa mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam ikiwataka viongozi wa Chadema walipe faini ya shilingi milioni 350 itumike kuwalipa fidia wazazi wa marehemu Akwilina Akwiline. Haingii akilini hii pesa kurudi serikalini wakati waathirika wakubwa wa mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi la Polisi la Tanzania ni familia ya marehemu Akwilina.

Ni muda muafaka kwa familia ya marehemu Akwilina kutafuta mwanasheria mzuri na kufungua kesi ya madai ya kifo cha mtoto wao mpendwa dhidi ya Jeshi la Polisi Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kesi hii ya madai ilenge kudai fidia kutokana na pesa zitakazopatikana kupitia faini hiyo.

Rais Magufuli amekuwa akijipambanua kuwa yeye ni rais wa wanyonge, basi huu ndio muda muafaka kuonyesha kwa vitendo upendo wake kwa wanyonge kwa kuagiza pesa zote zitakazopatikana kutokana na faini dhidi ya viongozi wa Chadema zilipwe kwa familia ya marehemu Akwilina Akwiline.

 
Sheria inasemaje au unaropoka tu?
Sheria ipi? Fafanua. Walilipwa fidia wezi wa mafuta Morogoro na sasa wanajengewa mnara wa mashujaa! Wale wa kijiji kizima huko Mbeya hawakulipwa wala hawakujengewa mnara wa mashujaa kutokana na wizi wao wa mafuta.
 
Kwani CDM wanahusikaje hapa? Fidia maana yake nini?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geeque,
UMEKOSA MTAJII WAMAISHA MNATAKAA KUCHANGIWA KUPITIA AKWILINA HIZO FAMILIA ZA AJABU AISEE PAMBANEN NA HALI ZENUU PESA ZA MAHAKAMA.SIO ZA MAHAWARA UNACHAGUA UMPE NANI
ALLAH ONDOA HIII KICHEFI CHEF
 
Mafisadi na Majizi ya ccm yamepanga kuitumia hiyo fedha kwa familia zao
 
Geeque,

..sijui hili litakuchekesha au kukukasirisha.

..lakini serikali iliwavutia bomba la maji familia ya Akwilina.
 
Sheria inasemaje au unaropoka tu?

..Familia ya Lt.Gen.Imran Kombe ambaye aliuawa kimakosa na askari polisi wakati wa utawala wa Raisi Mkapa waliishtaki serikali na kulipwa fidia.

..kwa upande wa Akwilina familia yake inatakiwa ifungue kesi ya madai dhidi ya serikali. Kuna ugumu ktk kesi yao ambao sitataka kuutaja hapa, lakini they should try.

..mwingine anayepaswa kufungua kesi dhidi ya serikali ni familia ya muandishi wa habari Daudi Mwangosi ambaye aliuwa na askari wa kikosi cha kutuliza fujo wakati wa utawala wa Raisi Kikwete.
 
Kwani aliye muua akwilina ni nani? Maana hakuna mahali katika hukumu pameonesha kuwa viongozi wa CDM walikuwa na bunduki na kuwa walimuua Akwi. Maana hakuna shita la mauaji kwa viongozi hao. Waliokiri kumuua Akwi ni polisi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…