Faiza Ally ampa ushauri mzito Diamond Platnumz ‘hujaiona dunia hata robo’

Faiza Ally ampa ushauri mzito Diamond Platnumz ‘hujaiona dunia hata robo’

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amempa ushauri msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuwa kwa sasa ni muda wake wa kula ujana na kuizunguuka dunia na sio muda wa kujipa majukumu mazito ile hali umri wake bado mdogo.
Faiza Ally amesema Diamond bado hajamaliza hata robo ya dunia hivyo ingawaje ana jina kubwa barani Afrika hivyo angefanya kwanza vitu kama hivyo kuizunguuka dunia ikibidi ajiweke kando na mambo ya mahusiano.
wegvrtd.jpg

Diamond kijana mdogo sana anahitaji kuhave funny na watoto wenzie na sisi wadada wazima lazima taungalie watu wa kutoka nao, Go baba have a funny enjoy the world ndio useto down,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshauri kuwa ikibidi ajiweke mbali na mahusiano.

Jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano, bado hujaiona dunia hata robo wewe ni star hela ipo there is alot to see nasema with clean heart no hate kwa Zari au kwa yeyote.“ameandika Faiza.

Ushauri huo umekuja ikiwa ni wiki sasa imepita tangu kuenee tetesi kuwa Diamond Platnumz yupo kwenye mahusiano na msichana maarufu kwenye mitandao ya kijamii anayejulikana kwa jina la Tunda.
-Bongo5-
Faiza hajamumunya maneno... Chibu ale maisha tu kwa sasa
 
Kama sikosei kulikuwa enzi hizo na uzi wa kumlaumu Diamond kuhusu kumwachisha shule huyu binti au nazeeka vibaya
uzi ule ulikuwa unamuhusu lynn,yule video qn wa "Kwetu" wa rayvanny na sio Tunda.
 
Diamond kijana mdogo sana anahitaji kuhave funny
anahitaji kuhave fun....lugha ya malkia hii
 
Back
Top Bottom