Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Natahadharisha!
Ukiona jambo nalizungumzuia ujue tayari nimeshalipima. Lina uzito.
Utani na mzahamzaha unaoendelea kwenye nchi yetu unaunda falsafa na mtazamo mpya juu ya kizazi kijacho katika taifa letu.
Kujidharau
Kujidunisha na kujiona sisi ni taifa la hivyo.
Watu wetu ni wa hovyo.
Vijana wetu ni wa hovyo na vioja.
Wanawake wetu ni wahovyo
Wanaume ni viongozi wa hovyo.
Zingatia hakunaga kitu chenye akili kikachekesha. Vichekesho na vioja hulenga zaidi kuufanya ujinga au mzaha ufurahishe.
Vitu makini au vyenye kutumia akili havichekeshi wala kuchekesha.
Tumekubali kujitambulisha kama taifa la vichekesho?
Taifa la Watu wakuchekwa?
Taifa la futuhi!
Taifa la vikatuni!
Kizazi chipukizi tunakilea katika msingi wa kuchekesha, kuchekwa na kuwa wachekeshaji mahiri Duniani.
Tunahitaji viongozi wa kuliona hili, tunahitaji viongozi wenye macho na kujua taifa hili linahitaji ulinzi sio tuu wa mali na rasilimali bali ulinzi wa Fikra, falsafa, na mitazamo ambayo ndio huleta maendeleo kwa Watu.
Taifa ambalo falsafa yake itajengwa kama channel ya vichekesho haliwezi kuwa taifa la maana. Haliwezi kuwa taifa la kutegemewa, haliwezi kuwa taifa makini lenye maendeleo.
Watu wa propaganda na wahusika wote wa mambo ya habari, mawasiliano na ûtamaduni angaliane jambo hili.
Nimemaliza.
Robèrt Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam