MTANZANIA620
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 105
- 116
FALSAFA YA 4R NI JIBU LA SIASA ZA TANZANIA YA LEO NA KESHO
Ameandika: Cde Shaka Hamdu Shaka
SIASA BILA FALSAFA NI KELELE
Kila kiongozi mkubwa duniani anakumbukwa kwa falsafa yake. Kwa Tanzania mfano ulio hai ni Mwalimu Julius K. Nyerere, leo anakumbukwa na amekuwa urithi wetu kutokana na falsafa yake ya Ujamaa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiletea Tanzania falsafa yake ya 4R - na hapa ndipo inawezekana kuna ambao kwa namna moja ama nyingine hawajamwelewa. 4R si maneno ya mkutano, ni Itikadi ya Utawala (Political Doctrine) inayokuja kupambana na magonjwa matatu makubwa ya siasa za Afrika: Kisasi, Hofu na Mkwamo.
1. RECONCILIATION (MARIDHIANO)
Kabla ya 4R, siasa za nchi nyingi za Afrika zilijengwa juu ya kulipiza kisasi. Kiongozi mpya akija anafuta kila kitu cha mtangulizi wake. Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuja na Maridhiano. Maana yake kisiasa ni nini?
1. Maridhiano ya Ndani ya CCM: Kuunganisha makundi yote ndani ya Chama. Hakuna mzee wa CCM, hakuna kijana wa CCM - wote ni damu moja.
2. Maridhiano ya Kitaifa: Kufungua milango kwa upinzani, kwa vyombo vya habari, kwa makundi yote. Siasa si vita na mpinzani si adui wa Taifa.
3. Maridhiano na Historia: Hakumkana yeyote. Badala yake alisema, kila awamu ina mchango wake. Hii ndiyo siasa ya kiungwana.
Wanaosema Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mpole, hawajui kuwa Maridhiano ndiyo silaha ngumu kuliko bunduki. Ni ujasiri wa hali ya juu kusamehe na kuunganisha kuliko kulipiza.
Kwa nini tunasema "Maridhiano ni Silaha Ngumu Kuliko Bunduki"?
Bunduki inalazimisha mtu anyamaze kwa hofu, lakini Maridhiano yanamfanya mtu anyamaze kwa heshima na kukubaliana. Maridhiano yana nguvu kubwa ya kumaliza chuki na kupandikiza upendo kwa kizazi na kizazi.
Hii ndiyo sababu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuchagua silaha ngumu. Ni rahisi sana kwa Rais kulipiza kisasi, lakini alichagua njia ngumu zaidi: Kusamehe na Kuunganisha.
Kusamehe kunahitaji moyo wa chuma, kulipiza kisasi kunahitaji hasira tu - hata mtu dhaifu anaweza kulipiza. Ndiyo maana tunasema Maridhiano ni Ujasiri, si Uoga. Ni Iron Lady anayeweza kusimama katikati ya watu waliomkosea na kusema "Tusonge mbele", akiamini kuwa maridhiano yanajenga Taifa. Na ni ukweli usiopingika kuwa Taifa letu leo linahitaji Maridhiano kwa ajili ya hatima ya kizazi cha leo, kijacho na Taifa kwa ujumla.
2. RESILIENCE (USTAHIMILIVU)
Ustahimilivu kisiasa ni uwezo wa nchi kusimama imara wakati dunia inatikisika.
Wakati wa UVIKO-19, vita vya Ukraine, na kupanda kwa bei za mafuta, nchi nyingi zilianguka. Tanzania haikuanguka. Kwa nini? Kwa sababu ya Resilience.
Kisiasa, Resilience inamaanisha:
Hii ndiyo maana tunasema Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Iron Lady. Chuma chake kiko kwenye ustahimilivu, si kwenye kelele.
3. REFORM (MAGEUZI)
Kuna watu wanaendelea kushuhudia mabadiliko mbalimbali ya siasa za kidunia lakini wanaogopa mageuzi. Wanataka kila kitu kibaki kama cha 1977.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasema HAPANA. Lazima tuendane na mahitaji ya wakati, kinachohitaji kurekebishwa kirekebishike. Baadhi ya mageuzi ya 4R ni:
1. Mageuzi ya Kiuchumi: Kuruhusu sekta binafsi kuajiri vijana, si kila kitu Serikali.
2. Mageuzi ya Kisheria: Kuunda Tume ya Haki Jinai, kuboresha sheria za uchaguzi na vyama vya siasa.
3. Mageuzi ya Kiutawala: Serikali ya kidigitali, kupunguza urasimu.
Mageuzi haya ndiyo yanayoifanya CCM isibaki kuwa chama cha historia, bali chama cha kesho. Ukweli unabaki kuwa, yeyote anayepinga mageuzi, anapinga maendeleo ya CCM yenyewe, ambayo nguvu yake ni kubwa kisiasa kwa vile imebeba hatima thabiti ya Taifa letu.
4. REBUILDING (KUJENGA UPYA)
Baada ya maridhiano, ustahimilivu na mageuzi, hatua ya mwisho ni Kujenga Upya. Kujenga upya si kujenga barabara tu. Ni kujenga upya:
Dkt. Samia Suluhu Hassan anajenga upya Taifa ambalo kila Mtanzania ajivunie. Anajenga upya CCM ili iendelee kuaminika zaidi kwa kusimamia maendeleo endelevu katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa, katika mustakabali mzima wa amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu.
4R ZA DKT. SAMIA NDIO CHAGUO PEKEE
Leo Tanzania ina njia mbili tu kama ifuatavyo;
Njia ya Kwanza: Ni njia ya siasa za majungu, za kisasi, za kupayuka mitandaoni, za kusema kila kitu kibaya na kutaka nchi ichafuke ili viongozi waonekane wamefeli.
Njia ya Pili: Ni njia ya 4R. Njia ya maridhiano, ustahimilivu, mageuzi, kujenga upya na kusameheana.
Tunao wajibu mkubwa wa kuendelea kukumbushana na kuelimishana kama Taifa ili kusimama imara kwenye Njia ya Pili, ambayo ndiyo njia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan (IRON LADY).
Kwa sababu 4R si falsafa ya Dkt. Samia peke yake, ni falsafa ya Tanzania inayotaka amani, mshikamano na umoja wa kitaifa. Kwenye hili, yeyote anayeipinga 4R, anataka Tanzania irudi kwenye siasa za chuki na kisasi. Kuzingatia kuwa Watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na hilo, wote kwa umoja wetu kama Taifa tunayo kila sababu ya kusimama pamoja na kumuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya dhamira yake hii njema. Iko siku historia ya nchi itamkumbuka kuwa ni miongoni mwa viongozi mashuhuri waliohubiri na kusimamia Amani ya kweli katika Taifa letu.
Wasalaam.

- Kutokutikisika na kelele za mitandaoni.
- Kutokupandikiza nchi kwenye vita vya kibeberu vya mataifa makubwa.
- Kulinda uchumi wa wananchi licha ya dhoruba.
Hii ndiyo maana tunasema Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Iron Lady. Chuma chake kiko kwenye ustahimilivu, si kwenye kelele.
3. REFORM (MAGEUZI)
Kuna watu wanaendelea kushuhudia mabadiliko mbalimbali ya siasa za kidunia lakini wanaogopa mageuzi. Wanataka kila kitu kibaki kama cha 1977.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasema HAPANA. Lazima tuendane na mahitaji ya wakati, kinachohitaji kurekebishwa kirekebishike. Baadhi ya mageuzi ya 4R ni:
1. Mageuzi ya Kiuchumi: Kuruhusu sekta binafsi kuajiri vijana, si kila kitu Serikali.
2. Mageuzi ya Kisheria: Kuunda Tume ya Haki Jinai, kuboresha sheria za uchaguzi na vyama vya siasa.
3. Mageuzi ya Kiutawala: Serikali ya kidigitali, kupunguza urasimu.
Mageuzi haya ndiyo yanayoifanya CCM isibaki kuwa chama cha historia, bali chama cha kesho. Ukweli unabaki kuwa, yeyote anayepinga mageuzi, anapinga maendeleo ya CCM yenyewe, ambayo nguvu yake ni kubwa kisiasa kwa vile imebeba hatima thabiti ya Taifa letu.
4. REBUILDING (KUJENGA UPYA)
Baada ya maridhiano, ustahimilivu na mageuzi, hatua ya mwisho ni Kujenga Upya. Kujenga upya si kujenga barabara tu. Ni kujenga upya:
- Imani ya wananchi kwa Serikali yao.
- Heshima ya Tanzania duniani.
- Umoja wa Kitaifa uliokuwa umeanza kupasuka.