NosimLaizer
New Member
- Aug 2, 2022
- 2
- 0
Na mwandishi Nosim.
Elimu ni ujuzi, utambuzi au maarifa. Kwa kulitambua hili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano
waTanzania imejidhatiti katika sekta ya elimu kwa kuipa kipaumbele. Serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto kubwa inayopelekea wananchi haswa vijana na watoto kukosa elimu bora.
Mnamo mwaka 2016 serikali ya Tanzania iliamua kupitisha sera ya elimu bila malipo kwa wananchi wake, kwa ngazi ya shule za msingi na sekondari. Habari hii ilikua njema sana kwa kila mzazi na mlezi aliyesikia kuhusu hili. Wazazi na walezi waliona kama wametua mzigo mzito kichwani.
Elimu bila malipo imekua neema kwa kila mzazi na mlezi kwani, asilimia kubwa ya wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo walifanikiwa kurudi na kuendelea na masomo.
Licha ya elimu bila malipo kufanikisha wanafunzi walioshindwa kusoma kwa sababu ya changamoto za kifedha, elimu bila malipo haijafanikiwa kutimiza ndoto za vijana wengi.
Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, elimu bila malipo imefanikisha wazazi na walezi kuwapeleka watoto shuleni kwa ngazi za elimu ya msingi na sekondari. Vivyo hivyo wameshindwa kutimiza ndoto za watoto wao kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, hivyo wameishia kuwapeleka shule za msingi na sekondari na kushindwa kuwafikisha elimu ya juu (yaani chuo kikuu).
Hali hii imepelekea kuongezeka kwa wimbi kubwa la makundi hatarishi. Vijana wengi wameshindwa kuendelea na masomo sababu kubwa ikiwa hali duni ya maisha na hivyo kupelekea kuongezeka kwa makundi hatarishi. Makundi haya yanajumuisha matendo maovu kama vile wizi na ukabaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya,nk.
Vijana huamua kujiunga na makundi haya lengo kubwa likiwa kupata kipato kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Janga hili lingeweza kuepukika endapo vijana hawa wangepata nafasi ya kusoma na kuhitimu masomo yao ya chuo kikuu, ambapo wangeweza kujiajiri au kuajiriwa. Ni vijana wachache sana hupata ajira au kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao kwa ngazi ya sekondari.
Nini kifanyike ili kupunguza wimbi la makundi hatarishi yatokanayo na vijana kushindwa kusoma na kufikia malengo yao?
(I) Serikali inapaswa kufanya jambo ili kusaidia vijana wanaoshindwa kumaliza masomo yao kwa ngazi ya kidato cha tano na cha sita, na ngazi ya chuo kikuu kutimiza malengo yao.
Serikali inapaswa kutoa mikopo kuanzia ngazi ya cheti na si astashahada peke yake kama ilivyo sasa. Kufanya hivi kutasaidia vijana wenye hali duni za maisha kuweza kujikimu na kujiendeleza kimasomo. Serikali itakapotekeleza hili, itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kukomesha matendo ya kiuhalifu yanayosababishwa na vijana, lengo likiwa ni kujikimu kimaisha.
(II) Wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa serikali, ili kutimiza ndoto za vijana.
Serikali ya Tanzania ilipoanzisha falsafa ya Elimu bila malipo, wazazi na walezi wengi wamekuwa wapuuziaji kwa kutofuatilia elimu wanazopewa watoto wao wakiamini Serikali imechukua jukumu zima. Hali hii imepelekea watoto kukosa elimu bora kwa sababu Serikali peke yake haiwezi kubeba jukumu la kufuatilia elimu kwa kila mwanafunzi, bila ushirikiano wa wazazi na walezi.
Serikali inapaswa kutoa hamasa au elimu kwa wazazi na walezi kuwa jukumu la kusomesha na kufuatilia elimu wanazopewa wanafunzi, si la serikali peke yake! Badala yake, wazazi na walezi wanapaswa kutoa ushirikiano ili kutimiza ndoto na malengo ya vijana.
(III) Serikali inapaswa kuanzisha mfumo wa wanafunzi (haswa wanafunzi wa ngazi ya sekondari) kuelimishwa jinsi ya kujitegemea haswa wanapomaliza masomo yao (yaani kidato cha nne).
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wanapohitimu masomo yao, hutegemea kuajiriwa na Serikali. Mtazamo huu umepelekea idadi ya vijana wasio na ajira kuongezeka kila mwaka. Elimu ya namna ya kujitegemea itakapotolewa kwa wanafunzi, itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza fikra za vijana na kupunguza au kuondoa kabisa wimbi la vijana wasio na ajira.
(IV) Serikali inapaswa kutoa elimu kwa vijana kwa kuwaondolea mtazamo hasi kwamba wanasoma ili waajiriwe/wajiajiri.
Watanzania wengi wamekuwa na mtazamo kwamba wanasoma au wanawapeleka watoto mashuleni kwa lengo la kumaliza masomo kisha kujiajiri au kuajiriwa! Hii si sawa, dhana hii imepelekea watu kuwa na vyeo wasivyostahili! Dhana hii imepelekea wanafunzi kutozingatia elimu wanazopatiwa mashuleni, badala yake wanasoma ili kufaulu mitihani na si kujifunza!
Wananchi wanapaswa kuelimishwa kwamba elimu si kwa ajili ya kuajiriwa au kujiajiri, elimu ipo kwa lengo la kujifunza. Serikali itakapoelimisha wananchi juu ya hili, itasaidia kuondokana na dhana ya kwamba elimu ipo kwa lengo la watu kupata ajira, badala yake elimu ipo kwa lengo la kufunza.
(V) Serikali inapaswa kuwashika mkono vijana wenye vipaji, huu utakuwa msaada kwa vijana wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na hali duni ya kimaisha, kujiajiri kwa kutumia vipaji vyao na kupunguza wimbi la vijana wa mitaani.
Tafiti zinaonyesha kwamba vijana wengi wana vipaji lakini wanashindwa kuvitumia kutokana na kukosa sapoti. Mitaani kuna vijana wenye vipaji mbalimbali kama vile kuimba, kucheza, utunzi, utengenezaji wa vitu mbalimbali, n.k. Baadhi ya vijana wenye vipaji wamejikuta wanajiingiza katika makundi hatarishi kama vile ukabaji, uporaji mali, nk. Lengo kuu la kujiingiza katika makundi hatarishi ni kuweza kujikimu kimaisha.
Vijana hawa wangepata watu wa kuwashika mikono au sapoti kutoka serikalini, hakika wasingejiingiza katika makundi hayo! Serikali inapaswa kuweka mkakati wa kuwasaidia vijana wenye vipaji mbalimbali, hii si tu kwa faida yao, bali pia kwa faida ya nchi. Vijana wengi wana vipaji vikubwa ambavyo vingeweza kuitangaza nchi yetu, lakini wamekosa sapoti, wamekosa watu wa kuwashika mikono!
Nina Imani serikali ikifanya jambo kwa vijana hawa, si tu itawasaidia vijana hawa, bali pia itasaidia Taifa la Tanzania kupiga hatua kubwa na kujitangaza.
Mwisho
Nina imani Serikali ya Tanzania ni Serikali sikivu, na inayojali wananchi wake. Endapo Serikali itaamua kusikiliza na kutekeleza mawazo chanya kutoka kwa baadhi ya wananchi, hakika nchi yetu itajikwamua kwa kiasi fulani. Si tu wananchi watafaidika bali pia Taifa letu litapiga hatua zaidi.
Wananchi wanapaswa kupewa elimu itakayosaidia kubadili mitazamo hasi waliyoizoea, na badala yake waelimike na kubadilika kifikra ili kupunguza na kuondoa lawama dhidi ya Serikali tukufu.

Upvote
0