zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Kama ni hiki mbona Hitler alifanya zaidi ya haya kwa Raia wake je ilitosha kumfanya kuwa mtu mwema? Idd Amini je unajua kwamba uchumi wa Uganda ulikua vizuri kipindi Cha Amin kuliko hata baada ya kumpindua?? Inamfanya kuwa mtu mwema?Mimi binafsi, bila chembe hata moja ya unafiki, naamini kwa 98% JPM yupo Mbinguni pamoja na Malaika wa Mungu.
Watanzania, tutaacha lini kufikiri kipurure namna hiyo?
Ukweli ni kwamba, Rais legelege/ mtepetevu huua watu wengi mara mia zaidi ya Rais mwajibikaji kama alivyokuwa JPM.
Kwa maana hiyo, JPM katika uongozi wake ameokoa maisha ya watanzania wengi zaidi kuliko Rais yeyote yule ukiachana na Nyerere.
Maeneo ambayo JPM ameokoa maisha ya watanzania wengi ni kama vile:-
1. AJALI ZA BARABARANI.
Ajali za barabarani ambazo zilikuwa zikigharimu maisha ya watanzania wengi zilikwisha kutokana na uongozi shupavu wa JPM.
2.VIBAKA MITAANI.
Vibaka mitaani walikwisha kutokana na Askari kufanya kazi kwa bidii wakiogopa kukutana na mkono wa JPM.
3.WAGONJWA MAHOSPITALINI.
Wagonjwa wengi mahospitalini wameokoa maisha yao kutokana na Madaktari kuacha uzembe kazini kwa kuogopa kukutana na mkono wa JPM.
Hayo ni maeneo machache tu niliyoyataja.
Kwa hiyo, Rais legelege/ mtepetevu hawezi kusimamia mambo hayo kwa nguvu zote na kusababisha kuzaliwa kwa majanga ya kila aina katika Nchi.
Majanga hayo ni pamoja na uzembe makazini, Rushwa, uonevu, wizi wa mali za umma, unyang'anyi, vibaka kutapakaa mitaani, utapeli, uhujumu wa mali za umma nk.
Hayo yote huleta madhara makubwa sana kwa Wananchi.
JPM alijitahidi sana kupigania hayo, hivyo, anakosaje kuingia Mbinguni?
Rais legelege anaweza asifike Mbinguni kutokana na kutoweza kuyasimamia hayo na hatimaye kusababisha madhara makubwa kabisa kwa Wananchi.
JPM anaweza kuwa kiongozi mzuri kwa waliokubalia uongozi wake ila kusema eti kujenga barabara ndio kupeleka mbinguni ni kupotoshana. Kama ukifanya yote hayo ila ulilala na mke wa mtu imakula kwako. Kama ukifanya yote hayo ukabariki mtu kumiminiwa risasi 16 then mbinguni utapasikia tu.