Familia inateseka sana. Nisaidieni natafuta Kazi, Kibarua

Familia inateseka sana. Nisaidieni natafuta Kazi, Kibarua

Wanaoropoka kuwa Morogoro au Mbeya ndiyo Kuna Maisha nafuu wanaishi mikoa hiyo au wanabwabwaja tu? Au huko ndiyo ataokota vyakula barabarani au Nyumba za kuishi zipo za bure au? Humu kuna watu wanawaza na kutoa ushauri kwa kutumia mata... Kwa Kweli..

Nimeshuhudia wadau wanatoka Morogoro wanakuja kuanza upya Dodoma..halafu Kuna Mtu yumo humu anasema nenda Morogoro kana kwamba kinachomtoa au alicholikosa Dodoma mikoa hiyo kipo mtaroni..

Shame on wote mliotoa uhauri huo
Nina kaa morogoro tena mvomero huku Kodi nalipa Self elfu 50 sijaona kwanini watu wanasemaga maisha ya Moro ni mepesi sijui wanatumia akili gani kuongea hivyo.

Wakati sehemu ninayoishi na mjini naul 1000 bado chakula ni cha kununua
 
Afadhali umepata mwanamke mvumilivu, angekuwa mwingine tayari ungekuta kisha leta nguo za mabwana zake wahamie kwako.

Ukipata hela usije ukamsahau mkeo
Siyo mvumilivu, unadhani mwanamke mwenye mtoto mchanga ataenda wapi lazima awe mpole tu. Mungu ni mwema utavuka.
 
Habari wana JF,

Mie kijana wa kiume, naishi Dodoma! Nina mke na mtoto mchanga wa miezi 4. Kitaalum ni muhitimu wa Bachelor ya Computer Science, na nilikuwa nimeajiriwa sehem lkn tulipunguzwa kipindi kile janga la corona limepamba moto.

Sina kazi maalum kwa muda sasa, naunga unga tu kiukweli, nikibahatisha kupata kazi ya mtu binafsi mfano kutengeneza website au la kidogo imekuwa ikinibeba hasa kulipia kodi, lkn sijapata hizo kazi kitambo sasa! nimejaribu sana na bado naendelea kutuma maombi lkn sijafanikiwa, hali imekuwa ngumu kweli kweli kwetu! Nafanya vibarua sometimes hadi vya kubeba zege japo tu familia ipate mlo hasa mke anaenyonyesha!

Lakini saa nane kasoro hii usiku naandika hapa, tumelala njaa, leo nimejaribu vibarua bila mafanikio, hatuna hata sh. mia hapa ndani, imeniuma sana ndio maana nimekuja kwenu kuomba kazi, kibarua chochote halali hata cha kipato kidogo tu!

Mtoto wa miezi minne imebidi tu aanze kunywa uji maana mlo wetu mmoja kwa siku mama anakosa maziwa ya kutosha!

Mwenye chumba kanivumilia hadi kachoka kaniambia nikabidhi tu chumba, japo hii laptop naitumia kwa kazi zangu, lakn kama kuna mteja wana JF naiuza laki3, au kama kuna mtu anakopesha niiweke bond, atunusuru tafadhalini tunatolewa kwenye hii nyumba!

Nipo tayari kuja popote kufanya kazi/kibarua chochote halali! Naombeni sapoti nateseka sana, hasa huyu mzazi kulala njaa hivi inanipa stress sana!

Kwa mawasiliano, namba zangu 0767 960 255 au 0629 531 358.

Natanguliza Shukrani na Mungu atubariki!
Pole sana ndugu yangu na kijana mwenzangu pambana wewe ni jembe, don't give up.
 
Achana na mambo ya kanisa mkuu. Unapoteza muda bure kwa mambo ambayo hayana uhalisia.

Pambania kombe dingilai.
Hapa unatafuta vita mkuu, umempa ushauri mzuri tu. Lakini haya mambo ya imani ni mzoea sio rahisi mtu kuyakwepa.
 
Hapa JF ni mengi yametupata. Unampeleka mtu kwa mnaoheshimiana unakuta ni mbabaishaji au ni tapeli. Kabla ya kukubali kirahisi ukatapeliwa ni bora kujiridhisha. Unajua ukimuudhi mtu ndipo unamjua. Mfano akina kibatala wakiwa mahakamani utasiki, wewe si ni kikojozi, unahamaki - hapo ndipo ukweli unautoa. Tunafaa kuwa waangalifu maana unaambiwa kosa si kosa ila kurudia kosa. Nadhani angalau wenye akili za kiutu uzima wamenipata.
Bado haujafunguka, umewahi kumpeleka wapi Samweli aka Liverpool???
 
Back
Top Bottom