Familia mbili zagombania kuzika maiti ya mume wao

Familia mbili zagombania kuzika maiti ya mume wao

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Taharuki kubwa imeibuka nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure baada ya familia mbili kuzua sintofahamu kwa kugombania mwili wa marehemu Wambura Mwita Mampya, huku kila upande ukidai kuwa una haki ya kuandaa na kusimamia mazishi yake licha ya madai kuwa marehemu aliacha wosia unaoeleza mahali alipotaka azikwe endapo umauti utamfika.

Mke mkubwa wa marehemu amesema anaamini kuwa ana haki ya kushiriki na kusimamia mazishi ya mume wake, akieleza kuwa ndoa yao ilikuwa halali na hivyo haoni sababu ya kuzuiwa kushiriki taratibu za mwisho za kumuenzi marehemu.

Kwa upande wake, Kaka wa marehemu amesema Wambura Mwita Mampya aliacha wosia kabla ya kufariki akieleza kuwa endapo angefariki dunia angependa kuzikwa akiwa upande wa mke mdogo. Amesema uamuzi huo ulitokana na mgogoro uliodumu kati ya marehemu na mke mkubwa, ambao kwa mujibu wake haukuwa umepatiwa suluhu hadi wakati marehemu anafariki dunia.
 
Utakuwa "wosia" wa maneno tu siyo official document yaleyale ya Edgar Lungu.

Wabongo na wosia wapi na wapi?
Lungu alikosea wapi,mbona familia imeshinda kesi na anazikwa South kama Wosia wake usemavyo.
 
Ndoa yao ni ya kanisani, msikitini, bomani ama kimila ? Na ndoa ya mwanzo ilikufa kwa case ni ndoa ya mke mmoja ?? kama ni ya wake wengi vipi wosia unaeleza nn ?

Vipi Kuna mali?? Walogane tuu ukerewe sio mbali
 
Back
Top Bottom